Unaweza kutupa ushahidi wa bandiko la gazeti au barua au tangazo la katazo la watu kutokutazama tv?
Nikukumbushe tu miaka hiyo hakukuwa na vyombo vya habari kama sasa ila kuna watu walikuwa wanafunga madishi makubwa sana kuvuta mawimbi ya television,wengine walitumia antena. Ila ilikuwa ni nadra sana kukuta nyumba zina television.
Hakukuwa na katazo ila ni mawazo ya watu wa nyakati hizo kama hivi sasa baadae kuna watu watakuja kusema miaka ya 2025 serikali ilikataza watu kumiliki magari ya kimagharibi ya bei kali kama Ferrari, Bugatti, Aston Martin, etc kwasababu tu miaka yao hayakuwapo kwa wingi Tanzania na watu hawakuwa wakiyanunua.
Watu waongo waongo kila enzi huwa hawakosekani.