Kwanini nchi za Afrika ikiwemo Tanzania bado maskini licha ya kupokea Misaada na Mikopo ya mamilioni ya Fedha kutoka nchi zilizoendelea? - Part I

socialism imeharibu sana watu akili, si chama chenu ndo kinakoleza moto wa misaada, magufuli alivoamua tuanze kujitegemea mkamuona diktetea kwa kifupi nyie mnatakiwa wote mumfuate mbowe ukonga ni janga kwa hii dunia
Propaganda tu tujitegemee kwa sera zipi hali tulikuwa tunaenda kucollaps Mungu asingeingilia kati.
Huwezi jitegemea kama unaua sekta binafsi,yaani unaua export then tujitegemee.
 
Kama nchi zinashindwa ama hazitaki kulipa madeni ya ndani wananchi wake watainukaje kiuchumi
 
True kabisa.
Nyerere alikuwa ni mzuri kwenye kuongoza watu lkn hakuwa mzuri kwenye uchumi thus hata uchumi alivyoachiwa na wakoloni akaua.
 
Haya ni mawazo ya kikomunist asili yake ni miaka ya 70 toka chuo cha patrick lumumba Urusi yaliandaliwa na warusi enzi za vita baridi lengo ni kujenga chuki kwa kambi ya magharibi iliyokuwa upande wa wazungu,hizi ideology ziliingizwa mashuleni kuanzia miaka ya 70.
Kipi kilichogundulika Afrika kwa manufaa ya mwafrika Mzungu akakizuia.
Au kipi Mzungu kashindwa kukipata Afrika hadi ampige vita muafrika ndipo akipate hali wao ndo tunawategemea wanunue vitu vyetu.Tusipouza raslimali zetu kwao kwetu ni useless.
Nani anakula madini, dhahabu,nk.
 
Propaganda tu tujitegemee kwa sera zipi hali tulikuwa tunaenda kucollaps Mungu asingeingilia kati.
Huwezi jitegemea kama unaua sekta binafsi,yaani unaua export then tujitegemee.

export zpi izo zmeuliwa mkuu
 
80% mifukoni mwa watawala, 20% tunajengea madarasa na madaraja.
 
Hahhaah wanaaleta sitori na mawaza ya mwaka 47
 
Hatuna adabu na matumizi ya misaada hiyo, pamoja na mapato ya ndani.
Usipokuwa na nidhamu na matumizi basi ujue unakwama pakubwa. Angalia matumizi ya serikali kwenye posho, ununuzi wa magari nk.
 
Kuna kitu nchi za Africa bado hazijafahamu, tunatakiwa kukimbia mikopo na kujikita kusimama bila ya mikopo au misaada. Wanaofaidika na mikopo ni alietoa mkopo.

Jambo jengine kubwa ambalo tunatakiwa kuepukana nalo ni kuwa supplier wa raw materials. Badala yake tunatakiwa iwe tunasafirisha bidhaa zilizotayari kutumika na sio raw materials. Ukianza kutengeneza bidhaa ajira zitapanda, export itaongezeka n.k ndio tutakuwa tunaendelea.

Niliwahi kumsikia raisi wa Ghana akipinga kuuza coco-beans kwa Swis na badala yake anataka atengeneze chocolate kulikimbia hili. Obviously ameona mbali wamagharibi wanatufanyia mchezo mchafu kwenye hili la kutueka kama raw materials supplier.
 
Misaada haisaidii
Imagine unapewa msaada then unapangiwa ukanunue chanjo ya corona
Hiyo corona imekuja mwaka Jana tu, Lakini mikopo tumekuwa tukikopa tangu Uhuru upatikane mwaka 1961, je mikopo yote tuliyokopeshwa kama nchi tulipangiwa cha kufanya ?
 
Vietnam iko Afrika?
Ungetafakari japo kidogo basi. Ninazungumzia weupe na weusi. Ndiyo vita ilipo.

Kwa taarifa yako misaada waliyopewa Vietnam ni tofauti sana na ya Afrika kuanzia riba hadi masharti.
Kwa mfano, Tz inapewa msaada wa dola 5m. Masaharti ni pamoja na utaajiri baadhi ya wataalam kutoka kwa mtoa msaada, utanunua vifaa vyote kutoka kwake na si nchi nyingine. Sehemu ya fedha inaletwa kwa maelezo ishachotwa kulipa hao watumishi wa nje na mitambo toka kwao. Lakini riba ndo usiseme.

Mwisho wa siku utalipa riba hata hela aliyobaki nayo kulipa wataalam na mitambo, wakati hela hiyo haikugusa Tz ikaongeza mzunguko na hiyo mitambo huisha unapoisha mradi. Unabaki na nini zaidi ya deni? Wakati huohuo mradi si wa kuzalisha fedha bali ni wa matumizi tu.
 
Uko sahihi hakuna mzungu anayezuia teknolojia kugunduliwa Africa kuna mzungu mmoja alisema nasikia mna teknolojia ya kuruka na ungo Kama usafiri wa anga akasema si mfungue Viwanda vya nyungo muuze na muanze safari za kusafirisha abiria kwa njia ya anga mshindane kibiashara na ndege za Wazungu? Teknolojia hiyo Africa tunayo na hakuna mzungu kazuia Sasa mbona hatuitambui commercialize? Tuandike kama wao Fly KLM au fly Swiss air sisi zetu Tuandike fly Ungo the best and fastest flight in the world?
 
Uongo utakuuwa dogo, chanjo tumepewa bure kama ambavyo tunapewa bure kondomu, vyandarua, kujengewe vyoo kwa msaada wa Marekani etc etc by the way unajua maana ya Aids, Grants & loans??
Wewe ndo mwongo. Tunapewa mkopo ili tukanunue chanjo. Hakuna chanjo ya bure. Mlionjeshwa mkanunue hamu a dezo.
 
Ni ngumu mno kuendelea kwa kutumia misaada yenye masharti uzitumiaje bila kusahau riba.
Wazungu wakiona kiongozi hataki misaada wanamtafutia zengwe mf. Gadafi,JPM nk.
Hata waswahili husema mtegemea Cha nduguye hufa maskini.
Umesema kweli tupu. Kuna watu wanjilinganisha na nchi za singapore na vietnam
 
Misaada haisaidii
Imagine unapewa msaada then unapangiwa ukanunue chanjo ya corona
Mb9na
Ni bora serikali hii ya awamu ya 6 ipo wazi.mwendazake alituambia nchi tajiri tena bila aibu tumeingia uchumi wa kati.nchi zilizomo katika uchumiwa kati mwananchi wa kawaida anapata kima cha chini US dollars 3500.sawa na mamilioni xeti.
 
Tatizo fedha nyingi zinazopatikana iwe kwenye makusanyo ya kodi au Misaada na mikopo kutoka nje zinaishia kwenye kuhudumia tabaka dogo la watawala(rulling class)
Hebu fikiria kwenye jimbo au Wilaya moja kuna
1.Mkuu wa Wilaya
2.Mkurugenzi
3.MBUNGE
4.Katibu Tawala
5.Mwenyekiti wa Halmashauri na Madiwani
Hapo hujaenda Serikali kuu,tunatumia fedha nyingi kuhudumia kikundi cha watu wachache kuliko kuhudumia wananchi walipa kodi na tozo wa nchi hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…