Kwanini naamini Putin ni Pandikizi la Marekani nchini Urusi

Kwanini naamini Putin ni Pandikizi la Marekani nchini Urusi

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
1: Alichoamua kukifanya angeweza kushambulia tu maeneo ya kimkakati kuonyesha hakubaliani na Ukraine kujiunga na NATO bila kuingiza jeshi lote. Amefanya makusudi, Russia ipigwe vikwazo uchumi udolole nchi ikoswe kutawalika Russia ivunjike vipande na US awe Superpower Wa Muda wote ili kutimiza ajenda vificho za waovu Wa dunia hii.

2: Zamani nilijua hawa jamaa ni maadui hadi vita vya Syria. Wakati marekani inataka kushambulia eneo ambalo nilikuwa na makomando na majeshi Wa kirusi Syria, kwa mujibu Wa mitandao ya kijajusi Urusi walitaarifiwa kwa channel maalumu, kisha wakahamisha majeshi ili marekani ipige inapotaka. Hawa maadui gani ambao wanajeshi wake wanapeana habari za kutoathiriana?

Hivyo kwa akili na uchambuzi wangu Wa darasa la Saba la mkoloni , tujikite kwenye matoleo ya hii vita. Kuna kitu kikubwa kinatengenezwa ambacho kitabadili gia ya safari ya sayari dunia.

Yangu ni hayo.

Ila nawapongeza maana vita hivi vimekuwa sababu ya dunia kupewa likizo isiyo na matibabu ya korona
 
Putin hana ushirika wowote na USA na ni mpingaji mzuri sana wa Sera za America hususani ushoga. Putin ni mzalendo wa kweli wa nchi yake na zaidi ya yote anaipenda sana Urusi kuliko anavyojipenda yenyewe.

Putin anachofanya ni kukamilisha unabii wa Ezekiel 38 na 39 na zaidi ya yote yanayoendelea ni kukamilisha nabii zilizowahi kutolewa.
 
Sawa, mkuu. Lakini kwa maoni yangu sidhani kama Putin atakuwa pandikizi la Marekani, kwani nakumbuka kipindi fulani Marekani walitaka kuivamia Korea ya Kaskazini, Putin akawaambia Wamarekani kuwa, wafanye chochote kile juu ya Korea ya Kaskazini lakini si kuivamia.
Baada ya kuambiwa hivyo, Marekani waliufyata.
 
Ni kawaida watu ku share taarifa za kiintelejensia pale ambapo shughuli moja itamuaffect mwengine kuepusha migongano
 
Nimeishia hiyo hoja ya kwanza, chini sijasoma, nadhani utapata jibu nililowaza juu yako.

Tchao.
 
Nitaisoma kila siku mpaka niielewe hii thread
Nalog off
 
Hio Ni kawaida kwa nchi kubwa zenye uwezo mkubwa kijeshi. Hupeana taarifa ili kuepusha direct conflict..
Usichojua hata Israel pia hutoa taarifa kw Rusland juu y mashambulizi katikA Syria
 
Back
Top Bottom