Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Picha ya kwanza juu ni kiongozi wa Jamhuri ya Watu wa Donetsk bwana Denis Pushilin, Na picha ya chini ni kiongozi wa Jamhuri ya Watu wa Luhansk bwana Leonid Pasechnik, Jamhuri hizo ni majimbo yaliyojitenga toka Ukraine.
Naomba nianze utangulize wa makala yangu kwakusema, Dunia ili iwe salama inatakiwa kuwa na wakubwa wawili au zaidi (balance of power), sio mmoja tu anaamua yeye kwaajili ya dunia na hapingwi, Mbele ya Urusi sasa hatutaona vita vya holela vya Marekani na washirika wake.
Sababu ya kwanza ya kuunga mkono Urusi ni kwamba ni hatua muhimu ya kukomesha mauaji ya miaka karibu kumi sasa yanayofanywa na Ukraine dhidi ya Wananchi wa Majimbo ya Luhansk na Donetsk. Kwa msiojua Mtangulizi wa Rais Zelensk wa Ukraine, bwana Petro Poroshenko tangu ashike madaraka 2014 aliendesha mauaji ya wapinzani wengi katika majimbo ya DPR na LPR yaliyotaka kujitenga hadi alipoondoka tu vita havikumalizika.
Alipoingia Zelensk nae akafuata nyayo za mtangulizi wakw, akaigeuza Ukraine kuwa jehanamu kwa aliowaita waasi, aliendesha mauaji makubwa sana hasahasa 2021 dhidi ya raia kule katika miji ya Donbass katika kile alichokiita kudhibiti waasi wanaotaka kujitenga. Dunia hii ilikaa kimya, Urusi ikawa ndio pango la kupokea wakimbizi zaidi la laki tatu,
Kiongozi Jimbo la Donetsk Bwana Denis Pushilin amenusurika mauaji zaidi ya marakumi hadi alipoomba ulinzi wa kimataifa kutoka Moscow, na mwisho akaongoza mapambano na kufanikiwa kujitangazia Uhuru.
Vile vile kiongozi wa jimbo la Luhansk bwana Leonid Pasechnik nae ilimlazimu kutafuta hifadhi ya kisiasa Moscow kwa lengo la kunusuru maisha yake dhidi ya Rais wa Ukraine bwana Zelensk aliyeapa kufuta uasi katika majimbo hayo, Aliongoza mapambano kwa ushirika wa Kiongozi wa jimbo la Donetsk bwana Pushilin na hatimaye wiki jana wamefanikiwa kumshinda Zelensk na Kujitangazia Uhuru.Urusi imeyatambua majimbo hayo kama nchi huru, Belarus na nchi nyingine tano yayari zimetambua. Ukraine imepinga uhuru huo ikaapa kuendesha vita nzito zaidi dhidi ya waliojitenga, Hatua hiyo ikawalazimu viongozi wa mapinduzi waombe msaada wa kijeshi kutoka Urusi. Na wameupata. Oparesheni ya Urusi ndio mwarobaini wa kukomesha mauaji ya miaka zaidi ya kumi sasa, kinyume na hapo miji itaendelea kuvuja damu kila kukicha.
Sababu ya pili ya kuunga mkono Urusi ni kitendo cha Marekani kutaka kujenga ngome ya kijeshi Ukraine, na katika kutimiza hilo Marekani kwakutumia washirika wake wa Nato wakamshawishi avunje Mkataba wa Minsk wa 2015 pamoja na mambo mengine, ulisema Ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Urusi (Ukraine) uliokuwa Umoja wa Kisoviet ya zamani Hautaruhusiwa kujiunga na Umoj wa Ulaya. Katika kibri cha Zelensk akaomba kujiunga NATO. Moscow akajibu kwa moto.
Sababu ya tatu ya kuunga mkono Urusi ni kitendo cha Marekani kupitia shirika lake la kijasusi la CIA kuvuruga dili la Urusi la kujenga bomba la awamu ya pili la gesi maarufu kama NORD STREAM II, ambalo lingelisha gesi Ulaya yote kwa 90% tofauti na sasa mbapo Ulaya inategemea gesi ya Urusi kwa 40% tu, Marekani ameitumia Ukraine kukwamisha mradi huu na baadhi ya nchi za Nato. Kitendo hiki ilikuwa ni uchokozi wa kiuchumi na kijasusi, Jibu la Urusi limeanzia kwa Ukraine kwanza.
Mtazamo wangu kama Yericko Nyerere, vita hivi ni kati ya Urusi na Marekani, na vitaisha kwa nchi hizi mbili kukaa chini na kukubaliana terms and conditions kama mihimili miwili mikuu duniani. Na sio vinginvyo, Ukraine kwa sasa ni uwanja wa biashara ya Silaha ya ulaya na Marekani.
Baada ya vita hii Urusi ataheshimiwa na kuogopwa sana, na vikwazo hivi amini ni geresha tu, havitachukua miezi 18 vitaondolewa, Rejea vikwazo vya 1990 alivyowekewa Urusi alipoivami Afghanustan vilimwathiri nani na viliishia wapi zaidi ya Afghanistan kusambaratishwa? Haya vikwazo vya Urusi vya 2008 alipoivamia Georgia viliishia wapi na vilimwathiri nani zaidi ya Georgia kuwa eneo muhimu la Urusi hadi leo? Vikwazo vya Urusi vya juzi tu baada ya kuivamia Cremia vimefiki wapi?.
Kikwazo ambacho kilikuwa tishio kwa uchumi wa Urusi alichowekewa na EU ni hiki cha kuzuia huduma ya kibenki ya SWIFT, Lakini ndani ya saa 24 tu, Rais wa Urusi Vlamir Putin ametangaza hatua za dharula kukabili vikwazo vya kiuchumi, na haraka Urusi na China wamekubaliana kutumia huduma ya kibenki ya China ya Cross-Border Interbank Payment System, or CIPS. Kwa tafrisi hiyo nikuwa kikwazo cha uchumi hakitaiathiri Urusi moj kwa moja.
Ukweli ni kuwa Nchi nyingi duniani haziwezi kuendesha chumi zao, katika nyanja nyingi kama za kijeshi na mengineyo bila Urusi. Dunia inaihitaji Urusi kuliko Urusi inavyo ihitaji dunia yenyewe. Japo wanategemeana. Mataifa ya Umoja wa Ulaya (EU) yapo 27, ukijumlisha na Marekani jumla ni nchi 28 tu, haya mataifa sio yote yanaipinga Urusi, Dunia ina nchi 195 + Donetsk na Luhansk, ni 197, Sasa jiulize nchi 164+ ziko upande upi?. Bado mtu anasema Urusi imetengwa na dunia? Basi huyo mtu haijui dunia sawasawa.
Ni wazi kwamba, Dunia leo iko mapande matatu, kuna Urusi, Kuna Uchina na kuna Marekani... Kwenye nchi 28 Uchina hayuko huko, zingatia kuna nchi za kati zenye uchuki mkubwa ambazo ni India hayuko na Ukraine, huko Brazil hayuko huko na Ukraine... Na hawa wanamuunga mkono Mrusi.... Dunia sasa inastawi na hii ndio balance ya dunia na inapumua vizuri sasa.
Na Yericko Nyerere