Mara nyingine unaweza kujiuliza kwanini mtu kachagua ID fulani, Unaweza kucheka, kuchukia au kubaki kawaida na maswali yako. Kwa upande wangu nastahili kuitwa/ kujiita mcharuko. Naongea kutoka moyoni kwa sababu naamini ni Mungu pekee ndo ananijua vizuri kwa wengine hapa jukwaani nitaendela kuwa kivuli.
Mwk 2001 nikiwa kidato cha kwanza nilifiwa na mama yangu mzazi. Nilikuwa mtoto wa pekee kwa baba na mama. Nikabaki na baba peke yake ambaye mara nyingi alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kisukari hadialipopoteza maisha miaka miwili baadae. Tayari maisha yalishakuwa magumu lakini baada ya kufariki baba ugumu ulizidi.
Mara nyingi nilikuwa naenda kuomba misaada kwa marafiki wa karibu wa baba wengi wao walinisaidia lakini wakaanza kunitongoza. Sielewi ni kwanini wakati baba yuko hai nilikuwa mtoto wao lakini baada ya kifo cha baba wakaanza kunifanyia hivyo. Asilimia 90 ya wanaume niliowaomba msaada walinitongoza. Nilikuwa sina jinsi. Wengi nilifanya nao...... lakini hawakunisaidia tena baada ya msaada wa kwanza
na wao kupata walichohitaji.
Toka Muda huo maisha yangu yamekuwa ni ya kuuza mwili wangu mpaka mwaka 2008 ambapo nilijiunga na chuo cha Elimu ya Biashara CBE. Hapo sikuwa na jinsi ndo nikaingia kwenye biashara rasmi ya uchangudoa. Sitatokea kumpenda mwanaume maisha yangu yote. Na hata pale nilipoleta thread kuhusu wanaume wafupi nilikuwa nimezungumza kutokana na uzoefu nilioupata kutokana na biashara hiyo.
Najitahidi kuileta akili yangu katika hali ya kawaida ili niwapende wanaume lakini nashindwa kwangu mwanaume ni mteja na mtu katili asiye na huruma. Nawachukia nawachukiakutoka moyoni. Rafiki wa karibu wa baba yangu ambao nimetembea nao mpaka sasa ni 5. Hivi kweli kuna haja ya kuwa na imani na wanaume?
Story yako inaweza kuwa ya kusikitisha kwa upande mwingine na ya kulaumiwa kwa upande mwingine. Kwa ridhaa yako nirususu kusema yafuatayo:
1: Ni kweli kwamba watu huchagua majina mara nyingi kuendana na tabia, lifestyle na maisha yao kwa ujumla, yeyote atakayepinga hili hana uelewa wa kutosha kwa hapa tunakubaliana.
2: Kwa upande mwingine, Your Life style is Your Own Doing!
Nikiongelea zaidi hapa niseme, Matatizo yote mtu anayokumbana nayo ndiyo yanayomfanya awe mtu katili au mtu mwema, awe jasiri awe akate tamaa. Na jambo zuri ni kwamba, mtu anapokabiliwa na matatizo anakuwa na WIDE WINDOW OF CHOICES. Ukipata nafasi usoma kitabuu Cha Mtanzania mmoja kiko amazon, 'Anaother Story..Not! na Siri Za Maisha, mwandishi, Dr. Isangula anasema ' Ni lazima kila binadamu autane na matatizo ili aweze kubapata 'Wisdom'' . Kwamba 'Problems if met in the right ways,they can be stepping stones to success'' Kina mambo mengi sana hasa akiongelea falsafa ya Vinctor Frankyl na Pavlov, kwa kunukuu tena kwama ,Pavlov alisema ukiwa na stimuli au kichochea una respond na wewe huna uamuzi kwa response zako' mfano umefiwa na mzani unasikitika na lazima utafute msaada,unatongozwa na hao jamaa na unasema huna jinsi. Lakini Victor Frankyl anasema Kila mtu anapokubana na matatizo kuna dirisha pana la kufanya maamuzi ,kwamba kuna 1) Imagination- Uwezo wa kujenga picha ya jinsi maisha yako yatakavyokuwa kulingana na maamuzi yako, 2)Independent will kwamba hakuna anayekulazimisha kuamua unachoamua,yaani ni wewe mwenyewe na matatizo yalikusukuma tu lakini hayakukulazimisha 2) Self awareness- Uwezo wa kutambua madhara yatakayojitokeza kutokana na maamuzi yako mfano ni lazima ulifikiria kuhusu Ukimwi,Mimba maginjwa ya zinaa kabla ya kuamua kutoa uloda 4) Conscience -ulitambua kuwa unacho/utakachofanya ni kinyume cha maadili,tamaduni na misingi ya dini. Ukifikiria yote hayo, naendelea kunukuu ' Then you have a Freedom and Power to choose... and
though you Have the Freedom to Choose, there is always the Counter force to your Freedom, If the FORCES inside you are so STRONG than your FREEDOM then you'll make the WRONG DECISION''
Hapo unaona kuna Counter force ambayo kwako ilisukumwa sana na matatizo yako lakini mwisho wa siku ulikuwa na UHURU wa kuchagua na labda unegekuwa hauko katika biashara hiyo na ungekuwa
mtu mwema kabisa. Simaanishi wewe si mwema, lakini kwa kuwa una chuki dhidi ya wanaume na unawaona makatili hapo umepoteza wema. Mwanaume kukutongoza si kosa, kosa ni wewe kukubali! Si vema kusema 'Hukuwa na jinsi' hapo juu tumeona ulikuwa na Freedom ya kuchagua. Kama unegesema walikubaka hapo inekuwa story nyingine lakini, '
Uliamua kukubali' Hapa neno muhimu ni kuwa
Uliamua kukubali! Ukaamuza kuwa na Maisha yako uliyo nayo sasa! Ukaamua kuziba hisia za utu wako!
Ukaamua Shida zikuongoze kufanya maamuzi mabaya!
Ukaamua kuondoka nyumbani na kumfuata mwanaume kama ni gesti au wapi!
Ukaamua kuvua nguo mwenyewe ukika gesti!At least
uliamua kutafuta shule lakini ulipofika hapo shuleni CBE
ukaamua kuwa changudoa. Sehemu nyingi ya Maelezo yako ULIAMUA mwenyewe! Ukweli ni kwamba hapa si Wanaume bali ni maamuzi yako mwenyewe
FAHAMU KUWA HAPA SIKUHUKUMU bali najenga hoja yako kwa kuwa JF ni sehemu ya Kusaidiana
NINI CHA KUFANYA
Awali nilinukuu kuwa kila mtu lazima apitie matatizo ili apate wisdom na mwishowe awe mtu mwema au mbaya. Kwa kuwa inaonekana una Uwezo wa KUAMUA, kumbe sasa wawezo kuyatumia matatizo yako kama STEPPING stone kupata wisdom na SUCCESS. Waweza sasa KUAMUA kuacha maisha yako. Nakushauri utafute kitabu cha huyu jamaa kina Busara nyingi ambazo siwezi kuzieleza hapa. Acha ninukuu kwa mara ya mwisho, 'Maisha au matatizo uliyonayo sasa yametokana na Maamuzi yako ya siku za nyuma, ndiyo maana una maisha mazuri au mabaya kabisa kupindukia, kwa kuwa maisha ya siku za mbele FUTURE ni muhimu zaidi na kwa kuwa huwezi kuibadili PAST yako, Unayo nafasi ya kuishi maisha mazuri sasa ili FUTURE yako iwe nzuri. Maisha unayoishi sasa yatakuwa PAST katika FUTURE yako na kama ukiishi kwa UBAYA sasa basi Hukumu yake utaipata katika FUTURE yako kama maisha ya PAST yako yanavyokuhukumu sasa, sasa ambapo ni FUTURE ya iliyokuwa PAST yako'' Japo hata mimi nilipata shida kuelewa jamaa anamaaisha nini kwa PAST na FUTURE ila ukisoma kwa utulivu utajua anamaanisha nini.
Wewe si Mcharuko, unayo POWER within You! Una nafasi ya kubadili maisha yako hasa kama hujawa addicted na UCHANGUDOA. Kaza msuli katika Shule, Soma mama, Ukombozi wa Masikini ni elimu. Taratibu jiondoe katika Uchangudoa. Wanaume japo wapo wakatili wapo wenye utu wanaojua kupenda, wapo vijana wa saizi yako. Nimeambatanisha link za vitabu vya huyu Dr Isangula ambavyo vitakusaidia katika hii transition ya Kujenga Maisha yako Mapya, kujenga Future yako! Maisha ni zaidi ya kuwa na fedha Mfukoni! Maisha ni kuishi kwa Weama na WISDOM
All the best sasa UNAPOMUA kujenga FUTURE yako
Nisamehe kama nimetumia maneno makali ya kukukwaza na pia sikufanya spell check kwa kuwa nimebanwa kidogo na majukumu na nilitaka upate ujumbe
http://www.amazon.com/Siri-Za-Maish...=sr_1_1?s=books&ie=UTF8&qid=1319814431&sr=1-1
http://www.amazon.com/Another-Story...r_1_12?s=books&ie=UTF8&qid=1319814454&sr=1-12