Kwanini nawachukia wanaume?

Sasa we dada alipokukula rafiki wa babako wa kwanza si ungeshtuka!!!Sasa ukaendelea tena!Then ukaamua kubobea!!sasa we kubadilika ni ngumu dada...
 
pole sana mcharuko ila wanaume ndo tulivyo wapo wakweli na wauongo ni wengi sana nawalaumu sana rafiki wa baba yako ambao walitumia nafasi hiyo kupata utamu wako kwajinsi ilivyona chuki na sisi ungekuwa mchawi ungetuloga sana wote wanaotembea nawe
 
pole mwaya, nakuonea huruma sana ila ni mapito tu hayo. Unahitaji counseling maana utakuwa umeathirika kisaokolojia na ndio maana unawaona wanyama. Jaribu kutafuta counselling ingawa sijui vituo vyao.
survival for the fittest, the weak are always in trouble. Unyonge wa akili, mwili na roho ni mateso, tabu kubadili fikra potofu za mwanadamu.
 
Pole sana kwa uchungu ulionao.Usisikitike kwa kudhani hao marafiki wa babako walikutongoza kwa sabab ni yatima,hapana mwanaume mkware hana condition ni wasichana wengi wanatongozwa,wanarubuniwa na hata kutembea na marafiki wa baba zao.
 
Mcharuko!
kwanza nianze kwa kukupa pole kwa yalikukuta, nimesikitika sana sana. Lakini napenda kukuambia kuwa Mungu bado anamakusudi na maisha yako, GOD LOVES YOU!!! maana hata kule kujitambua tu, na kuamua kushare hapa, inaonesha ni jinsi gani ulivyokuwa unatenda bila kupenda. Wanaume kama ulivyosema, baadhi ni wa ajabu sana, lakini yuko mmoja, ukimpata huyo, maisha yako yatabadilika; maana anasema yeye ni Mungu wa yatima, Mungu wa wanyonge, JESUS OF NAZARETH, he will give you the perfect peace, mpe yeye maisha yako sasa, na atabadilisha hata mtizamo wako wa maisha. Surrender your life to him, he is faithful and trustfully.
 
Basi tusamehe na sisi wanaume tulioponzwa na hayo mabaradhuli yaliyokufanyia undava!!!

Hebu fafanua kidogo mkuu ,sidhani kama nimeelewa vizuri hapa! Some bad feelings tickling in my head!
 
emeeeeen! Praise the lord.

Halleluyah! Halafu wewe hebu ni pm.nianze yale maneno yetu kubembeleleza kabla wanoko hawajaja kututibulia.

Back 2 topic: Sipendi kuwatendea wanawake vibaya nikiwa na imani kwamba nina mtoto wa kike na ndugu wa kike pia kutokana hali kama ya dada mcharuko ni watu wengi sana wanapitia hali kama yake lakini hatujui na hawako wazi kwa kujionyesha jamvini kama alivyofanya ila ukweli ni kwamba tuna watu wengi sana wa aina yake ila hawajiuzi waziwazi kama mnavyodhani na hata wengine tumejichanganya nao na kutaka kufanya mahusiano ya kudumu lakini unakuta tayari ameshaathirika ki saikolojia then tunawalaumu.

ushauri: dada kaa chini ingia chumba chako cha siri mwombe Mungu atakusamehe na kukupa unachotamani kulingana na hitaji la maisha yako ya baadaye na usiwasimulie watu matatizo yako maana wengine watachukulia kama ndiyo mlango wa kukusema, kukudharau, kukutangaza, kukusimanga na hata wengine kukutongoza.
 
Pole sana wangu ila usife moyo kiivyo muombe atakusaidia na utasahau yote.
 
dah,am so sad!pole sana,muombe mungu atakusaidia,tafuta biashara nyingine na uache hiyo.
 
Sio vizuri kwa wanaume ku-take advantage ya kufanya ngono pale msichana akiwa na shida. Nimefurahi kusikia sasa hivi umeacha biashara hiyo. Kaa tulia na umwombe Mungu, kutupenda sisi sio lazima kama moyo wako haupo huko. Unaweza kuamua kuishi maisha ya bila ndoa.
 
Pole sana dada hayo ni mapito tu na mshukuru Mungu kwakujitambua na mwombe sasa akubadilishe. Vp bado upo chuo au ashamaliza. MUNGU NDIYE JIBU PEKEE JUU YA MATATIZO YAKO
 
Pole Dada yangu kwa Maswahibu yaliyokukuta,jamani wanaume wenzangu tabia hii haifai jama. Hebu fikiria kama Huyu Dada angekuwa Mwanao halafu ukawa unashuhudia namna Majirani na Marafiki zako wanavyofanya naye Uchafu wa Namna hiyo! Inauma sana..lakini dada hayo yamepita Wapo wanaume wengi waliotendwa sana tu na Wanawake wao lakini hawakuwachukia wote, hivyo nakusihi na nakushauri urudishe imani yako kwetu na Utampata akupendaye kwa dhati
 

Pole sana ila sio wote tuko kama hao marafiki wa marehemu baba yako.
 
Dah! Mpendwa unamhitaji mungu zaidi ili uweze kuendelea mbele. Jiombee, mwaga moyo wako na umuombe mungu akusamehe,uwasamehe hao maaluni na akusaidie ujisamehe. Kujisamehe ni muhimu sana. Mungu akusaidie usikutane na ukimwi hadi ujikomboe. Aisee! I need fresh air...
 
Pole sana dada,ila unaitaj counseling,ungekuwa karbu ningekufanyia counseling coz nipo hapa udom napiga guidance and counseling,na hlo swala lako ,tiar psychologcaly umesha be affected,pole sana uko cbe ya wap' ,kama uko tiar kupewa counseling ,tel me. Au nitumie sms.tuwasiliane
 
Pole sana lakini pia nakupa hongera umekuwa muwazi. Pia nakupa hongera kwa uamuzi wa kwenda shule. Jaribu kumwomba mungu na kuwa buzy na mambo ya shule. Je upo mwaka wa ngapi?
 
Kwanza nimesikitishwa sana na story hii bila kujali uhalisia wake. Pia ungebadilisha hiyo ID. Pamoja na hivyo unatakiwa uone mapungufu yako. Hukujipenda tangu mwanzo. Ulifiwa na mama yako ukiwa form 1, ukafiwa na baba ukiwa form 3, 90% ya uliowaomba msaada wakakutongoza, kuna 10% imebaki uliifanyia nini? 'Wanaume ni mashetani' wale wanawake malaika wote kuanzia mashosti zako shuleni, mtaani/kijijini, ndugu zako malaika wa kike, walimu wa kike, waumini wenzako wakike iwe kanisani au msikitini... hao wooote walifanya nini??? Siwaungi mkono waliokutongoza lkn usipoona mapungufu yako kuingilia ndoa za hao mama zako kwa kisingizio cha kutafuta misaada, nakusikitikia sana. Wewe binafsi unaweza kutuwekea hapa uliwadhulumu wanaume wangapi hata ambao huwajui? Maana wadada wengi mkibalehe tu mnaanza wizi na utapeli wa kutumia hela za wanaume wote wanaoingia kwenye anga zenu hata kama hamna mpango nao.
 
Jamani pole sana yaani nimesoma nimetoa chozi

nime imagine kuwa lazima sio wewe tu uliyepitia haya
na pia nimeimagine mibaba marafiki wa wazee wangu waseme hivi ningefanyaje? naona shida labda na mie ningeingia mtego wao. nashukuru nimekua wazee bado wapo pia.

sasa vipi usome uanze maisha mapya pata mtu wa kuongea nae lia lia toa machozi yote ya chuki then labda utajisikia nafuu

soma soma binti then utaweza waonyesha hao mibaba kuwa wewe umesimama na una elimu yako na naomba usiendelee nao najua kuna shida jitahidi sana naogopa yaani usije pata magonjwa jiangalie wazee wapo lazima wanaweza kuumia walipo kwa tabia hii

Mungu atakubariki.

Pole sana anza kuwa wa Mungu na baraka zitakuzidia.

Masomo mema
 
Pole sana binti, sahau mambo yaliyopita uliache na hilo jina la mcharuko na mawazo ya kimcharuko, Mungu anakupenda sana ndo maana uko hai mpaka leo, na ana mpango na wewe. ukipata shida sana nitafute nikusaidie mahitaji yanayohusiana na shule tu ili angalau umalize chuo tu.
 
Na utaendelea sana kuwachukia ila wenge likikutoka utatupenda tu...kwa asilimia 90 ya wanaume watakutongoza kulingana na unavyojipresent kwao..
si rahisi mwanaume kukutongoza kama anakuona una msimamo flani isitoshe wewe ndio umewalegezea legezea unakwenda kuomba msaada huku unang'atax2 vidole unategemea nini?
Na nani aliyekwambia lazima ugawe K ili usaidiwe hukuwa na means yoyote ya kufikiria kujikimu na maisha? wangapi ni mfano bora wamepitia hayo maisha na hawakuuza K? je unadhani wewe ni wa kwanza kukutwa na hayo matatizo?
nyie ndo the same batch ya kina Sofia Simba nadhani production yenu ilikuwa moja sema we sijui umechelewa ukiwa wapi ...

sasa hapa unapoandika unaomba huruma ya jamii au ndo namna gani ...Nawachukia wanawake kama wewe kuliko kitu kingine ...
huwezi kutegemea K kwa kuishi halafu ujisifu

kwa taarifa yako hata kama unawachukia nadhani hata hapo hizo unazodisco lazima unaonyesha K na bado wataendekea kukutumia sana kama flash disk na hawatachagua port ya kuweka ...ukimaliza kusoma wakati unatafuta ajira utakutana nao na watadigg kama kawa ....


I hate a woman like u... wanaume ukijiheshimu utaheshimika haswaaaa ukijiwema watakuwema vile vile...

The BOSS alishasema hapa kuwa kuna wanaume na wavulana ninaimani kabisa ungeamua kutulia na kusema nia yako ya kusoma na kuomba msaada kwa wanaume na si wavulana UNGEPATA MSAADA na ungesoma na mahitaji ungepata smoothly ..sasa kwa sababu uliamua kuweka K mbele kama tai ndo hayo unayotwambia hapa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…