Kwanini nchi za Afrika ikiwemo Tanzania bado maskini licha ya kupokea Misaada na Mikopo ya mamilioni ya Fedha kutoka nchi zilizoendelea? - Part I

Wanananchi wengi hawana akili
Kama huna akili ni wewe tu.

Soma historia za maendeleo ya ulaya, Afrika na mambo yaliyojitokeza kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni. Jifunze uhusiano uliopo kati ya watawala wetu na sisi watawaliwa wao.

Mzungu halali, anafikiria namna ya kuinyonya Afrika. Anatumia hela nyingi kutengeneza mifumo ya kiunyonyaji ili tu awe mbele ya Afrika all the time.

Tatizo lilianzia pale teknolojia ya Afrika kupigwa marufuku na kuonekana ya kishenzi. Tukapokea dini zao zikitoa misaada bure ikatulemaza.

Hali hii hadi leo bado ipo. Afrika ikigundua kitu, wazungu hutafuta namna ya kuifanya ionekane haina ubora. Wakiona ina manufaa kwao, mgunduzi watamchukua aende kwao. Akiwa mbishi wanamwua.

Wanataka Afrika liendelee kuwa soko na siyo chanzo cha ugunduzi wa maendeleo kwa namna yoyote.

Kifupi matatizo ya nchi za Afrika ni planned na weupe. Halafu wewe unasema hatuna akili. Kama huna akili ni wewe.
 
Hiyo misaada haifiki chini inapigwa juu kwa juu na watawala kisha wanarudi kuficha mabenk ya ulaya.
 
Sawa mkuu. Lakini unadhani viongozi wetu wanapenda kushindwa?

Rais anaingia madarakani akiwa na mipango mizuri sana ya maendeleo. Analojaribu kuitekeleza, anakumbana na vikwazo hadi vya kifo. Mwoga huishia kufuata maagizo ya watishiaji na jasiri kama Gaddaf na Magufuli huishia hapo walipoishia.

Dunia ina siri nyingi, wahusika hawasemi. Ni mropokaji Magufuli tu alijaribu kusema ya ndani na mwisho wake tumeuona.

Mama anapepea na kilemba si kwa kupenda. Anafuata maagizo ya ndani na nje ili aishi.
 
Njia pekee ya kuisaidia afrika sio kuwapa pesa bali wao ndo waje wafanye hitaji watukabidhi na sio kuwapa pesa watawala zinaliwa juu kwa juu
Waje wajenge vyuo,shule,vituo vya afya,visima, barabara na wakabidhi kama afanyavyo Japan.
 
Mfano halisi wa Tanzania aside na akili ni were, Africa ndio pekee iliyotawaliwa? Nchi za Korea, Vietnam, Singapore,India n.k hazikutawaliwa na kupewa misaada baadae na wakoloni?

Watu wenye akili watakubali vipi na teknolojia Yao ipigwe marufuku?
Kwenye global trade Sub Sahara Africa hai account hata 0.5% ya manunuzi ya bidhaa, sasa nani awategemee kwa soko masikini wakubwa kama hawa?
Soma kwanza historia ya Dunia, na uchumi wa Dunia sio kuamini propaganda za akina Polepole
 
Misaada haisaidii
Imagine unapewa msaada then unapangiwa ukanunue chanjo ya corona
Uongo utakuuwa dogo, chanjo tumepewa bure kama ambavyo tunapewa bure kondomu, vyandarua, kujengewe vyoo kwa msaada wa Marekani etc etc by the way unajua maana ya Aids, Grants & loans??
 
Misaada inakuja na masharti mfano
Nunua chanjo ya corona
Masuala ya jinsia
Usijenge kiwanda nunua dawa toka kwao
Pia mikopo inakuja na masharti pia
Na asilimia kubwa ya mikopo inaishia nje ya malengo.kwenye matumbo ya wanasiasa
 
Ni ngumu mno kuendelea kwa kutumia misaada yenye masharti uzitumiaje bila kusahau riba.
Wazungu wakiona kiongozi hataki misaada wanamtafutia zengwe mf. Gadafi,JPM nk.
Hata waswahili husema mtegemea Cha nduguye hufa maskini.
 
socialism imeharibu sana watu akili, si chama chenu ndo kinakoleza moto wa misaada, magufuli alivoamua tuanze kujitegemea mkamuona diktetea kwa kifupi nyie mnatakiwa wote mumfuate mbowe ukonga ni janga kwa hii dunia
Kwani wewe umemfuata kaburini kwake au kuzikwa naye?
 
Chanjo sio bure go and check your source
Uongo utakuuwa dogo, chanjo tumepewa bure kama ambavyo tunapewa bure kondomu, vyandarua, kujengewe vyoo kwa msaada wa Marekani etc etc by the way unajua maana ya Aids, Grants & loans??
 
Kuna koo Zimeendele kama za akina Dewji, Mengi, Bakhersa nk

Unadhani kwa nini ukoo wako ni choka Mbaya kimaisha? Ni uongozi mbaya ndani ya ukoo wenu, ubinafsi, uvivu na ufisadi wa viongozi wako wa ukoo?
Nazungumzia maendeleo ya jumla sizungumzii kuchomoka kwa mtu mmoja mmoja.
Kwann nchi za afrika ya weupe wao angalau wameendelea kwa ujumla kuliko afrika ya weusi.
Kama wakoloni kwa mda mfupi wao waliweza tuletea maendeleo makubwa Sana nyie ccm mmeshindwa vipi.Soon tunaingia jubilee miaka100 tukiendelea kusaidia kujengewa vyoo vya shule.
 
Ni ngumu mno kuendelea kwa kutumia misaada yenye masharti uzitumiaje bila kusahau riba.
Wazungu wakiona kiongozi hataki misaada wanamtafutia zengwe mf. Gadafi,JPM nk.
Hata waswahili husema mtegemea Cha nduguye hufa maskini.
Hayo ni mawazo ya kikomunist,mbona ulaya, Asia, latin america mbona wao wameendelea kwa misaada hio hio wanayopewa afrika.
 
Sio kweli idadi ya watoto iwe kikwazo cha kutoendelea
 
Misaada sio kwa ajili ya afrika pekee hata nchi za ulaya zinapewa misaada.Misaada sio tatizo tatizo inaishia wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…