Kwanini naunga mkono Urusi kuchukua hatua za kijeshi Ukraine?

Pamoja na Sababu zako zotee naona hamna
Bado yakupasa utambue

Ukraine ni nchi huru wana uhuru wa kuamua mambo yao as a state
Kwani iran sio nchi huru. Mbona wao wakitaka kutengeneza vinu vya nyuklia Marekani na jamaa zake wanaanza zengwe? Hii balance of power inahitajika sana kwa sasa.

Kuhusu vikwazo, nchi kama india ambayo inasemwa inahitaji 85% ya malighafi toka russia kwa ajili ya kuendeshea viwanda vyake vya xhuma watafanyaje sasa? Wafunge viwanda?
 
Marekani na washirika wake kuua watu ndio inatoa uhalali wa Russia au taifa lingine nalo kuua watu nyie mazombi?
Kwaiyo marekani na washirika wake +mayahudi kuuwa waco na hatia ni sawa??
 
Pamoja na Sababu zako zotee naona hamna
Bado yakupasa utambue

Ukraine ni nchi huru wana uhuru wa kuamua mambo yao as a state
Unajua nchi guru ipoje kwani Russia lini kamwingilia ukran kibabe. Hugo USA na Ukraine wanajua kosa lao sana hata nchi zingine sema wamejikausha tu
 
Kwanza inategemea hizo habari za Warusi kutomwuunga mkono Putin unazipata kutoka mtoa habari yupi. Hili ndiyo tatizo la Mtanzania. Uchambuzi wake wa masuala mengi tu ni mdogo.
Pili, Marekani makini wameshaiambia serikali yao Marekani yenyewe kuwa mbona Marekani haikubali Urusi iweke vifaa vyake vya vita Cuba (Cuba Missile Crisis: The JFK stand off with the USSR) ambayo iko mbali na Marekani kwa kilomita 90; iweje Urusi itegemewe kukaa kimyaa Ukraine ikikaribisha majeshi ya NATO, ambamo Marekani imo, yawe mpakani mwa Urusi? Mantiki gani Watanzania wanatumia isipokuwa kuleta ushabiki kwenye masuala mazito!?
 
Hii ndio typcal reflection ya viongozi wa chadema..huyu ni kiongozi mwandamizi wa chadema..watu wa visasi tuu..wakipewa nchi huyu atakuwa mshauri wa usalama kama anavyojinadi kujua sana mambo ya ujasusi wa kidola..sasa kwa msimamo wake huu wa kussuport mauji ya raia..watakapopewa uongozi wa nji hii..itakuwaje..watatumia miaka mingi kulipiza kisasi then maendeleo ya wananji ni baadae sana..pathetic.
 
Marekani na washirika wake kuua watu ndio inatoa uhalali wa Russia au taifa lingine nalo kuua watu nyie mazombi?

Kwaiyo kila kinachotamkwa na westerns unaamini? Hata kama ni Propaganda utaamini?? Eti puttin ameingiza asilimia 70% ya majeshi yake nchini ukrein 😁😁😁 wamejuwaje??? Hata mtoto mdogo huwezi kumwaminisha kijinga ivyo
 
Mada nyingine kama hz zinazoandikwa na watu wavivu wa kuona ktk macho ya kawaida na kufikiri,wanakopy sehemu alafu wanaleta hapa maneno ambayo sio ya kwao eti ss ndio tuanze kujadili mada kama hz tuwe tunapita na kuziacha bila kuchangia chochote ili mleta mada apate somo.
 
Kwa nini Urusi isivamiwe kwa sababu inaua raia wa jimbo la Chechnya wanaotaka kujitenga kwa muda mrefu sana?

Kwa nini China isivamiwe kwa kuendesha mauaji dhini ya majimbo yanayotaka kujitenga ya Tibet na Uyghurs?
 
Good point lakini kwa maono yangu nahisi hii itapelekea vita ya Nyuklia, tukumbuke tu kwamba Urusi ndio inaongoza duniani kwa Nyuklia na kwa sasa inabanwa na vikwazo ambavyo italazimishwa kutumia Nyuklia. Hii otakuwa vita ya 3 ya dunia. Tuombe Mungu tusifike huko.
 
Aisee nimependa uchambuzi wako safi sana
 
Baraza la Umoja wa Mataifa leo limepiga kura kwa azimio la kuilaani Urusi kwa uvamizi wake dhidi ya Ukraine. Nchi 141 zimeunga mkono azimio hilo na nchi 5 tu ambazo nyingi ni failed states ndizo zimelikataa hilo azimio
 
Tunazungumzia usalama siyo udikteta.
 
Toka mwano Naiunga Urusi chakaza hao wamarekani mie nipo na Putin
 
Kama NORD STREAM II ilikiwa isambaze asilimia 90 ya gesi Ulaya ila uvamazi wa umesababisha apoteze hata ile asimilia 40 sasa hizo ni akili au matope? Hapo kuna kipi cha kushangalia kwenye huo uvamizi kama amerudi kwenye 0% kabisa kusambaza gesi Ulaya?!
Halafu CIA kuvuruga dili lao kijasusi kwa amani na wao wanajibu kwa vita huoni huko ni kuwa kilaza kwa idara ya kijasusi ya FSB? Yani wamekubali wamezidiwa mbinu na CIA ni akili kubwa
 
Unacopy hapahapa na kusamba huku umefuta jina langu niliyeandika makala hii hapahapa?
 
Kwa Yerico anaye jitanabaisha kuwa ni mpenda haki na demokrasia, kusikia anaunga mkono mambo yasiyo ya kidemokrasia kama hivi, inatia shaka.
Bila shaka alikuwa anamuunga mkono jiwe, ila walipishana maslahi binafsi
Umesoma sababu na kuzielewa lakini kabla hujachangia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…