Kwanini naupenda mti huu

Kwanini naupenda mti huu

Kuna raia moja wa Kilimanjaro anapenda kuingia jf kwa ajili yako.
Jamaa anakukubali haina mfano.
Ukiitaja jf yeye anataja Bujibuji halafu anacheeeka.

Cc Maxell Remy [emoji1787][emoji1787]
Let him be blessed by my Lord Jesus Christ
 
Kwanini naupenda mti huu.
View attachment 2415649
Kuna historia kubwa sana ya mazingira niliyoishi kwenye udogo wangu .

Miti mingi ilikua ni hii , wenyewe tuliita mi Krismas

Kuchanua kwake kuliashiria holiday-sikukuu imekaribia ,
Na shule inakaribia kufungwa ,
Vilevile Krismas haikua mbali hivyo nguo , viatu vipya vinanukia .

Ni miti maalumu sana ,
Nikiona inachanua nafarijika kukumbuka mambo kemkem yaliyo burudisha maisha yangu zama hizo .

Kiimani .
Mti huu kwangu unafumbo la imani kwa waliokata tamaa.
Mti huu hunyauka kabisa kuanzia Julai , Agost , Septemba na Octoba ....ni mti ambao hukwepa ukali wa jua na ukame kwakuruhusu kupukutisha majani yote .
Huungua kabisa na hutia huruma .

Inapofika wiki ya 3 ya Octoba miti hiyo huchanua maua , na maua huendelea kuufunika mti usio na majani .

Kiimani ,
Mungu husema nasi kupitia mazingira kuwa katikati ya dhiki uskate tamaa .

Katikati ya mateso usikose tumaini ,

Hata unahisi dunia inakuelemea Mungu huleta faraja zake kwa namna aitakayo na apendavyo.

Mti huu kwangu hunifunza uvumilivu , kusamehe na kutojiumiza kwa mambo yaliyo nje ya uwezo wangu.
Heshima kwa Samson Mwasakafyuka Ndwanga
Shukrani kaka Bujibuji Simba Nyamaume nimepata faraja kubwa na ukomavu katika uvumilivu
 
Kumbe wewe mtoto wa kishua?

Ethiopian restaurant, Jacaranda, knight support, Mezaruna, 40/40 lounge...Impala?
Kuna Watanzania wa kawaida kabisa tunaishi maeneo hayo mkuu,inategemea eneo lilinunuliwa lini.
 
Ni jamaa flani muungwana na hana makuu kabisa.
Huyu mtu unaweza kumchukukia poa lakini sivyo.
Ana kitu cha tofauti sana
True aisee. Unaweza kumuona kama comedian fulani hivi, lakini ndani ya mistari yake kuna hekima kubwa sana bro
 
Back
Top Bottom