Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tuanze kwanza kujenga taasisi imara. Tukishindwa maendeleo tusahau.Ili tuendelee tufanyeje?
We jamaa mweupe sana, unasikia hearsay za mtaani unazileta JF, kwa taarifa yako tu, nchi nyingi za nje ya Africa zimepitia dhoruba na madhila makubwa kuliko nchi yako hii ya Tz na ila zimenyanyuka na ni developed Kea kufanya kazi na elimu , Waafrica kinachowaangusha ni uvivu na kutokufikiriVietnam iko Afrika?
Ungetafakari japo kidogo basi. Ninazungumzia weupe na weusi. Ndiyo vita ilipo.
Kwa taarifa yako misaada waliyopewa Vietnam ni tofauti sana na ya Afrika kuanzia riba hadi masharti.
Kwa mfano, Tz inapewa msaada wa dola 5m. Masaharti ni pamoja na utaajiri baadhi ya wataalam kutoka kwa mtoa msaada, utanunua vifaa vyote kutoka kwake na si nchi nyingine. Sehemu ya fedha inaletwa kwa maelezo ishachotwa kulipa hao watumishi wa nje na mitambo toka kwao. Lakini riba ndo usiseme.
Mwisho wa siku utalipa riba hata hela aliyobaki nayo kulipa wataalam na mitambo, wakati hela hiyo haikugusa Tz ikaongeza mzunguko na hiyo mitambo huisha unapoisha mradi. Unabaki na nini zaidi ya deni? Wakati huohuo mradi si wa kuzalisha fedha bali ni wa matumizi tu.
Basi katika mfano niliyotoa, ni Ujerumani baada ya uharibifu wa vita kuu ya pili. Kama unaijua, hongera! Hapo upigamizi ni kuhusu nini? Lete hoja!Mkuu, usifikiri hilo la "Development Assistance" ni jipya na kwamba hata sisi wengine hatulijui. Tunalijua sana, ila hatukubaliani na wewe juu ya misaada hiyo kuleta maendeleo ndani ya nchi hizo unazotutolea kama mfano.
Hakuna hata moja katika aya hizo tatu ulizoandika hapo.Sekta ya kilimo tuliyoitilia mkazo tangu tumepata uhuru ilidorora kwa sababu nyingi tuu ambazo ziko nje ya uwezo wa serikali. Kwa mfano bei za mkonge ziliporomoka kwenye soko la dunia walipogundua katani feki. Kahawa tulikuwa ni moja ya wazalishaji wakubwa siku hizi mpaka China inalima kahawa tena inazalisha kahawa kuliko sisi. Pamba nayo ni vile vile. Korosho kidogo ina afadhali sasa. Labda serikali iwekeze sana kwenye kilimo cha korosho tuone tutafikia wapi.
Kwenye swala la elimu nakubaliana na wewe ila hata kama tungeboresha elimu, ajira ziko wapi? Vijana wetu hata wakienda kusoma nje ya nchi wakirudi wataajiriwa na nani? Wengi wanabakia kuhangaika na maisha bila kujua maisha yao yakoje huko mbele. Wanabakia kufanya kazi ambazo wangeweza kuzifanya bila ya familia zako kutumia au kukopa hela nyingi za kuwasomesha. Na hata serikali ingesema makampuni ya nje yote yanayowekeza hapa lazima yajiiri Watanzania tuu, bado kutakuwa na tatizo la ajira.
Halafu nchi za Afrika kuzilinganisha na nchi za Malaysia na Vietnam siyo sawa. Kihistoria hizo nchi hazikuongozwa kikabila kama nchi zetu. Sisi mfano wetu ni nchi kama Afghanistan au nchi kama Iraq. Kihistoria watu wa hizo nchi walikuwa wanaongozwa kikabila mpaka pale zilipotawaliwa na wakoloni. Kwa Afghanistan, Marekani imetumia zaidi ya dola trilioni moja, wamekaa miaka 20 na bado wameshindwa kuleta maendeleo kwenye nchi ya watu milioni 38 tuu. Maendeleo yameishia Kabul, sehemu zingine bado masikini.
Ujerumani ni nchi iliyokuwa imeendelea hata kuizidi Marekani kabla ya vita. Hali ilikuwa ni hivyohivyo kwa Japan.Basi katika mfano niliyotoa, ni Ujerumani baada ya uharibifu wa vita kuu ya pili. Kama unaijua, hongera! Hapo upigamizi ni kuhusu nini? Lete hoja!
Asante kwa jinbu lako, angalau mara moja moja kupata majadiliano ya maana!Ujerumani ni nchi iliyokuwa imeendelea hata kuizidi Marekani kabla ya vita. Hali ilikuwa ni hivyohivyo kwa Japan.
Hii ina maana, uharibifu ulioletwa na vita na kuharibu miundombinu na sekta mbalimbali za uchumi, ilikuwa ni kazi tu ya kuirejesha na kuweka mingine.
Hiyo misaada ya "Marshall" unayoizungumzia, ilikuwa ni nyenzo tu ya kurudishia sehemu zilizoharibika na kuanzisha viwanda vilivyoharibiwa.Hawa watu tayari walikuwa wameendelea, siyo misaada iliyowaletea maendeleo.
Na sisi kama tuna dhamira ya kweli ya kupata maendeleo, ni lazima tujizatiti kuleta maendeleo hayo. Hii misaada kamwe haitaweza hata siku moja kutuletea maendeleo. Itatusaidia tu kama nyenzo ya kuyapata maendeleo hayo kwa bdii zetu wenyewe.
Juzi tumepata msaada (pesa ya bure) toka Ujerumani,; sijui bilioni ngapi zile. Na hii haikuwa mara ya kwanza benki hiyo kutoa msaada kama huo kwetu. Yalitolewa maelezo mareeeefu kuhusu malengo ya msaada huo, utakapotumika kiasi kwamba unasoma hadi unakaribia kupata usingizi!
Hawa watu wanajua fika, wananchi wetu wengi ni wakulima, tena wa kilimo hiki cha vieka vitano. Kila mwaka wanalia gharama za kununulia mbolea, mbegu bora hawapati, na mahitaji mengine ya kuwawezesha hivi viekari vyao vitano angalau vizalishe mazao ya kutosha. Hawa watoa misaada wanaijua vizuri sana hali hii duni inayowakabili wakulima wetu. Uliwahi kusikia hata mwaka mmoja akatokea mtoa msaada unawalenga wakulima hawa, wapate mbolea na mahitaji mengine ili kilimo chao kiwe cha tija?
Ni muhimu niseme yafuatayo nisije nikaeleweka vibaya:Asante kwa jinbu lako, angalau mara moja moja kupata majadiliano ya maana!
Ndiyo nimesikia mara nyingi kuna miradi ya kulenga wakulima hasa.
Naona kuna sentensi moja muhimu kwako "Hawa watu tayari walikuwa wameendelea", yaani nakubali watu (the human factor) ni msingi wa maendeleo.
Ukiacha mfano wa nchi zilizoharibika baada ya vita kuu, tunaweza kuangalia pia tofauti ya maendeleo baina Asia na Afrika.
Maana mnamo 1950 mara nyingi uwezo wa kiuchumi (kwa vipimo vilivyopatikana) ulikuwa juu zaidi Afrika.
Maana Asia mara nyingi umaskininulikuwa mkali zaidi.
Leo ni tofauti. Machoni pako kwa nini?
Lile gari alilojisifia Polepole Vile ni la aina gani?Niliuliza hili swali kupata maoni, sio hapa tu ni kwenye majukwaa mbalimbali, Asante kwa wote waliotoa maoni yao.
Lakini kwa ufupi misaada na Mikopo kihistoria vilianza miaka ya 1945 na ilikuwa baada ya vita kuu ya pili ya dunia kwa malengo mawili;
i) Kujenga miundombinu iliyoharibiwa wakati wa vita na jukumu hili ilipewa Benki ya Dunia.
(ii) Na lengo la pili lilikuwa ni kuharakisha maendeleo ikiwemo biashara na kudhibiti masuala yote yahusuyo Fedha Duniani, jukumu hili likawa ni la Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Shirika la Biashara Duniani.
Lakini kwa pamoja mashirika haya waliyaweka pia kwaajili ya kudhibiti ama kuzuia kutokea tena kwa mdororo wa uchumi (Great Economic Depression) uliowahi kutokea miaka ya 1930's (Hawa watu wana akili [emoji4], kumbuka Kati ya wadau 700 waliokuwa wanajadili haya, hakuna mdau hata mmoja aliyetoka Afrika kwa ujumla).
Mwaka 1946 na 1947 nchi za Ulaya zilichukua mikopo na misaada kutoka kwenye mashirika haya. Nchi kama Ufaransa, Denmark, Netherlands na Luxembourg waliweza kufanikisha kuunda upya nchi zao na kufuta uharibifu wote uliosababishwa na vita, pamoja na kujenga uchumi wao. Kwa kiasi kikubwa taasisi hizi za Kimataifa zilimudu kudhibiti na kuchochea Uchumi wa Dunia.
Sasa ni nini kilizikuta nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ambapo nchi hizi zinaonekana kuwa na ugonjwa sugu wa Umaskini usiosikia dawa licha ya kupewa mikopo na misaada ya matrilioni ya Fedha? Tutaona Part (ii)
View attachment 1929403
Hivi kwani bado tunapokea misaada kutoka kwa mabeberu?
Si tulishakuwaga uchumi wa kati na matajiri a.k a dona kantriii.
Umenena vyema mkuuMisaada ina dumaza akili na ubunifu maana wanakupa msaada uku wameishakupa masharti na maelekezo ya vipi uutumie(hawataki wakupe msaada alafu wakuache utumie akili na ubunifu wako ni jinsi gani utumie huo msaada ili ujikomboe)
Wizi, rushwa na ubinafsi: hii nayo inachangia tusiendelee pamaoja na kupatiwa hio misaada maana mingi haifikii walengwa kama ilivyo pangwa. Pia waafrika wengi hatuna ushirikiano mzuri kati ya nchi na nchi, viongozi kwa viongozi na hii inawafanya wajanja watutumie kama fursa kupitia misaada yao.
Kukosekana ubunifu, akili na usimamizi wa rasilimali tulizonazo. Kama vya ndani tulivyopewa bure na Mungu tunashindwa kuvisimamia hivi vinavyotoka nje tutaweza kweli!?
Watawaka hata mjadala wa kitaifa wanauogopaTungekuwa ni watu makini (tuliomo JF) huu ungekuwa ni mjadala mahsusi, tena wenye ushahidi wa tarakimu kuonyesha matumizi makubwa kwa watumishi hawa.
Tungedadavua na faida za kuwa nao watu hao wote sehemu hizo walipo kuonyesha umuhimu wao.
Lakini muda wa kufanya hivyo hatuna, na badala yake tunapapasa tu na kwenda zetu.
socialism imeharibu sana watu akili, si chama chenu ndo kinakoleza moto wa misaada, magufuli alivoamua tuanze kujitegemea mkamuona diktetea kwa kifupi nyie mnatakiwa wote mumfuate mbowe ukonga ni janga kwa hii dunia
Bora hata Magu alivyokufa kwasababu
1. Alikuwa anazidi kukopa pesa hasa kwa wachina. Mchina ana roho mbaya sana. Amechukua bandari ya Sri Lanka miaka 100 baada ya kushindwa kulipa mkopo
2. Alifuta ajira Kuna sekta km Ualimu na madaktari walikuwa wanaajiriwa kila mwaka baada ya kuingia yeye tu, ajira akafuta
3. Alikuwa anatengeneza kundi la viongozi wasiofuata sheria na mgawanyo wa majukumu. Kina makonda, Sambaya n.k kiongozi anatoka ofisini anaenda kuchapa wanafunzi. Km anapenda kuchapa wanafunzi apangiwe shule ya kufundisha
4. Kuwepo kwa watu wasiojulikana. Ukikosoa serikali au ukazinguana na kiongozi wanakupiga risasi au wanakuteka. Watu wengi sana wamepotea.
5. Kubambikiwa kesi, mfano hai Rugamalira.
6. Hakuna posho, upandishwaji wa vyeo na hakuna nyongeza za mshahara kwa wafanyakazi wa umma
Kuna vifo ambavyo huwa ni furaha kwa wengine. Magufuli alitimiza hilo
1) National dept ya marekani mpaka tunapoongea saahv ni kiasi gan? uyo anaekupa ushauri usikope kwa mchina hajakopa kwake?
2) Mpaka magufuli anapoteza uhai hakuna kipindi watu hawajaajiriwa, kama ulitimuliwa hilo ni lako!
3) Nitajie sehem moja magufuli hakufuata sheria (ambayo ilikua na ulazima wa kufuatwa): na toka izo sheria zmewekwa mpaka leo zilipotufikisha nadhan hapahitaji maelezo zaidi
4) hata saaahv bado wapo, "Kosoa serikali kwa staha na utoe ushauri unaoeleweka"
5) Hilo alilifanya na ilikua kosa kubwa
6) sasa kupandishwa cheo ni kanuni?
Time isnt fixed, time is an illusion, somewhere in time your already dead, lets say someone living in year 2100 right now anajua umeshakufa na kufukiwa muda mrefu sana.
Kinachokupa kiburi ni muda unaoishi saaahv, you feel like you have a long time to live but somewhere ahead your already dead, and so what differentiates you and death is only TIME:
- someone living in 2019 right now anamuona magu akiwa hai and likewise to everyone else