Kwanini naunga mkono Urusi kuchukua hatua za kijeshi Ukraine?

Usichanganye Chadema na Yericco
 
Ccm leo imegoma kupiga kura ya kuihukumu Urusi, Una maoni gani kada mtiifu?
 
Mkuu, tahadhari kuponda BBC na CNN. Hizo sio media za propaganda. BBC inaendeshwa kwa bajeti ya serikali ya UK, lakini Waziri Mkuu wa UK akiharibu inaongoza mashambulizi kumwajibisha. CNN ni private media ya US. Lakini iko huru kuibua uozo wowote wa serikali na taasisi za US.

Kwa mfano, katika harakati za kuondoka Afghanistan mwaka jana, jeshi la US lilituma drone ikaua watu 10 wa familia moja na kudai walimlenga kiongozi wa ISIS aliyekuwa akipanga mashambulizi dhidi ya askari wanaoondoka. CNN walichunguza na kutangaza kimataifa kuwa si kweli; aliyeuawa ni mfanyakazi wa NGO ya kimataifa na familia yake. Pentagon hatimaye wakakubali kosa. Hapa kwetu CNN wangeitwa wasaliti wametoa siri za jeshi.

Media outlets kama RT na CGTN, na zingine za India ndizo zimejaa propaganda za serikali.

Kifupi, kuna source kubwa habari za kimataifa zikiwemo tatu kubwa: Agence France-Presse (AFP), Associated Press (AP), and Reuters . CNN, BBC, Aljazeera wanapata habari zao nyingi toka huko na source zao wenyewe. Unaweza kwenda moja kwa moja kwenye mitandao ya AP, AFP na Reuters kwa kujihakikishia zaidi kuliko huko kwingine. uwe tayari kusubscribe.
 
Mkuu naunga mkono hoja lakini kuna swali fikilishi je vipi itakuwa iwapo marekani wataamua kutumia nguvu yao ya ushawishi kwa mataifa yenye nguvu kivita ikiwemo islaeli kuungana ili kumpiga mrusi?

Hipi hasa nguvu ya mrusi kivita kushindana na mataifa haya?

Na ikitokea mrusi ameshindwa hiyo vita nini hatima yake ya nguvu ya kivita?

Mwisho nafaham anaetafutwa ni mmarekan katika mgogoro wa ukrein vipi Kama ataamua kutosogea uwanjani lengo la mrusi litatimiaje kwa marekani inyotafutwa?

Nawasilisha hoja mkuu.
 
Andiko lako limejaa bias sana umeonesha mahaba na russia hivyo wenye pro amarica lazima wakupinge, nimefuatilia maandiko yako sana ila hili limekaa hovyo sana
 
Huelewei vikwazo vya uchumi vya magharibi vinavyofanya kazi, ni kilaza eneo hilo ndio maana unafikiri China atamuokoa Russia katika kuzama kiuchumi.
Ulimwengu wa magharibi ukikuwekea vikwazo utaifuata njia ya Zimbabwe na Korea Kaskazini tu, Utaishia kuchapisha noti za laki, milioni, bilioni na trillion, utakuwa kituko.

Washirika wakubwa wa biashara wa China anaanza Marekani, Umoja wa Ulaya, Japan na nchi nyingine nyingi kabla ya Urusi ambayo hata haiko kwenye top ten ya China. China sio mjinga akubali kukiuka vikwazo vya Marekani na EU apoteze soko lake kubwa kuliko yote, China siku zote anatanguliza maslahi yake mbele kwanza kabla ya jambo lingine lolote.
Chochote atakochafanya China kuisadia Russia kiuchumi kwa sasa ni sawa na kuchota maji kwa kijiko kwenye pipa, yatapungua ila kwa tabu sanu.
 
thanks for your well informed article. haujaandika kwa kusukumwa na hisia wala ushabiki, umeandika ukweli halisi.

bandiko hili nitalitumia kama reference ya kile kinachoendelea sasa. nitakuwa narudi kulisoma mara kwa mara.

update:
we jamaa kumbe nimekupa sifa za bure, ume copy na ku paste makala ya mtu mwingine bila hata kutoa credit. sio poa.
 
Ukraine haijakubaliwa NATO wala EU. US hawakuweka majeshi au silaha zozote Ukraine. Situation ni tofauti kabisa na ya Cuban Missile crisis ya 1962 ambapo USSR walisimika makombora ya nuclear Cuba yakagunduliwa na ndege za kijasusi za US.

Haiyumkiniki leo hii Urusi kushambulia Ukraine na kuua watu kwa sababu hawajapewa guarantee na NATO na US kuwa Ukraine haitajiunga na NATO huko mbeleni. Ni kama kumpiga mtu panga leo kwa vile hajakuhakikishia kuwa hatakushambulia kwa bunduki ukija kumuudhi siku zijazo! Strange logic. Vita si suala la mchezo kiasi hicho. Halafu wanaouawa na kujeruhiwa ni ndugu zao wa warusi, sio wamarekani. Marekani ni kama watazamaji compassionate tu. Sad!
 
Vita vingi vya kiholela na migogoro mikubwa duniani husababishwa na madikteta wanaokaa madarakani muda mrefu, wanaopuuza katiba na kukandamiza haki za raia wao. Hiyo ni kuanzia Ujerumani ya Hitler, Italia ya Mussolini, South Africa ya Makaburu, Syria ya Assad, Libya ya Gaddafi, Uganda ya Amini, Iraq ya Saddam, Afghanistan ya Taliban, DRC, Biafra, Chad, Ivory Coast, CAR, Rwanda, Burundi na nyingine nyingi. Madikteta waliozigeuza nchi zao kuwa mali zao binafsi kama alivyofanya Putin Russia ndio chanzo cha machafuko siku zote.
 
vipi kuhusiana na IRAN?
UKRAINE acha anyooshwe kama mnaweza ninyi ama NATO mukamsaidie maana haya maneno hayamuepushi na kipigo kizitooo
 
Huyu PUTIN na yeyey ni dikteta uchwara mwenye tabia ya kuuwa wapinzani wake mchana kweupe na kuwafunga kwa tuhuma za ugaidi na uhujumu uchumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…