Kwanini na kuna siri gani katika wewe kuchagua siku yako ya kuzaliwa?

Kwanini na kuna siri gani katika wewe kuchagua siku yako ya kuzaliwa?

science inasema kua, ile zygote ( yai lililo rutubishwa ) baada ya mimba kutungwa katika ile miezi ya mwanzo kabisa, inafanana sana katika kingdom animalia yote

yaani kijusi ( zygote ) ya binadamu, simba, ng'ombe, mbuzi, kuku etc zinafanana sana

kadri muda unavyoenda ndo vinazidi kutofautiana na kupata muonekano halisi wa kiumbe husika,

pia siku hizi mimba inaweza kutungwa nje ya mfuko wa uzazi na nje kabisa ya mwili yaani maabara

pia ile zygote inapokua bado na seli chache inaweza kugawanyishwa na kila moja ikaendelea kukua na ikawa kiumbe

pia kuna uwezekano wa kufanya cloning na kuzalisha kiumbe kutokana na seli fulani za kiumbe husika.

miezi tisa ni kipindi tu cha ukuaji ambacho baada ya yai kurutubishwa linakua limefikia kua kiumbe kamili anayeweza kuishi nje ya mwili ( kwa binadamu ) kila kiumbe kina muda wake wa development
 
Rudia tena taratibu. Vipo wazi
Hapana. Havipo wazi kwani umechanganya Biological facts na Nadharia zilizokuwepo zamani (Darwinism) na Unavyodhania wewe. Hapo lazima msomaji wako atashindwa kukuelewa unaleta hoja gani. Umechanganya aina Tatu (3) za mtizamo kwenye mada moja. Hebu rudia kuisoma vizuri mada yako halafu uone kama ina Logic. (Samahani lakini).
 
HAPANA.

Mbegu ina kichwa kiwiliwili na mkia na ina uwezo wa kuogelea kwenye majiuke kulitafuta yai.
Lakini bado sio kiumbe.

Mbegu kuwa na kichwa, kiwiliwili na mkia sio kigezo cha kuitwa kiumbe.

Bado ni mbegu tu.
How amazing!
Kabla ya muunganiko wa mbegu ya kiume na yai la kike, Hakuna kiumbe.
 
Mbegu huitaji mazingira (udongo) ili kumea.

Lakini mazingira hayahitaji kumactivate mbegu. Mazingira hayako hai.

Mbegu ndipo chimbuko la taarifa ya kwanza ya uhai inakotoka.

Yaani mbegu ya Baba Rachel ina taarifa zote za Rachel na baba yake huku yai linakuwa supporting environment
 
Ni kweli kabisa, lakini vyote ni hai

Ok. Tuseme ni hai kwa kuwa tafsiri ya uhai iko compressed.

Ukidecompress tafsiri ya uhai utagundua hadi mate yako yapo hai.

HADI KUCHA ZAKO.

Kasoro simu yangu.

Lakini hapa tunajadili uwezo wa kuamua na kuchagua kuliko uwezo wa kumiliki uhai.
 
Sijaona shida Kwa watu kuitambua siku ya kuzaliwa kwani ndio siku ambayo watu walitambua uwepo wako.
Kule tumboni/kwenye manii kweli uhai ulikuwepo lakini Bado ufanano au taswira yako ilikuwa imejificha.
Na pia uhakika kuwa kweli utavuka mipaka ya tumbo na kuja nje huku unakuwa nusunusu
 
Science and spiritism are neither differing nor two things.

Science finds practical answers to spiritual questions.

Couples!!
sijaelewa inakuaje sperms " kiumbe " according to you zinachagua host, zina interfere with your conscious na kufanya uchague nani wa kushiriki naye au miongoni mwa unakutana nao ndo zinachagua, vipi ikitokea mbegu za pande mbili zimekutana na "kiumbe" hakijampenda host inatokea nini miscarriage au
 
K
Kwa jamii nyingi duniani, kiumbe huhesabiwa ya kwamba kipo hai pale kinapozaliwa na kuonyesha dalili za kwanza za uhai. Lakini ipo mijadala dunia nzima kuhusiana na uhai wa mimba.

Kwamba mimba ihesabiwe kama kiumbe hai au isubiriwe hadi uzazi ndipo ipewe haki ya uhai.

Lakini wote wanaojadiliana hapo wanasahau siri kwamba mimba hii ilikuwa hai hata kabla ya kutungwa.

Ipo hivi,
Wakati inapotungwa mimba manii hubeba viumbe hadi zaidi ya milioni 10 ambavyo hutarajiwa kimoja au viwili kwa hali ya kawaida au zaidi ya vitatu katika hali isiyo ya kawaida KUCHAGUA kuwa hai katika tarehe fulani miezi 9 baadae.

Yaani kwa kila binadamu unayemuona, tambua kwamba aliibuka mshindi katika shindano na wenzie zaidi ya milioni 10 na akachagua kuzaliwa katika tarehe fulani miezi 9 baadae.

Hii inathibitisha kwamba binadamu huyu alikuwa hai kabla ya kutungwa kwa mimba yake, na ALICHAGUA kuwa wa kuzaliwa katika tarehe hiyo atakayoamua yeye kutoka katika tumbo la mama yake miezi 9 (au 10 au 8 au 7) mbele.

Uchaguzi wa HIYARI
Kwani mkuu hiyo mbegu inayopata ushindi wa riadha kwenye 'womb', huwaga siyo hai mpaka ipate kwanza ushindi wa kutungiwa mimba?

Je washindani wenziye wanaoshindwa na kupoteza sifa, hufanya mashindano hayo bila ya kuwa hai?

Nimeuliza hayo kutokana na namna ulivyojenga hoja yako, vinginevyo usahihishe hoja kwa kujibu maswali haya.
 
Sijaona shida Kwa watu kuitambua siku ya kuzaliwa kwani ndio siku ambayo watu walitambua uwepo wako.
Kule tumboni/kwenye manii kweli uhai ulikuwepo lakini Bado ufanano au taswira yako ilikuwa imejificha.
Na pia uhakika kuwa kweli utavuka mipaka ya tumbo na kuja nje huku unakuwa nusunusu
Nanukuu: "Kule tumboni/kwenye manii kweli uhai ulikuwepo lakini Bado ufanano au taswira yako ilikuwa imejificha".
Hii dhana 👆 👆 bado haijapata Hitimisho kisayansi kwani manii(Sperms) ina 23 chromosomes na yai lina 23 chromosomes ili kukamilisha binadamu ambaye huwa ana 46 chromosomes. Kwa mantiki hiyo, ina maana kabla manii na yai havijakutana (Fertilization) huyo sio mtu ila ndo malighafi ambayo kwayo mtu hufanyika/huumbika.
Lakini bado hoja inakuja kwamba, kwa wanasayansi na wasomi nguli, bado upo utata kwenye hoja hiyo kwa sababu sperms huonekna kutembea na yai kujisogeza na kujilengesha kwenye mirija ya uzazi(Fallopian tubes) kitu ambacho ni Tabia ya viumbe hai kwamba je, UHAI unaanza saa ngapi, halafu kwa nini sperms ziwe mamilioni ilhali inatakiwa moja tuu na mwanamke hupoteza yai moja kila mwezi kana kwamba sio kitu cha maana kivile. (It is a controversial issue)
 
Mkuu hoja yako ipo sahihi,ila nilijibu vile Kwa hoja ya mtoa mada aliyejaribu kuhoji juu ya ipi siku sahihi ya kuikumbuka kati ya kuzaliwa au uhai ulipoanzia.
Mfano,je hivi ni sahihi kuadhimisha siku hai lilipokutana na sperm katika mrija wa fallopian?au siku yai lilipotungwa na sperms kutengenezwa?
 
Back
Top Bottom