Kwanini na kuna siri gani katika wewe kuchagua siku yako ya kuzaliwa?

Kwanini na kuna siri gani katika wewe kuchagua siku yako ya kuzaliwa?

Rachel P

Senior Member
Joined
Dec 26, 2024
Posts
151
Reaction score
617
Kwa jamii nyingi duniani, kiumbe huhesabiwa ya kwamba kipo hai pale kinapozaliwa na kuonyesha dalili za kwanza za uhai. Lakini ipo mijadala dunia nzima kuhusiana na uhai wa mimba.

Kwamba mimba ihesabiwe kama kiumbe hai au isubiriwe hadi uzazi ndipo ipewe haki ya uhai.

Lakini wote wanaojadiliana hapo wanasahau siri kwamba mimba hii ilikuwa hai hata kabla ya kutungwa.

Ipo hivi,
Wakati inapotungwa mimba manii hubeba viumbe hadi zaidi ya milioni 10 ambavyo hutarajiwa kimoja au viwili kwa hali ya kawaida au zaidi ya vitatu katika hali isiyo ya kawaida KUCHAGUA kuwa hai katika tarehe fulani miezi 9 baadae.

Yaani kwa kila binadamu unayemuona, tambua kwamba aliibuka mshindi katika shindano na wenzie zaidi ya milioni 10 na akachagua kuzaliwa katika tarehe fulani miezi 9 baadae.

Hii inathibitisha kwamba binadamu huyu alikuwa hai kabla ya kutungwa kwa mimba yake, na ALICHAGUA kuwa wa kuzaliwa katika tarehe hiyo atakayoamua yeye kutoka katika tumbo la mama yake miezi 9 (au 10 au 8 au 7) mbele.

Uchaguzi wa HIYARI
 
Uchaguzi huu wa HIYARI huamuliwa na nguvu ya uhai iliyomo ndani ya kiumbe huyu mdogo mwenye siha zote za kuwa binadamu endapo tu atapatiwa host wa kumbeba katika mazingira anayoyataka yeye (mji wa mimba) hadi ifike hatua anapojiona hahitaji tena host na anaweza kujisimamia mwenyewe katika vichache vya muhimu kati ya vingi visivyo na umuhimu.

Ni wazi kwamba maamuzi ya kiumbe huyu kuwa hai yalifanyika hata kabla hajatengenezwa kuwa manii yenye nguvu (alpha) kuwashinda wenzie zaidi ya milioni 10 ambao wanapoteza chance hiyo ya kuwa hai.

Kisha kiumbe huyu mpya anakuwa na maamuzi ya jinsia yake, haiba yake na hata maisha yake kutegemea host na hata baada ya kuachana na host.

Haya yote yanahitaji hekima na ujuzi wa mengi ili kufanikisha kila hatua.

SWALI LINAKUWA kwa nini kiumbe wewe ulichagua kuwa hai leo kwa kutumia tarehe ile uliyoingia kwa host na kuchagua tarehe ile uliyoamua kutoka kwa host?

Hakuna jambo linalotokea kwa bahati mbaya katika ulimwengu huu.

KILA JAMBO HUPANGWA NA MATOKEO HUJULIKANA KABLA
 
Kwa kuwa matumizi ya kalenda na saa ni maendeleo yaliyokuja baadae kupitia wanadamu.
Viumbe wale wadogo ambao hawajatungwa mimba bado, huitumia mizunguko ya dunia, jua, mwezi na sayari mbalimbali ili kufahamu majira na nyakati zinazofaa au ZISIZOFAA wao kuingia kwa host na kuwa mimba.
Yaani kwa kufuatisha mirindimo ya matufe hayo makubwa, viumbe hao HUCHAGUA nyakati zao BORA ZAIDI za kuchukua mwili na kuitwa binadamu (au hayawani yeyote).
Kisha huchagua wazazi (host) na jinsia.
Maana yake, wewe ulichagua vinavyokuhusu sasa na vijavyo siku ulipochagua tarehe yako ya kutungwa mimba kwa kuangalia mivutano (gravitational pull) kati ya dunia jua mwezi na sayari zote zinazofikisha mivutano yake duniani (micro-gravitational pulls).

Hivyo hiyo inatupatia taarifa kwamba ulikuja na survival plan ambayo ndiyo chimbuko la uchaguzi wako. Yaani life purpose.

KWA MFANO
Tujaribu kumchunguza kiumbe aliyechagua kutungwa mimba labda tarehe 10 september na kuzaliwa wiki 36 mbele (miezi 9).

Kiumbe huyu ...
 
Sperm sio binadamu bado.

Kabla ya mimba kutungwa hakuna kiumbe wala binadamu. Kuna mbegu za kiume na Yai la kike.

Hakuna kiumbe wala binadamu.

Hakuna kiumbe au binadamu aliyechagua siku yake ya kuzaliwa.

Kati ya mbegu na yai kimoja kipo hai tayari na kimeshapata umbo na KIMEFANYA MAAMUZI kabla ya kukubali kutungwa
 
...Mkuu wa itifaki Rachel p, Hongera kwa uzi mzuri lakini umeandika kwa knowledge yako sio katika dhana ya uhalisia ya uumbaji.

Hakuna mtu aliyechagua kuja duniani, Wala kuchagua tarehe au jinsia, na shahawa sio mtu.
Mungu pekee ndo anayepanga Nani azaliwe kesho , mwezi ujao, mwakani, au baada ya miaka 10.
 
Hata twazungumzia BEFORE birthday.
"SWALI LINAKUWA kwa nini kiumbe wewe ulichagua kuwa hai leo kwa kutumia tarehe ile uliyoingia kwa host na kuchagua tarehe ile uliyoamua kutoka kwa host?"

Hapo umemaanisha nini?
 
"SWALI LINAKUWA kwa nini kiumbe wewe ulichagua kuwa hai leo kwa kutumia tarehe ile uliyoingia kwa host na kuchagua tarehe ile uliyoamua kutoka kwa host?"

Hapo umemaanisha nini?

Kwa sababu mimba ni KIUMBE HAI huwa inakuwa na maamuzi ya kuanza na pia kumaliza. Yaani yule mtoto ndio huwa anasema nataka kuzaliwa NIMESHAKUWA. Na sio maamuzi ya mama mjamzito wala baba mtoto
 
Kwa sababu mimba ni KIUMBE HAI huwa inakuwa na maamuzi ya kuanza na pia kumaliza. Yaani yule mtoto ndio huwa anasema nataka kuzaliwa NIMESHAKUWA. Na sio maamuzi ya mama mjamzito wala baba mtoto
Mama anaweza kuamua hasa km anazaa kwa operation. Ile tar ya kujifungua anaweza kuisogeza mbele siku kadhaa au wiki
 
Back
Top Bottom