Kwanini naunga mkono Urusi kuchukua hatua za kijeshi Ukraine?

Hivi ikitokea mikoa wa Mwanza na Kagera zikatangaza uasi dhidi ya serikali ya jamhuri ya Tanzania vipi Rais atakaekuwepo ataacha hiyo Hali iendelee?vipi hatachukua hatua za kijeshi ili kulinda Taifa lake na kuleta umoja wa kitaifa? Je huoni kwamba asipochukua hatua za kijeshi ni kama atachochea mikoa mingine kujitenga?
Kwa maana hiyo je kosa la Zelenski liko wapi Mana alikua anazima uasi ili kulete umoja wa Taifa lake?
Pia tambua Ukurain ni Taifa huru hivo kujiunga NATO sio kosa

Mwisho acha kudanganya watu vikwazo vya kiuchumi lazima vitaua uchumi wa Urusi ni swala la muda tu.
Kwa hii thread Leo umepuyanga.
Umeshawahi kujiuliza ikitokea mikoa uliyoitaja ikatangazwa kuwa ni mali ya Uganda au mikoa ya Mbeya na Songwe ikatangazwa kuwa mali ya Zambia bila ridhaa yao?
Tafuta kwanza historia ya hayo majimbo ya Donbass ndo uje kucomment
 
Ni peace ipi mnayoitaka iwapo marekani alipovamia Libya na Iraq mlikaa kimya?

Nyie ndiyo wanafiki tunaoomba kila leo mpotee duniani,haifai kuliunga kundi la marekani hata kidogo kwani yeye ndiyo chanzo cha migogoro duniani hasa kwa tamaa ya mali na kuuza silaha.

Kwa majuha kama nyie na inferirity complex mliyonayo hamtaweza kujua umuhimu wa Russia na ubaya wa USA.

PUTIN keep it up!!

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
With all my respect kwako, wewe sio msemaji wangu na why umenisemea mimi kuwa nipo USA corner wakati hunijui na sijasema hivyo?why?kwa USA au nchi yeyote kuvamia another sovereign country ni makosa na end of day uvamizi unaleta maafa makubwa hasa kwa wanawake, wazee na watoto, next time show little bit kuwa ni middle class unayajitambua.
 
Swali langu moja tu.

Kwa ufafanuzi huu wenye mantiki kubwa hivi (plausible), inakuwaje Putin anakosa uungwaji mkono mkubwa na wananchi wake hadi kutegemea kuwa na bunge ambalo ni "rubber stamp", kudhibiti upinzani kwa mkono wa chuma, kutumia vikosi vya wasiojulikana kudhibiti ukosoaji (police state), kuimarisha tawala za kidikteta huko Belarus na Venezuela, n.k.

Wnanachi wa Urusi wamesikika wakilalamikia vikwazo vya NATO na Marekani kwamba si fair kwao kwani wao "hawakumchagua" Putin kuwa rais wao! Hiyo ni vita yake binafsi! Akwamishwe yeye na wapambe wake; sio raia wote wa Urusi.

Inafahamika kuwa huko Urusi, utawala wa Putin ni "one man show": hashauriwi, hakosolewi wala hapingwi na mhimili wowote. In maana kuwa ni yeye peke yake anayejua na kuyaona maslahi ya Urusi na ya Warusi? Wananchi wa Urusi hawana habari ndugu zao wakinyanyaswa na kuuawa huko Donbass, Crimea na Georgia? Warusi wote hawaoni janja ya Marekani na NATO kujiimarisha kijeshi kutishia usalama wa Urusi kupitia Ukraine na nchi zingine jirani (former USSR)?

Hoja yako inashawishi (plausible) lakini inatia shaka - doesn't sound rational. Ingekuwa hivyo, huyu mtu angetambuliwa na watu wake kama shujaa na sauti yao kumkubali ingesikika bila mikwaruzo. Au Marekani pia wamefanikiwa kudhibiti kikamilifu sauti halali ya Warusi? Au wamewageuza Warusi wengi kuwa vibaraka wao?
Mfano urusi ndio iwe tz. Chifu angaya ndiye awe putin. Unafikili chadema wangeunga mkono hiyo vita?? Hiyo ndio hali iliyopo urusi
 
Picha ya kwanza juu ni kiongozi wa Jamhuri ya Watu wa Donetsk bwana Denis Pushilin, Na picha ya chini ni kiongozi wa Jamhuri ya Watu wa Luhansk bwana Leonid Pasechnik, Jamhuri hizo ni majimbo yaliyojitenga toka Ukraine.

Naomba nianze utangulize wa makala yangu kwakusema, Dunia ili iwe salama inatakiwa kuwa na wakubwa wawili au zaidi (balance of power), sio mmoja tu anaamua yeye kwaajili ya dunia na hapingwi, Mbele ya Urusi sasa hatutaona vita vya holela vya Marekani na washirika wake.

Sababu ya kwanza ya kuunga mkono Urusi ni kwamba ni hatua muhimu ya kukomesha mauaji ya miaka karibu kumi sasa yanayofanywa na Ukraine dhidi ya Wananchi wa Majimbo ya Luhansk na Donetsk. Kwa msiojua Mtangulizi wa Rais Zelensk wa Ukraine, bwana Petro Poroshenko tangu ashike madaraka 2014 aliendesha mauaji ya wapinzani wengi katika majimbo ya DPR na LPR yaliyotaka kujitenga hadi alipoondoka tu vita havikumalizika.

Alipoingia Zelensk nae akafuata nyayo za mtangulizi wakw, akaigeuza Ukraine kuwa jehanamu kwa aliowaita waasi, aliendesha mauaji makubwa sana hasahasa 2021 dhidi ya raia kule katika miji ya Donbass katika kile alichokiita kudhibiti waasi wanaotaka kujitenga. Dunia hii ilikaa kimya, Urusi ikawa ndio pango la kupokea wakimbizi zaidi la laki tatu,

Kiongozi Jimbo la Donetsk Bwana Denis Pushilin amenusurika mauaji zaidi ya marakumi hadi alipoomba ulinzi wa kimataifa kutoka Moscow, na mwisho akaongoza mapambano na kufanikiwa kujitangazia Uhuru.

Vile vile kiongozi wa jimbo la Luhansk bwana Leonid Pasechnik nae ilimlazimu kutafuta hifadhi ya kisiasa Moscow kwa lengo la kunusuru maisha yake dhidi ya Rais wa Ukraine bwana Zelensk aliyeapa kufuta uasi katika majimbo hayo, Aliongoza mapambano kwa ushirika wa Kiongozi wa jimbo la Donetsk bwana Pushilin na hatimaye wiki jana wamefanikiwa kumshinda Zelensk na Kujitangazia Uhuru.Urusi imeyatambua majimbo hayo kama nchi huru, Belarus na nchi nyingine tano yayari zimetambua. Ukraine imepinga uhuru huo ikaapa kuendesha vita nzito zaidi dhidi ya waliojitenga, Hatua hiyo ikawalazimu viongozi wa mapinduzi waombe msaada wa kijeshi kutoka Urusi. Na wameupata. Oparesheni ya Urusi ndio mwarobaini wa kukomesha mauaji ya miaka zaidi ya kumi sasa, kinyume na hapo miji itaendelea kuvuja damu kila kukicha.

Sababu ya pili ya kuunga mkono Urusi ni kitendo cha Marekani kutaka kujenga ngome ya kijeshi Ukraine, na katika kutimiza hilo Marekani kwakutumia washirika wake wa Nato wakamshawishi avunje Mkataba wa Minsk wa 2015 pamoja na mambo mengine, ulisema Ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Urusi (Ukraine) uliokuwa Umoja wa Kisoviet ya zamani Hautaruhusiwa kujiunga na Umoj wa Ulaya. Katika kibri cha Zelensk akaomba kujiunga NATO. Moscow akajibu kwa moto.

Sababu ya tatu ya kuunga mkono Urusi ni kitendo cha Marekani kupitia shirika lake la kijasusi la CIA kuvuruga dili la Urusi la kujenga bomba la awamu ya pili la gesi maarufu kama NORD STREAM II, ambalo lingelisha gesi Ulaya yote kwa 90% tofauti na sasa mbapo Ulaya inategemea gesi ya Urusi kwa 40% tu, Marekani ameitumia Ukraine kukwamisha mradi huu na baadhi ya nchi za Nato. Kitendo hiki ilikuwa ni uchokozi wa kiuchumi na kijasusi, Jibu la Urusi limeanzia kwa Ukraine kwanza.

Mtazamo wangu vita hivi ni kati ya Urusi na Marekani, na vitaisha kwa nchi hizi mbili kukaa chini na kukubaliana terms and conditions kama mihimili miwili mikuu duniani. Na sio vinginvyo, Ukraine kwa sasa ni uwanja wa biashara ya Silaha ya ulaya na Marekani.

Baada ya vita hii Urusi ataheshimiwa na kuogopwa sana, na vikwazo hivi amini ni geresha tu, havitachukua miezi 18 vitaondolewa, Rejea vikwazo vya 1990 alivyowekewa Urusi alipoivami Afghanustan vilimwathiri nani na viliishia wapi zaidi ya Afghanistan kusambaratishwa? Haya vikwazo vya Urusi vya 2008 alipoivamia Georgia viliishia wapi na vilimwathiri nani zaidi ya Georgia kuwa eneo muhimu la Urusi hadi leo? Vikwazo vya Urusi vya juzi tu baada ya kuivamia Cremia vimefiki wapi?.

Kikwazo ambacho kilikuwa tishio kwa uchumi wa Urusi alichowekewa na EU ni hiki cha kuzuia huduma ya kibenki ya SWIFT, Lakini ndani ya saa 24 tu, Rais wa Urusi Vlamir Putin ametangaza hatua za dharula kukabili vikwazo vya kiuchumi, na haraka Urusi na China wamekubaliana kutumia huduma ya kibenki ya China ya Cross-Border Interbank Payment System, or CIPS. Kwa tafrisi hiyo nikuwa kikwazo cha uchumi hakitaiathiri Urusi moj kwa moja.

Ukweli ni kuwa Nchi nyingi duniani haziwezi kuendesha chumi zao, katika nyanja nyingi kama za kijeshi na mengineyo bila Urusi. Dunia inaihitaji Urusi kuliko Urusi inavyo ihitaji dunia yenyewe. Japo wanategemeana. Mataifa ya Umoja wa Ulaya (EU) yapo 27, ukijumlisha na Marekani jumla ni nchi 28 tu, haya mataifa sio yote yanaipinga Urusi, Dunia ina nchi 195 + Donetsk na Luhansk, ni 197, Sasa jiulize nchi 164+ ziko upande upi?. Bado mtu anasema Urusi imetengwa na dunia? Basi huyo mtu haijui dunia sawasawa.

Ni wazi kwamba, Dunia leo iko mapande matatu, kuna Urusi, Kuna Uchina na kuna Marekani... Kwenye nchi 28 Uchina hayuko huko, zingatia kuna nchi za kati zenye uchuki mkubwa ambazo ni India hayuko na Ukraine, huko Brazil hayuko huko na Ukraine... Na hawa wanamuunga mkono Mrusi.... Dunia sasa inastawi na hii ndio balance ya dunia na inapumua vizuri sasa.

Na Yericko Nyerere
View attachment 2136291View attachment 2136292
🤝🤝 Misukule ya malekani hawatakuelewa kwa sasa. Watakuja kuelewa baadae kuwa ili tueshimiane, inatakiwa tuwe na wababe zaidi ya mmoja
 
Hivi mmesoma vizuri UZI wa Yeriko au umeishai kusoma kichwa cha habari? Mbona jamaa kafafanua kwamba huyo rais wa Ukraine kaua sana na alikua anaendelea kuua sana na Urusi akawa anabeba mzigo wa wakimbizi??? Nashawishika kuamini kwamba hamjasoma UZI. Kwa maana ya upande unao unga mkono ni upi kati ya Ukrein na Urusi hilo sina tatizo nalo, kila mtu anaweza kubakia na mtazamo wake, nina shida na the way ulivyo weka maelezo yako maanake kama ni kutetea mauaji, ungeanza kumlaumu rais wa Ukrain kwanza
Unarudia upuuzi? Yeriko anatutafunia propaganda ya uwingo tu. Rais wa Ukraine alimwua nani???? Si kweli anachosema.
Pamoja hayo kweli hana habari. Soma jinsi Yeriko anavyodai nchi za Ulaya pekee ambazo ni chache zimpinga Putin. Ambayo si kweli.
Jioni hii Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa ulitoa tamko kusema vita ya Putin ni jinai, anatakiwa kuondoka mara moja na kulipa fidia! Mataifa 143 yaliunga mkono, 5 tu yalipinga!
 
Hivi ikitokea mikoa wa Mwanza na Kagera zikatangaza uasi dhidi ya serikali ya jamhuri ya Tanzania vipi Rais atakaekuwepo ataacha hiyo Hali iendelee?vipi hatachukua hatua za kijeshi ili kulinda Taifa lake na kuleta umoja wa kitaifa? Je huoni kwamba asipochukua hatua za kijeshi ni kama atachochea mikoa mingine kujitenga?
Kwa maana hiyo je kosa la Zelenski liko wapi Mana alikua anazima uasi ili kulete umoja wa Taifa lake?
Pia tambua Ukurain ni Taifa huru hivo kujiunga NATO sio kosa

Mwisho acha kudanganya watu vikwazo vya kiuchumi lazima vitaua uchumi wa Urusi ni swala la muda tu.
Kwa hii thread Leo umepuyanga.
Walijitenga kwa sababu zipi bwashee?
 
Rubbish, huwa nakuunga mkono mambo mengi lakini sikuungi kwa ujinga huu wa kuua watu wasio na hatia, kama mrusi ana nguvu kwanini asiende kuvamia Marekani?
Wewe ni shabiki usiejua chochote! Na ndiyo maana kuna msamiati wa neno “vita” hata biblia inatambua
 
Rubbish, huwa nakuunga mkono mambo mengi lakini sikuungi kwa ujinga huu wa kuua watu wasio na hatia, kama mrusi ana nguvu kwanini asiende kuvamia Marekani?
Wewe ni shabiki usiejua chochote! Na ndiyo maana kuna msamiati wa neno “vita” hata biblia inatambua
 
Kwanini naunga mkono Urusi kuchukua hatua za kijeshi Ukraine?

Naomba nianze utangulize wa makala yangu kwakusema, Dunia ili iwe salama inatakiwa kuwa na wakubwa wawili au zaidi (balance of power), sio mmoja tu anaamua yeye kwaajili ya dunia na hapingwi, Mbele ya Urusi sasa hatutaona vita vya holela vya Marekani na washirika wake.

Sababu ya kwanza ya kuunga mkono Urusi ni kwamba ni hatua muhimu ya kukomesha mauaji ya miaka karibu kumi sasa yanayofanywa na Ukraine dhidi ya Wananchi wa Majimbo ya Luhansk na Donetsk. Kwa msiojua Mtangulizi wa Rais Zelensk wa Ukraine, bwana Petro Poroshenko tangu ashike madaraka 2014 aliendesha mauaji ya wapinzani wengi katika majimbo ya DPR na LPR yaliyotaka kujitenga hadi alipoondoka tu vita havikumalizika.

Alipoingia Zelensk nae akafuata nyayo za mtangulizi wakw, akaigeuza Ukraine kuwa jehanamu kwa aliowaita waasi, aliendesha mauaji makubwa sana hasahasa 2021 dhidi ya raia kule katika miji ya Donbass katika kile alichokiita kudhibiti waasi wanaotaka kujitenga. Dunia hii ilikaa kimya, Urusi ikawa ndio pango la kupokea wakimbizi zaidi la laki tatu,

Kiongozi Jimbo la Donetsk Bwana Denis Pushilin amenusurika mauaji zaidi ya marakumi hadi alipoomba ulinzi wa kimataifa kutoka Moscow, na mwisho akaongoza mapambano na kufanikiwa kujitangazia Uhuru.

Vile vile kiongozi wa jimbo la Luhansk bwana Leonid Pasechnik nae ilimlazimu kutafuta hifadhi ya kisiasa Moscow kwa lengo la kunusuru maisha yake dhidi ya Rais wa Ukraine bwana Zelensk aliyeapa kufuta uasi katika majimbo hayo, Aliongoza mapambano kwa ushirika wa Kiongozi wa jimbo la Donetsk bwana Pushilin na hatimaye wiki jana wamefanikiwa kumshinda Zelensk na Kujitangazia Uhuru.Urusi imeyatambua majimbo hayo kama nchi huru, Belarus na nchi nyingine tano yayari zimetambua. Ukraine imepinga uhuru huo ikaapa kuendesha vita nzito zaidi dhidi ya waliojitenga, Hatua hiyo ikawalazimu viongozi wa mapinduzi waombe msaada wa kijeshi kutoka Urusi. Na wameupata. Oparesheni ya Urusi ndio mwarobaini wa kukomesha mauaji ya miaka zaidi ya kumi sasa, kinyume na hapo miji itaendelea kuvuja damu kila kukicha.

Sababu ya pili ya kuunga mkono Urusi ni kitendo cha Marekani kutaka kujenga ngome ya kijeshi Ukraine, na katika kutimiza hilo Marekani kwakutumia washirika wake wa Nato wakamshawishi avunje Mkataba wa Minsk wa 2015 pamoja na mambo mengine, ulisema Ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Urusi (Ukraine) uliokuwa Umoja wa Kisoviet ya zamani Hautaruhusiwa kujiunga na Umoj wa Ulaya. Katika kibri cha Zelensk akaomba kujiunga NATO. Moscow akajibu kwa moto.

Sababu ya tatu ya kuunga mkono Urusi ni kitendo cha Marekani kupitia shirika lake la kijasusi la CIA kuvuruga dili la Urusi la kujenga bomba la awamu ya pili la gesi maarufu kama NORD STREAM II, ambalo lingelisha gesi Ulaya yote kwa 90% tofauti na sasa mbapo Ulaya inategemea gesi ya Urusi kwa 40% tu, Marekani ameitumia Ukraine kukwamisha mradi huu na baadhi ya nchi za Nato. Kitendo hiki ilikuwa ni uchokozi wa kiuchumi na kijasusi, Jibu la Urusi limeanzia kwa Ukraine kwanza.

Mtazamo wangu vita hivi ni kati ya Urusi na Marekani, na vitaisha kwa nchi hizi mbili kukaa chini na kukubaliana terms and conditions kama mihimili miwili mikuu duniani. Na sio vinginvyo, Ukraine kwa sasa ni uwanja wa biashara ya Silaha ya ulaya na Marekani.

Baada ya vita hii Urusi ataheshimiwa na kuogopwa sana, na vikwazo hivi amini ni geresha tu, havitachukua miezi 18 vitaondolewa, Rejea vikwazo vya 1990 alivyowekewa Urusi alipoivami Afghanustan vilimwathiri nani na viliishia wapi zaidi ya Afghanistan kusambaratishwa? Haya vikwazo vya Urusi vya 2008 alipoivamia Georgia viliishia wapi na vilimwathiri nani zaidi ya Georgia kuwa eneo muhimu la Urusi hadi leo? Vikwazo vya Urusi vya juzi tu baada ya kuivamia Cremia vimefiki wapi?.

Kikwazo ambacho kilikuwa tishio kwa uchumi wa Urusi alichowekewa na EU ni hiki cha kuzuia huduma ya kibenki ya SWIFT, Lakini ndani ya saa 24 tu, Rais wa Urusi Vlamir Putin ametangaza hatua za dharula kukabili vikwazo vya kiuchumi, na haraka Urusi na China wamekubaliana kutumia huduma ya kibenki ya China ya Cross-Border Interbank Payment System, or CIPS. Kwa tafrisi hiyo nikuwa kikwazo cha uchumi hakitaiathiri Urusi moj kwa moja.

Ukweli ni kuwa Nchi nyingi duniani haziwezi kuendesha chumi zao, katika nyanja nyingi kama za kijeshi na mengineyo bila Urusi. Dunia inaihitaji Urusi kuliko Urusi inavyo ihitaji dunia yenyewe. Japo wanategemeana. Mataifa ya Umoja wa Ulaya (EU) yapo 27, ukijumlisha na Marekani jumla ni nchi 28 tu, haya mataifa sio yote yanaipinga Urusi, Dunia ina nchi 195 + Donetsk na Luhansk, ni 197, Sasa jiulize nchi 164+ ziko upande upi?. Bado mtu anasema Urusi imetengwa na dunia? Basi huyo mtu haijui dunia sawasawa.

Ni wazi kwamba, Dunia leo iko mapande matatu, kuna Urusi, Kuna Uchina na kuna Marekani... Kwenye nchi 28 Uchina hayuko huko, zingatia kuna nchi za kati zenye uchuki mkubwa ambazo ni India hayuko na Ukraine, huko Brazil hayuko huko na Ukraine... Na hawa wanamuunga mkono Mrusi.... Dunia sasa inastawi na hii ndio balance ya dunia na inapumua vizuri sasa.
 
Pro ukrainians watapinga[emoji4]
IMG_20220302_182926.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfano urusi ndio iwe tz. Chifu angaya ndiye awe putin. Unafikili chadema wangeunga mkono hiyo vita?? Hiyo ndio hali iliyopo urusi
Mfano wa chifu Hangaya na CHADEMA hauna uwiano Urusi. Kwanza, naamini Hangaya hana akili mbovu kiasi hicho.

Pili, hakuna "CHADEMA" Urusi. Wapinzani rasmi wa Putin ni ama wamekufa, au wako jela/kizuizini au wako hoi hospitali. Putin hataki upinzani kabisa. Kauli yake ndiyo ya mwisho. Hakuna chama cha siasa kilichosikika Urusi kuhusu vita hiyo. Bunge halina kauli zaidi ya kupitisha tu. Wananchi ndio wanaondamana barabarani na kulalamika mitandaoni kuhusu vita hiyo na vikwazo vinavyowaathiri.
 
Umepuyanga

Back
Top Bottom