Lovelovie
JF-Expert Member
- Oct 2, 2021
- 12,582
- 26,053
A
AminaKwanini naupenda mti huu.
View attachment 2415649
Kuna historia kubwa sana ya mazingira niliyoishi kwenye udogo wangu .
Miti mingi ilikua ni hii , wenyewe tuliita mi Krismas
Kuchanua kwake kuliashiria holiday-sikukuu imekaribia ,
Na shule inakaribia kufungwa ,
Vilevile Krismas haikua mbali hivyo nguo , viatu vipya vinanukia .
Ni miti maalumu sana ,
Nikiona inachanua nafarijika kukumbuka mambo kemkem yaliyo burudisha maisha yangu zama hizo .
Kiimani .
Mti huu kwangu unafumbo la imani kwa waliokata tamaa.
Mti huu hunyauka kabisa kuanzia Julai , Agost , Septemba na Octoba ....ni mti ambao hukwepa ukali wa jua na ukame kwakuruhusu kupukutisha majani yote .
Huungua kabisa na hutia huruma .
Inapofika wiki ya 3 ya Octoba miti hiyo huchanua maua , na maua huendelea kuufunika mti usio na majani .
Kiimani ,
Mungu husema nasi kupitia mazingira kuwa katikati ya dhiki uskate tamaa .
Katikati ya mateso usikose tumaini ,
Hata unahisi dunia inakuelemea Mungu huleta faraja zake kwa namna aitakayo na apendavyo.
Mti huu kwangu hunifunza uvumilivu , kusamehe na kutojiumiza kwa mambo yaliyo nje ya uwezo wangu.
Heshima kwa Samson Mwasakafyuka Ndwanga