Kwanini naunga mkono tozo

Kwanini naunga mkono tozo

Hapa US kuna watu wanaosema ni kwanini serikali inatoa misaada nchi nyingine wakati kuna ombaomba wengi na watu wasio na nyumba? Hii ni mifumo na hatuwezi kukubaliana na kila kitu wangekubaliana na hawa tusingepata $600M kama msaada kutoka US wa Afya miaka miwili iliyopita
Kumbe upo US halafu unaongea ujinga namna hii.

Unaleta stori za kufikirika kwakua upo mbali na moto.

Tulio kwenye chungu ndio tunajua maumivu yake.
 
Nakubaliana na wewe lakini tujue tu hizi ni tozo mpya na serikali inahitaji muda kuonyesha kimefanyika nini. Hatutaweza kujua kwasasa manufaa ya uwekezaji kwenye kilimo cha umwagiliaji wakati hata tozo na uwekezaji haujafanyika. Lakini kwenye hizi tozo tujiulize mfano hayo makato ya kibank na yale ya simu ambayo yapo je viwango vilikuwa halisi au walikuwa nao wanaweka juu sana?. Bank mfano ATM fees tunajua pesa yote hiyo ni ya nini wakati mifumo ya pesa ni rahisi na bank kuu inafanya kila kitu
Huwezi kuhoji gharama wanazo kata benki kwa ajili ya kukutunzia pesa yako. Watumishi wa benki wote, pango, bili za umeme na maji, mifumo wanayotumia, vyote hivyo vinalipiwa na mgharamiaji unapaswa kuwa wewe muweka fedha.

Tozo ni aina fulani ya kodi ya kichwa, maana haijalishi umeingiza kipato au hujaingiza, ili mradi unamiliki laini ya simu na unajaza salio basi utalipa labda uwe hufiki ile threshold ya kukatwa tozo. Tozo si jambo baya kabisa provided viwango ni affordable na havishawishi watu kuvikwepa au kuvichukia. Pia tozo ikielekezwa kwenye mambo mahususi yanayozalisha ajira kwa mtanzania, ndani ya miaka 10 ijayo kila mtu atashuhudia faida za tozo.
 
tatizo sio tozo wala hizo Kodi ila tatizo kubwa la Tanzania ni MATUMIZI ie yaani hata kama tutaongeza/tutaweka Kodi na tozo kwenye kila kitu ila hakuna nidhamu ya matumizi ni kazi bure
20220903_092128.jpg
20220610_094227.jpg
 
Kwanza tuweke mambo sawa tozo ni aina ya kodi. Hivyo tusiongelee tozo kama vile sio kodi.

Mimi binafsi sijaona ubaya wowote wa serikali kuweka tozo na nina fikiri hakuna njia nyingine kwa wakati huu zaidi ya tozo na nitajaribu kuweka hoja hapa vizuri. Tanzania kama nchi inayoendelea inahitaji pesa ili iweze kuwekeza kwenye miradi mingi sana kuanzia elimu, maji, barabara, umeme, kilimo, ulinzi.......n.k

Sasa vyanzo vya mapato ni hivi
  1. Missada kutoka nje
  2. kodi na tozo
  3. mikopo
Tanzania tumeshakopa na bado tutaendelea kukopa kama tutapata mikopo nafuu lakini vilevile tunakusanya kodi mbalimbali. Lakini ukiangalia vizuri budget zetu pesa ya kodi ambayo haitoshi hata kwenye budget bado inaenda kwenye shughuli ambazo sizo za kimaendeleo hivyo sio uwekezaji wa nchi bali ni matumizi. Kuna miradi tunalipia kwenye kodi kama ya maji na umeme lakini wakati wa Kikwete pesa karibu yote ilikuwa ni kulipa mishahara na matumizi ya serikali.

Sasa kama nchi tuko kwenye kipindi cha uwekezaji kwa mara ya kwanza tunaanza kuona barabara za kisasa, shule bora, hospitali na umeme hasa vijijini. Sasa tumefikaje hapa ? Ni kuwekeza kwa kodi mpya na tozo. Umeme mfano wa vijijini umepelekwa na tozo maalamu kwenye luku za nyumbani na barabara za vijijini nyingi zinatengenezwa na tozo kwenye mafuta. Lakini ili kama nchi tuweze kuwekeza na kuongeza walipa kodi ni lazima tuwekeze kwenye kilimo. Kilimo kitaongeza mapato kwenye kodi lakini tatizo hatuna mfumo mzuri wa kilimo kuwa na uazalishaji wa uhakika. Bashe amekuja na mpango mzuri wa kuongeza uzalishaji kwa kufanya yafuatayo (1) Serikali itatoa ruzuku kwenye mbolea (2) Serikali itawekeza kwenye umwagiliaji (3) watatoa mbegu (4) watafuta wawekezaji wa viwanda (5) kutafuta masoko. Hii ndiyo mojawapo kubwa ya kuongeza ajira na kodi lakini mtaji wa yote haya ni karibu Trillion moja sasa mtaji unatoka wapi? Hii ndiyo sababu imeenda kwenye tozo hivyo tozo ni muhimu kwasababu ni mtaji wa uhakika wa kuongeza kodi kwa miaka ijayo. Lakini ni tukiangalia vizuri tatizo letu ni utamaduni mbovu watu wengi walizoea kukaa bila kulipa kodi wala tozo

Mimi ni diaspora wa muda mrefu sana na naishi na kutafuta maslahi yangu jimbo la Texas. Hili jimbo letu linajulikana kwa kuwa na kodi ndogo lakini ngoja niwape data kidogo ili mgundue tonavyolipa kodi.

  • Nyumba kila mwaka nalipa 3% ya thamani ya nyumba. Hivyo kwa mfano kama nyumba pale Tanzania yenye thamani ya Tsh 100,000,000 basi unatakiwa kulipa kila mwaka Tsh 3,000,000. Hakuna mjadala kwenye hili na usikolipa unapekwa mahakamani na nyumba inapigwa mnada
  • Jumuia na majiradi vilevile wana kitu kinaitwa HOA-Housing Owners Association hii ni jumuia ya makazi yako na majirani kila nyumba inalipa $350-$1000 kwa mwaka kwa usafi wa jumla kama kukata majani na kusafisha mitaro. Hii ni nje ya nyumba yako hii nayo ni lazima na kisheria wanaweza kwenda na utaratibu mpaka wakapiga mnada nyumba
  • Tuna tozo za maji na kuchukuwa taka. Kila wiki wanapita kuchukuwa taka kwenye magaloni maalumu. Hii inafanywa na manispaa huwezi kuchoma matakataka ovyo ovyo. Maji unalipa kutokana ma matumizi lakini taka utalipia unataka au hautaki jumla sio chini ya $100 kila mwezi. Ukitupa uchafu ovyo ni faini, usipoweka uchafu vizuri kwenye mifuko ni faini....
  • Barabara nyingi zinajegwa kwa mikopo inayoitwa goverment bonds hivyo ni lazima ilipwe. Kila nikienda kazini kwa mfano ni lazima nipitie kwenye barabara za kulipia "toll roads" na natumia sio chini ya $5-$7 kwenda kwa siku moja na kurudi. Tena hii ni rahisi New York wanatumia $12-$15.
  • Ukienda kwenye hotel na kokodi chumba karibu 35% ni kodi na tozo, kwenye simu, cable za TV au Dish hivyohivyo
  • Kwenye super market kila ukinunua kitu kuna 5% ya tozo inaenda kusaidia “Metro" ambayo ni kama mwendo kasi yetu.
  • Lakini hapa kuna bima ya karibu kila kitu nyumba ni lazima uwe na bima na kwenye hizi bima kuna pesa zinaenda kusaidia idara kama Zimamotto... na ambulance
Hapa sijaongelea tozo na kodi za mishahara. Lakini mjue hapa bado tuna nafuu sana kulinganisha na nchi za Ulaya au Canada ambako Tozo na kodi zipo juu sana. Familia yangu ina bahati tuna nyumba Uninio sehemu ambayo ina thamani sana lakini kodi zetu pale hazifiki hata 1% ya thamani wakati bodaboda wanalipa kodi kwenye mafuta. Hivyo kuna sehemu kiukweli wanaonufaika ni matajiri tu kusema ukweli.

Kuna ambao watasema huko Ulaya na US pesa inaonekana ni kweli tuna shule kwenye kila mtaa za watoto zina mabasi na ni bure lakini tunalipa 3% kwenye thamani ya nyumba na pesa inaenda huko. Hivyo hoja ni yaanze mayai au kuku lakini kodi ni muhimu na maendeleo ni muhimu. Ndiyo maana hoja yangu ni kwamba tozo ni muhimu kwasababu ni mtaji na utaratibu mpya wa kuongeza wigo la walipa kodi na kuweka mifumo ya kimaendeleo. Tatizo kubwa ni mazoea ya watu wengi walikuwa wamezoea kukaa bila shughuli na kubangaiza lakini kama tunataka umeme vijijini, barabara za lami na hospitali ni lazima zitengenezwe, kuwe na pesa za matengenezo kila mara na pesa za wahudumu. Ni lazima kuwe na mfumo wa mapato na wananchi ni lazima wazalishe ili waweze kuwa na mifumo hii. Huwezi kukaa kijijini hulipi kodi yeyote, huzalishi chochote halafu unahitaji barabara, maji, umeme ... pesa inatoka wapi? Ni lazima serikali iwekeze kwenye kilimo ili wewe mwanakijiji uweze kuchangia kodi na maendeleo na ndicho kinacho fanyika kwa sasa
Kwanza kabisa umesema unaishi Texas, hilo ni moja ya majimbo huko Marekani. System ya maisha ya marekani ni ya kuthamini utu. Huwezi fananisha na system ya bongo kila mtu anajijali yeye kwanza wengine mtajiju.

Katika mazingira ya maisha tu ukiwa Texas sitegemei utakuwa umetenga meza barabarani ukinadi sidiria za mtumba ama ukiuza supu ya pweza hapo.

Odds are that you are going to be having a decent job ambayo inakuwezesha kulipa hio 3% ya nyumba kwa mwaka, internet bills, water bills, electricity bills, road tolls. What you earn inaweza kuwa $3OO-$5OO on a daily basis na huenda matumizi ya siku ni only 1O% of what you earn. Unafikiria ungekuwa unauza supu ya
pweza mngejenga mbweni.

Kimsingi mnaweza ona mnakamuliwa ila by the end of the day hela unaiona kama unafanya kazi kweli. Maendeleo ya huko sio kitu cha kuuliza, transparency is there juu ya Taxes na tozo zinakwenda wapi.

Bongo mshahara laki 7 makato na tozo yanaweza fika asilimia 4O% ya salary. Mshahara ni huo huo toka mafuta yanauzwa 2,344 hadi sasa ambako mafuta yamefika 3,41O. Vitu vimekwea gharama sokoni by 5O% same salary.

Katika wakati huo huo Tozo zinakuwa introduced ili unategemea hali itakuwaje? Wanao impose tozo wao hawaishi kwa laki 7 kwa mwezi! They make 1O or more times the amount in their salaries bila kusahau ni kuwa wanakuwa covered na premium health insurance ya familia nzima,Communication and Transport allowance iko na ni unlimited. Its almost mishahara yao haitumiki kuendeshea maisha yao sababu wana acess ya maposho mlima.

Hivi watu wa aina hii wanawezaje kuwa na uchungu na wananchi wanaokwazika na tozo? Yani mtu anayeishi kama yuko peponi anakuwazaje mtu wa motoni?
 
Naimba kujua au kupata elimu kidogo hapa...Msaada kutoka nje na mkopo unatofauti gani..? Isn't the source the same "person"...?
Grant - Is a benefit from a donor country termed as a gift that we are never liable to repay be it monetary or

Loan- Is a monetary benefit from a financial institution that we are liable to
repay it in accordance to the agreed terms.
 
Thanks for the clarification.
Spot on!
 
Nakubaliana na wewe lakini tujue tu hizi ni tozo mpya na serikali inahitaji muda kuonyesha kimefanyika nini. Hatutaweza kujua kwasasa manufaa ya uwekezaji kwenye kilimo cha umwagiliaji wakati hata tozo na uwekezaji haujafanyika. Lakini kwenye hizi tozo tujiulize mfano hayo makato ya kibank na yale ya simu ambayo yapo je viwango vilikuwa halisi au walikuwa nao wanaweka juu sana?. Bank mfano ATM fees tunajua pesa yote hiyo ni ya nini wakati mifumo ya pesa ni rahisi na bank kuu inafanya kila kitu
Tunachotaka kuju tozo ni kiasi gani inakusanywa na
Impact yake ni kwa kiwango gani. Haitoshi tu kusema tozo zimejenga zahanati. Wakati hawatoi takwimu kuwa tozo makusanyo ni kiasi gani.

Hapo kinachofichwa ni ufisadi tu sio kingine. Kama budget yetu ikibanwa vizuri kodi ikaelekezwa kwenye mambo ya msingi na sio matumizi na wizi basi tunahitaji miaka michache sana tu ya kubadili nchi.

Matumizi mabaya ya tozo na kodi ukichanganya na usiri wa takwimu za makusanyo tutaendelea kuwa hivi hivi sababu watu watajichotea mihela gizani.
 
Bandiko refu harafu unaarisha Arisha utumbo WA nguruwe..........umezoea kukatwa katwa Tu ndio maana uoni maumivu yake........Sisi tunaomba Tu Kwa the most high atusaidie kuondoa nyie chawa na kunguni pale jumba jeupe mrudi kwenu kwenye masanduku
 
Tunachotaka kuju tozo ni kiasi gani inakusanywa na
Impact yake ni kwa kiwango gani. Haitoshi tu kusema tozo zimejenga zahanati. Wakati hawatoi takwimu kuwa tozo makusanyo ni kiasi gani.

Hapo kinachofichwa ni ufisadi tu sio kingine. Kama budget yetu ikibanwa vizuri kodi ikaelekezwa kwenye mambo ya msingi na sio matumizi na wizi basi tunahitaji miaka michache sana tu ya kubadili nchi.

Matumizi mabaya ya tozo na kodi ukichanganya na usiri wa takwimu za makusanyo tutaendelea kuwa hivi hivi sababu watu watajichotea mihela gizani.

Unaulizia tozo mpya au zilizokuwepo? Tuzo mpya ndizo zimeanza kukusanywa itachukuwa mwaka kujua. Pili ripoti ya CAG ndiyo kazi yake lakini watu wengi wanakuaga wana puuza hii ripoti halafu wanauliza kama wewe hapa. Vilevile Wabunge wetu wanatakiwa kuuliza huu ndiyo muda wa kwenda kwenye vikao vya jimboni kwako
 
Sidhani hata kama hizo tozo zinaingia hazina
 
Uliposema tu "Hakuna njia nyingne Kwa Sasa" nimeona unafikiria matako.Na wewe hufai kuwa kiongozi

Kiongozi unahitaji ubunifu wa njia mpya za mapato bila kuathiri Hali za wananchi.

Matako yako
 
Kwanza tuweke mambo sawa tozo ni aina ya kodi. Hivyo tusiongelee tozo kama vile sio kodi.

Mimi binafsi sijaona ubaya wowote wa serikali kuweka tozo na nina fikiri hakuna njia nyingine kwa wakati huu zaidi ya tozo na nitajaribu kuweka hoja hapa vizuri. Tanzania kama nchi inayoendelea inahitaji pesa ili iweze kuwekeza kwenye miradi mingi sana kuanzia elimu, maji, barabara, umeme, kilimo, ulinzi.......n.k

Sasa vyanzo vya mapato ni hivi
  1. Missada kutoka nje
  2. kodi na tozo
  3. mikopo
Tanzania tumeshakopa na bado tutaendelea kukopa kama tutapata mikopo nafuu lakini vilevile tunakusanya kodi mbalimbali. Lakini ukiangalia vizuri budget zetu pesa ya kodi ambayo haitoshi hata kwenye budget bado inaenda kwenye shughuli ambazo sizo za kimaendeleo hivyo sio uwekezaji wa nchi bali ni matumizi. Kuna miradi tunalipia kwenye kodi kama ya maji na umeme lakini wakati wa Kikwete pesa karibu yote ilikuwa ni kulipa mishahara na matumizi ya serikali.

Sasa kama nchi tuko kwenye kipindi cha uwekezaji kwa mara ya kwanza tunaanza kuona barabara za kisasa, shule bora, hospitali na umeme hasa vijijini. Sasa tumefikaje hapa ? Ni kuwekeza kwa kodi mpya na tozo. Umeme mfano wa vijijini umepelekwa na tozo maalamu kwenye luku za nyumbani na barabara za vijijini nyingi zinatengenezwa na tozo kwenye mafuta. Lakini ili kama nchi tuweze kuwekeza na kuongeza walipa kodi ni lazima tuwekeze kwenye kilimo. Kilimo kitaongeza mapato kwenye kodi lakini tatizo hatuna mfumo mzuri wa kilimo kuwa na uazalishaji wa uhakika. Bashe amekuja na mpango mzuri wa kuongeza uzalishaji kwa kufanya yafuatayo (1) Serikali itatoa ruzuku kwenye mbolea (2) Serikali itawekeza kwenye umwagiliaji (3) watatoa mbegu (4) watafuta wawekezaji wa viwanda (5) kutafuta masoko. Hii ndiyo mojawapo kubwa ya kuongeza ajira na kodi lakini mtaji wa yote haya ni karibu Trillion moja sasa mtaji unatoka wapi? Hii ndiyo sababu imeenda kwenye tozo hivyo tozo ni muhimu kwasababu ni mtaji wa uhakika wa kuongeza kodi kwa miaka ijayo. Lakini ni tukiangalia vizuri tatizo letu ni utamaduni mbovu watu wengi walizoea kukaa bila kulipa kodi wala tozo

Mimi ni diaspora wa muda mrefu sana na naishi na kutafuta maslahi yangu jimbo la Texas. Hili jimbo letu linajulikana kwa kuwa na kodi ndogo lakini ngoja niwape data kidogo ili mgundue tonavyolipa kodi.

  • Nyumba kila mwaka nalipa 3% ya thamani ya nyumba. Hivyo kwa mfano kama nyumba pale Tanzania yenye thamani ya Tsh 100,000,000 basi unatakiwa kulipa kila mwaka Tsh 3,000,000. Hakuna mjadala kwenye hili na usikolipa unapekwa mahakamani na nyumba inapigwa mnada
  • Jumuia na majiradi vilevile wana kitu kinaitwa HOA-Housing Owners Association hii ni jumuia ya makazi yako na majirani kila nyumba inalipa $350-$1000 kwa mwaka kwa usafi wa jumla kama kukata majani na kusafisha mitaro. Hii ni nje ya nyumba yako hii nayo ni lazima na kisheria wanaweza kwenda na utaratibu mpaka wakapiga mnada nyumba
  • Tuna tozo za maji na kuchukuwa taka. Kila wiki wanapita kuchukuwa taka kwenye magaloni maalumu. Hii inafanywa na manispaa huwezi kuchoma matakataka ovyo ovyo. Maji unalipa kutokana ma matumizi lakini taka utalipia unataka au hautaki jumla sio chini ya $100 kila mwezi. Ukitupa uchafu ovyo ni faini, usipoweka uchafu vizuri kwenye mifuko ni faini....
  • Barabara nyingi zinajegwa kwa mikopo inayoitwa goverment bonds hivyo ni lazima ilipwe. Kila nikienda kazini kwa mfano ni lazima nipitie kwenye barabara za kulipia "toll roads" na natumia sio chini ya $5-$7 kwenda kwa siku moja na kurudi. Tena hii ni rahisi New York wanatumia $12-$15.
  • Ukienda kwenye hotel na kokodi chumba karibu 35% ni kodi na tozo, kwenye simu, cable za TV au Dish hivyohivyo
  • Kwenye super market kila ukinunua kitu kuna 5% ya tozo inaenda kusaidia “Metro" ambayo ni kama mwendo kasi yetu.
  • Lakini hapa kuna bima ya karibu kila kitu nyumba ni lazima uwe na bima na kwenye hizi bima kuna pesa zinaenda kusaidia idara kama Zimamotto... na ambulance
Hapa sijaongelea tozo na kodi za mishahara. Lakini mjue hapa bado tuna nafuu sana kulinganisha na nchi za Ulaya au Canada ambako Tozo na kodi zipo juu sana. Familia yangu ina bahati tuna nyumba Uninio sehemu ambayo ina thamani sana lakini kodi zetu pale hazifiki hata 1% ya thamani wakati bodaboda wanalipa kodi kwenye mafuta. Hivyo kuna sehemu kiukweli wanaonufaika ni matajiri tu kusema ukweli.

Kuna ambao watasema huko Ulaya na US pesa inaonekana ni kweli tuna shule kwenye kila mtaa za watoto zina mabasi na ni bure lakini tunalipa 3% kwenye thamani ya nyumba na pesa inaenda huko. Hivyo hoja ni yaanze mayai au kuku lakini kodi ni muhimu na maendeleo ni muhimu. Ndiyo maana hoja yangu ni kwamba tozo ni muhimu kwasababu ni mtaji na utaratibu mpya wa kuongeza wigo la walipa kodi na kuweka mifumo ya kimaendeleo. Tatizo kubwa ni mazoea ya watu wengi walikuwa wamezoea kukaa bila shughuli na kubangaiza lakini kama tunataka umeme vijijini, barabara za lami na hospitali ni lazima zitengenezwe, kuwe na pesa za matengenezo kila mara na pesa za wahudumu. Ni lazima kuwe na mfumo wa mapato na wananchi ni lazima wazalishe ili waweze kuwa na mifumo hii. Huwezi kukaa kijijini hulipi kodi yeyote, huzalishi chochote halafu unahitaji barabara, maji, umeme ... pesa inatoka wapi? Ni lazima serikali iwekeze kwenye kilimo ili wewe mwanakijiji uweze kuchangia kodi na maendeleo na ndicho kinacho fanyika kwa sasa
Umesahau eneo la matumizi. Kwamba wakati umma unajifunga mkanda wengine wanaendelea kuingiza V8 brand new kwa hela za serikali!!
 
Hoja ni double taxation kitu ambacho ni kinyume na sheria ya kodi
 
Kuna hoja kwamba mwendazake angekuwepo miradi ingefanyika na unafuu kwa mwananchi wa kawaida ungezingatiwa. Hili halina uthibitisho ila linafikirisha - katika mazingira ya kwamba vita ya Russia/Ukraine haipo!
 
Kisingekuwa na unafuu wowote.

Mosi. Hakupandisha mishahara hivyo kwa kipindi Cha miaka 5, purchasing power ya Wafanyakazi nchini ilikuwa inashuka, kumbuka inflation ilikuwa inaongezeka mwaka hadi mwaka.

Pili. Kupigwa marufuku kuuza mazao nje ya nchi na bei za pembejeo kupanda,
Hii iliwaathiri wakulima wadogo wadongo ambao ndio wengi na bei ya mazao kudorora.

Tatu. Taasisi za fedha kudorora
Benki zilikuwa kwenye Hali mbaya mpaka kupelekea baadhi kufilisika.

Kifupi tulikuwa tunaenda kwenye mdororo wa uchumi.

Nne. Kutoajiri
Nadhani kila mtu alifahamu janga lililoachwa na yule mwenda kuhusu Hali ya ajira nchini.

Tano. Biashara kudorora na makampuni kukimbilia nje ya nchi

Sita.Miradi ilikuwa haipiti bungeni kujadiliwa hivyo ilikuwa one man show.

Angeendelea Hali ingekuwa mbaya zaidi kuliko hata Sasa.
 
Kwanza tuweke mambo sawa tozo ni aina ya kodi. Hivyo tusiongelee tozo kama vile sio kodi.

Mimi binafsi sijaona ubaya wowote wa serikali kuweka tozo na nina fikiri hakuna njia nyingine kwa wakati huu zaidi ya tozo na nitajaribu kuweka hoja hapa vizuri. Tanzania kama nchi inayoendelea inahitaji pesa ili iweze kuwekeza kwenye miradi mingi sana kuanzia elimu, maji, barabara, umeme, kilimo, ulinzi.......n.k

Sasa vyanzo vya mapato ni hivi
  1. Missada kutoka nje
  2. kodi na tozo
  3. mikopo
Tanzania tumeshakopa na bado tutaendelea kukopa kama tutapata mikopo nafuu lakini vilevile tunakusanya kodi mbalimbali. Lakini ukiangalia vizuri budget zetu pesa ya kodi ambayo haitoshi hata kwenye budget bado inaenda kwenye shughuli ambazo sizo za kimaendeleo hivyo sio uwekezaji wa nchi bali ni matumizi. Kuna miradi tunalipia kwenye kodi kama ya maji na umeme lakini wakati wa Kikwete pesa karibu yote ilikuwa ni kulipa mishahara na matumizi ya serikali.

Sasa kama nchi tuko kwenye kipindi cha uwekezaji kwa mara ya kwanza tunaanza kuona barabara za kisasa, shule bora, hospitali na umeme hasa vijijini. Sasa tumefikaje hapa ? Ni kuwekeza kwa kodi mpya na tozo. Umeme mfano wa vijijini umepelekwa na tozo maalamu kwenye luku za nyumbani na barabara za vijijini nyingi zinatengenezwa na tozo kwenye mafuta. Lakini ili kama nchi tuweze kuwekeza na kuongeza walipa kodi ni lazima tuwekeze kwenye kilimo. Kilimo kitaongeza mapato kwenye kodi lakini tatizo hatuna mfumo mzuri wa kilimo kuwa na uazalishaji wa uhakika. Bashe amekuja na mpango mzuri wa kuongeza uzalishaji kwa kufanya yafuatayo (1) Serikali itatoa ruzuku kwenye mbolea (2) Serikali itawekeza kwenye umwagiliaji (3) watatoa mbegu (4) watafuta wawekezaji wa viwanda (5) kutafuta masoko. Hii ndiyo mojawapo kubwa ya kuongeza ajira na kodi lakini mtaji wa yote haya ni karibu Trillion moja sasa mtaji unatoka wapi? Hii ndiyo sababu imeenda kwenye tozo hivyo tozo ni muhimu kwasababu ni mtaji wa uhakika wa kuongeza kodi kwa miaka ijayo. Lakini ni tukiangalia vizuri tatizo letu ni utamaduni mbovu watu wengi walizoea kukaa bila kulipa kodi wala tozo

Mimi ni diaspora wa muda mrefu sana na naishi na kutafuta maslahi yangu jimbo la Texas. Hili jimbo letu linajulikana kwa kuwa na kodi ndogo lakini ngoja niwape data kidogo ili mgundue tonavyolipa kodi.

  • Nyumba kila mwaka nalipa 3% ya thamani ya nyumba. Hivyo kwa mfano kama nyumba pale Tanzania yenye thamani ya Tsh 100,000,000 basi unatakiwa kulipa kila mwaka Tsh 3,000,000. Hakuna mjadala kwenye hili na usikolipa unapekwa mahakamani na nyumba inapigwa mnada
  • Jumuia na majiradi vilevile wana kitu kinaitwa HOA-Housing Owners Association hii ni jumuia ya makazi yako na majirani kila nyumba inalipa $350-$1000 kwa mwaka kwa usafi wa jumla kama kukata majani na kusafisha mitaro. Hii ni nje ya nyumba yako hii nayo ni lazima na kisheria wanaweza kwenda na utaratibu mpaka wakapiga mnada nyumba
  • Tuna tozo za maji na kuchukuwa taka. Kila wiki wanapita kuchukuwa taka kwenye magaloni maalumu. Hii inafanywa na manispaa huwezi kuchoma matakataka ovyo ovyo. Maji unalipa kutokana ma matumizi lakini taka utalipia unataka au hautaki jumla sio chini ya $100 kila mwezi. Ukitupa uchafu ovyo ni faini, usipoweka uchafu vizuri kwenye mifuko ni faini....
  • Barabara nyingi zinajegwa kwa mikopo inayoitwa goverment bonds hivyo ni lazima ilipwe. Kila nikienda kazini kwa mfano ni lazima nipitie kwenye barabara za kulipia "toll roads" na natumia sio chini ya $5-$7 kwenda kwa siku moja na kurudi. Tena hii ni rahisi New York wanatumia $12-$15.
  • Ukienda kwenye hotel na kokodi chumba karibu 35% ni kodi na tozo, kwenye simu, cable za TV au Dish hivyohivyo
  • Kwenye super market kila ukinunua kitu kuna 5% ya tozo inaenda kusaidia “Metro" ambayo ni kama mwendo kasi yetu.
  • Lakini hapa kuna bima ya karibu kila kitu nyumba ni lazima uwe na bima na kwenye hizi bima kuna pesa zinaenda kusaidia idara kama Zimamotto... na ambulance
Hapa sijaongelea tozo na kodi za mishahara. Lakini mjue hapa bado tuna nafuu sana kulinganisha na nchi za Ulaya au Canada ambako Tozo na kodi zipo juu sana. Familia yangu ina bahati tuna nyumba Uninio sehemu ambayo ina thamani sana lakini kodi zetu pale hazifiki hata 1% ya thamani wakati bodaboda wanalipa kodi kwenye mafuta. Hivyo kuna sehemu kiukweli wanaonufaika ni matajiri tu kusema ukweli.

Kuna ambao watasema huko Ulaya na US pesa inaonekana ni kweli tuna shule kwenye kila mtaa za watoto zina mabasi na ni bure lakini tunalipa 3% kwenye thamani ya nyumba na pesa inaenda huko. Hivyo hoja ni yaanze mayai au kuku lakini kodi ni muhimu na maendeleo ni muhimu. Ndiyo maana hoja yangu ni kwamba tozo ni muhimu kwasababu ni mtaji na utaratibu mpya wa kuongeza wigo la walipa kodi na kuweka mifumo ya kimaendeleo. Tatizo kubwa ni mazoea ya watu wengi walikuwa wamezoea kukaa bila shughuli na kubangaiza lakini kama tunataka umeme vijijini, barabara za lami na hospitali ni lazima zitengenezwe, kuwe na pesa za matengenezo kila mara na pesa za wahudumu. Ni lazima kuwe na mfumo wa mapato na wananchi ni lazima wazalishe ili waweze kuwa na mifumo hii. Huwezi kukaa kijijini hulipi kodi yeyote, huzalishi chochote halafu unahitaji barabara, maji, umeme ... pesa inatoka wapi? Ni lazima serikali iwekeze kwenye kilimo ili wewe mwanakijiji uweze kuchangia kodi na maendeleo na ndicho kinacho fanyika kwa sasa
Mkuu, naona umeongea mambo mengi lakini umeshindwa kufafanua uzuri kuhusu hizi kodi na tozo.

Ni kweli kuna kodi na ushuru na hizi zipo kisheria na zatambulika, kisha kuna tozo ambazo uingizaji wake katika mfumo wa kodi hakueleweki na kwahitaji ufafanuzi.

1. Kuna kodi ya maendeleo yaani PAYE, kodi ya ongezeko la thamani yaani VAT, kodi ya kiwanja yaani ambayo ni kwa maendeleo ya eneo unoishi, kodi ya uingizaji magari nchini, kodi ya uuzaji mali kama nyumba yaani "stamp duty", kodi za uingizaji bidhaa ndogondogo nchini, kodi kwenye usafirishaji bidhaa nje ya nchi na kodi zingine, ila hizi ni kodi na zimewekwa kisheria na zatambulika.

2. Kuna ushuru ambao pia watambulika kama ushuru kwenye mizani, ushuru wa gharama ya ujenzi wa reli, ushuru kwenye kupata leseni ya udereva na ushuru kwenye shughuli za mitandao (sifahamu kama zimeondolewa) na ushuru wa kusafirisha bidhaa zitokanazo na miti, ushuru wa vivuko ushuru mwingine.

3. Kuna tozo ambazo ndizo tatizo na serikali imezi-introduce kwa wananchi kinyemela, tozo ya miamala katika simu za mkononi, miamala kwenye mabenki, tozo katika majengo ambayo mpangaji ahusika. Tozo hizi ni zile ambazo zakatwa mara mbili yaani double Taxation baada ya mtu kukatwa mapato ya PAYE na VAT pamoja na kukatwa katika simu ya mkononi na kukatwa na mabenki ambayo nayo hukata fedha ambazo huziita "account maintenance".

Sasa mimi pia nimeishi huko Marekani na pia nimepata bahati ya kuishi katika nchi zingine lakini ni pale Uingereza ambako nilikaa kwa muda na niliona aina za kodi wanozitoza kwa wananchi wake na mimi kuwa ni mmoja wa watozwa kodi kwa miaka kama mitatu hivi.

Uingereza pale wana kodi ya PAYE, wana kodi ya maendeleo ambayo huiita "council Tax" ambayo kiufundi ni kodi ya majengo au kodi ya kichwa kwani hata mtoto akifika umri wa miaka 18 kama akianza kazi rasmi basi hutakiwa kulipa kodi hiyo.

Hii ndo sababu kubwa pale nchini Uingereza mtoto akifika umri wa miaka 18 huweza hata kufukuzwa ndani ya nyumba ili aende akajitegemee na ajitafutie maisha isipokuwa kama yupo bado asoma.

Hizi kodi mbili yaani kodi ya PAYE huenda serikalini moja kwa moja, lakini ile ya majengo hutozwa na manispaa husika ambayo hutathmini kodi hiyo kila mwaka.

Kodi hii ya manispaa ndiyo huenda kutoa huduma katika manispaa hiyo kama uzoaji taka, ujenzi au uboreshaji wa miundombinu, malipo ya huduma za wazima moto na polisi na shughuli zingine kama ujenzi wa nyumba za kijamii au "social housing", mashule, huduma kwa wazee na wasojiweza pamoja na usimamizi wa maeneo ya kujipumzisha au "recreation parks".

Sasa baada ya mazagazaga hayo ya hizi kodi ndio kuna tozo za kawaida ambazo ni hitaji la lazima kwa kila mwananchi kama tozo ya huduma ya Runinga au TV Lisence, kwamba ni lazima ulipie leseni ya Runinga kuangalia, na hiyo itakuwezesha kuangalia channels zote za bure nchini humo isipokuwa zile channels kali kama za mpira ambazo ni lazima ulipie gaharama za ziada kupitia ankara au bills za kila mwezi. Kwa mfano weye walipia Runinga kiasi kama pauni 245 kwa mwaka, basi hiyo ni mbali na gharama za kuangalia huduma kama za Sky ambazo hutoza kama pauni 60 hivi kwa mwezi na pia zipi huduma zingine kama virgin media na kadhalika.

Kisha kuna tozo ya huduma za simu ya mkononi yaani na ile simu ya ndani telephone bills pamoja na internet ambayo huja kwa vifurushi tofauti. Kuna tozo ya huduma ya maji, umeme, gesi na hizi ni huduma za lazima kwa kila nyumba nchini humo.

Hivyo wakati huu nchini humo wananchi wanalalamika gharama za maisha kupanda, mfumuko wa bei kuwa juu na gharama za mafuta na gesi kutabiriwa kuwa juu zaidi ifikapo mwezi Disemba na January. Lakini viongozi wa nchi hiyo mida hii wana wkati mgumu kuhakikisha kila mwananchi hawapati shida na wanatumia muda mwingi kueleza namna watavyolitatua tatizo hilo ambalo pamoja na kuathiri dunia nzima lakini kila mtu ataubeba msalaba wake.
Sasa nimekuelezea tofauti ya Kodi, Ushuru na tozo na kinachowaudhi watanzania wengi ni tozo ziloibuka bila maelezo na sababu za msingi na pia kuonekana wazi kwenye macho ya watanzania kwamba kitendo hicho ni "double taxation" ambayo yawamiza zaidi watanzania wa kawaida kabisa.

Kwenye hili hakuhitaji ushabiki wala ufuasi wa chama bali umakini na mjadala pevu kwa maslahi ya watanzania wote.

Mjadala huu wa kuhusu Tozo ni "genuine" yaani ni wa kweli na serikali wana budi kuketi na kutafakari namna ya kurekebisha tozo hizi kuendana na hali halisi ya nchi yetu kiuchumi kwa kubuni tozo rafiki zenye unafuu badala ya kutumia mabavu, maneno ya vitisho na kebehi kwamba wanouliza wahamie Burundi.
 
Kwanza tuweke mambo sawa tozo ni aina ya kodi. Hivyo tusiongelee tozo kama vile sio kodi.

Mimi binafsi sijaona ubaya wowote wa serikali kuweka tozo na nina fikiri hakuna njia nyingine kwa wakati huu zaidi ya tozo na nitajaribu kuweka hoja hapa vizuri. Tanzania kama nchi inayoendelea inahitaji pesa ili iweze kuwekeza kwenye miradi mingi sana kuanzia elimu, maji, barabara, umeme, kilimo, ulinzi.......n.k

Sasa vyanzo vya mapato ni hivi
  1. Missada kutoka nje
  2. kodi na tozo
  3. mikopo
Tanzania tumeshakopa na bado tutaendelea kukopa kama tutapata mikopo nafuu lakini vilevile tunakusanya kodi mbalimbali. Lakini ukiangalia vizuri budget zetu pesa ya kodi ambayo haitoshi hata kwenye budget bado inaenda kwenye shughuli ambazo sizo za kimaendeleo hivyo sio uwekezaji wa nchi bali ni matumizi. Kuna miradi tunalipia kwenye kodi kama ya maji na umeme lakini wakati wa Kikwete pesa karibu yote ilikuwa ni kulipa mishahara na matumizi ya serikali.

Sasa kama nchi tuko kwenye kipindi cha uwekezaji kwa mara ya kwanza tunaanza kuona barabara za kisasa, shule bora, hospitali na umeme hasa vijijini. Sasa tumefikaje hapa ? Ni kuwekeza kwa kodi mpya na tozo. Umeme mfano wa vijijini umepelekwa na tozo maalamu kwenye luku za nyumbani na barabara za vijijini nyingi zinatengenezwa na tozo kwenye mafuta. Lakini ili kama nchi tuweze kuwekeza na kuongeza walipa kodi ni lazima tuwekeze kwenye kilimo. Kilimo kitaongeza mapato kwenye kodi lakini tatizo hatuna mfumo mzuri wa kilimo kuwa na uazalishaji wa uhakika. Bashe amekuja na mpango mzuri wa kuongeza uzalishaji kwa kufanya yafuatayo (1) Serikali itatoa ruzuku kwenye mbolea (2) Serikali itawekeza kwenye umwagiliaji (3) watatoa mbegu (4) watafuta wawekezaji wa viwanda (5) kutafuta masoko. Hii ndiyo mojawapo kubwa ya kuongeza ajira na kodi lakini mtaji wa yote haya ni karibu Trillion moja sasa mtaji unatoka wapi? Hii ndiyo sababu imeenda kwenye tozo hivyo tozo ni muhimu kwasababu ni mtaji wa uhakika wa kuongeza kodi kwa miaka ijayo. Lakini ni tukiangalia vizuri tatizo letu ni utamaduni mbovu watu wengi walizoea kukaa bila kulipa kodi wala tozo

Mimi ni diaspora wa muda mrefu sana na naishi na kutafuta maslahi yangu jimbo la Texas. Hili jimbo letu linajulikana kwa kuwa na kodi ndogo lakini ngoja niwape data kidogo ili mgundue tonavyolipa kodi.

  • Nyumba kila mwaka nalipa 3% ya thamani ya nyumba. Hivyo kwa mfano kama nyumba pale Tanzania yenye thamani ya Tsh 100,000,000 basi unatakiwa kulipa kila mwaka Tsh 3,000,000. Hakuna mjadala kwenye hili na usikolipa unapekwa mahakamani na nyumba inapigwa mnada
  • Jumuia na majiradi vilevile wana kitu kinaitwa HOA-Housing Owners Association hii ni jumuia ya makazi yako na majirani kila nyumba inalipa $350-$1000 kwa mwaka kwa usafi wa jumla kama kukata majani na kusafisha mitaro. Hii ni nje ya nyumba yako hii nayo ni lazima na kisheria wanaweza kwenda na utaratibu mpaka wakapiga mnada nyumba
  • Tuna tozo za maji na kuchukuwa taka. Kila wiki wanapita kuchukuwa taka kwenye magaloni maalumu. Hii inafanywa na manispaa huwezi kuchoma matakataka ovyo ovyo. Maji unalipa kutokana ma matumizi lakini taka utalipia unataka au hautaki jumla sio chini ya $100 kila mwezi. Ukitupa uchafu ovyo ni faini, usipoweka uchafu vizuri kwenye mifuko ni faini....
  • Barabara nyingi zinajegwa kwa mikopo inayoitwa goverment bonds hivyo ni lazima ilipwe. Kila nikienda kazini kwa mfano ni lazima nipitie kwenye barabara za kulipia "toll roads" na natumia sio chini ya $5-$7 kwenda kwa siku moja na kurudi. Tena hii ni rahisi New York wanatumia $12-$15.
  • Ukienda kwenye hotel na kokodi chumba karibu 35% ni kodi na tozo, kwenye simu, cable za TV au Dish hivyohivyo
  • Kwenye super market kila ukinunua kitu kuna 5% ya tozo inaenda kusaidia “Metro" ambayo ni kama mwendo kasi yetu.
  • Lakini hapa kuna bima ya karibu kila kitu nyumba ni lazima uwe na bima na kwenye hizi bima kuna pesa zinaenda kusaidia idara kama Zimamotto... na ambulance
Hapa sijaongelea tozo na kodi za mishahara. Lakini mjue hapa bado tuna nafuu sana kulinganisha na nchi za Ulaya au Canada ambako Tozo na kodi zipo juu sana. Familia yangu ina bahati tuna nyumba Uninio sehemu ambayo ina thamani sana lakini kodi zetu pale hazifiki hata 1% ya thamani wakati bodaboda wanalipa kodi kwenye mafuta. Hivyo kuna sehemu kiukweli wanaonufaika ni matajiri tu kusema ukweli.

Kuna ambao watasema huko Ulaya na US pesa inaonekana ni kweli tuna shule kwenye kila mtaa za watoto zina mabasi na ni bure lakini tunalipa 3% kwenye thamani ya nyumba na pesa inaenda huko. Hivyo hoja ni yaanze mayai au kuku lakini kodi ni muhimu na maendeleo ni muhimu. Ndiyo maana hoja yangu ni kwamba tozo ni muhimu kwasababu ni mtaji na utaratibu mpya wa kuongeza wigo la walipa kodi na kuweka mifumo ya kimaendeleo. Tatizo kubwa ni mazoea ya watu wengi walikuwa wamezoea kukaa bila shughuli na kubangaiza lakini kama tunataka umeme vijijini, barabara za lami na hospitali ni lazima zitengenezwe, kuwe na pesa za matengenezo kila mara na pesa za wahudumu. Ni lazima kuwe na mfumo wa mapato na wananchi ni lazima wazalishe ili waweze kuwa na mifumo hii. Huwezi kukaa kijijini hulipi kodi yeyote, huzalishi chochote halafu unahitaji barabara, maji, umeme ... pesa inatoka wapi? Ni lazima serikali iwekeze kwenye kilimo ili wewe mwanakijiji uweze kuchangia kodi na maendeleo na ndicho kinacho fanyika kwa sasa
Kwanza kabisa, huwezi kufahamu kwa asilimia mia kwamba tozo ndizo zina changia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi. Matumizi ya serikali na jinsi ambavyo rasilimali hutumika siku zote ni siri. Jambo la kushangaza ni jinsi ambavyo kodi hubadilika kila mwaka. Sijawahi kusikia punguzo wala kufutwa kabisa kwa baadhi ya kodi. Siku zote serikali hutanua wigo na kuongeza kodi.
 
1 Ulikuwa unapendekeza serikali ifanye nini kuongeza wigo la walipa kodi kama hukubaliani na uwekezaji kwenye kilimo kutokana na tozo. Unataka tokope?, kuongeze kodi nyinginge na zipi?, au tusiwekeze kabila tubaki tulivyo. Hatuwezi kutegemea misaada kila siku
 
Sikubaliani na wewe unaposema kwamba madhumuni ya kodi ni kuwekeza zaidi kwenye kilimo. Hii ni taarifa ambayo lazima uwe ndani sana serikalini kufahamu ukweli. Mimi nina amini sana kwenye bajeti iliyo wasilishwa bungeni kwasababu hayo ndiyo mapato na matumizi tunayo yafahamu kama wananchi. Katika swali lako, ningependa sana turejee zaidi kwenye bajeti ya kilimo na tufuate makadirio yaliyo
wekwa kwa ajili ya mwaka huu. Kwanini serikali itafute fedha za ziada katikati ya mwaka wa fedha?
 
Back
Top Bottom