Wakuu zangu leo nimeingia tena mtamboni baada ya muda kwa sababu mada hii ina uzito mkubwa sana ktk kuelewa tulipotoka, tulipofika na tunaenda wapi.
Kwanza kabisa nakubaliana na wenzangu ktk hoja zao isipokuwa nitaongezea hali halisi iliyopo ndani ya UMOJA huu. Kifupi ni kwamba nchi zetu ziliungana kwa makubaliano kama ya kindoa, japo kila nchi ilikuwa na sababu zake ktk kujiunga na ukweli utabakia kwamba kutokana na hizo sababu binafsi ndizo zilizovunja Umoja wa kwanza mwaka 1977 na utaendelea kuvunja UMOJA huu..
Swala la jumuiya hii ya EAC ni sawa na swala la ndoa ambapo hutegemea watu wawili kuungana na kuwa kitu kimoja yaani mke na mume lakini inapotokea kwamba mmoja wao ana sababu zake nje ya lengo haswa la ndoa, basi ndoa hiyo haina maana na wala haiwezi kudumu japo watu watasukumiana lawama.
Kwa mfano ukioa mke ambaye hakupendi isipokuwa amekubali kuolewa kwa sababu ya Utajiri wako, basi ujue kutakuwepo na mume mwingine nje alopendwa, ama fedha zikiisha utaachwa na pengine atachota kiasi alichokitaka kisha utaachwa kwenye mataa maana hakuitaka ndoa kwa imani halisia.
Mwaka 1975 viongozi wa Jumuiya walikutana Kampala na kuweka makubaliano ambayo kwa njia moja ama nyingine kuweka uuwiano baina ya mataifa haya matatu ili kila mshirika apate kunufaika na jumuiya hiyo lakini baada ya makubaliano hayo tulishuhudia Jumuiya ikianza kukumbwa na migogoro...Pengine ndio asili yetu kuficha dhamira zetu maana ndoa nyingi siku hizi zimefunikwa na dhamira hasi toka pande zote, Tanganyika na Zanzibar yaleyale, na hata Chadema walipoungana na CUF hawakuwa na lengo moja (common goal) isipokuwa kila mmoja alikuwa kalenga kujinufaisha... Huu Ubinafsi hautaweza kujenga kitu kamwe.
Sasa narudi ktk ukweli wa haya yalotokea sasa hivi. Nijuavyo mimi swala la ARDHI limekwisha pewa ufumbuzi japo halina idhini ya wananchi. Hili sii tatizo kwa sasa hata kidogo japo ndilo liloikwaza Jumuiya kufikia muafaka kwa muda mrefu huko nyuma. Tanzania tukitaka ndoa hii iwe ya prenuptial agreement kuhusu umiliki wa ardhi maana ndio utajiri wetu ulobakia. Kwa wenzetu haikuleta maana kuunganisha watu lakini kuna mipaka ya umiliki wa ardhi na uhamiaji.
Hivyo japo walikwisha afikiana nina hakika swala la Ardhi na Uhamijaji yataendelea kuwa matatizo makubwa ya Jumuiya hii maana swala mla ardhi tu limepewa maamuzi na viongozi pasipo kuwashirikisha wananchi ktk maamuzi hayo japo Tanzania yenyewe ilijiunga na JUMUIYA hii kama hatua ya kwanza ya kuunda AFRIKA MOJA. Sisi hatukuwa na sababu wala lengo jinginelo zaidi wakati wenzetu walikuwa na malengo ya kiuchumi zaidi sio kuunda Afrika moja, hivyo tunapofika ktk swala la kiuchumi kwa maslahi ya kila nchi na sio EAC moja hapo ndipo mgongano unapoanzia.
Kwa maana hii nasema tunajua kuwa wenzetu hawakujiunga na EAC kama hatua ya kwanza kuunda United States of Africa, ila zaidi ni kuwa na sauti moja yenye nguvu ya kiuchumi, wakati kila mmoja akinufaika na umoja huu kulingana na rasilimali na maliasili zake. Hii ni ndoa ya kinafiki, sawa na kumuoa mwanamke/mme anayetaka kujenga kwao..wanandoa ambao hawataki kuondokana na kwao ili kuanza familia zao mpya utadhani baba na mama zao walikuwa ndugu. Na sii kosa letu ila ni Utamaduni wetu, unapooa ama kuolewa bado wazazi na familia yako wanatangulia mbele ya mume au mke maana ndoa inaweza vunjika kesho lakini ndugu na wazazi watabakia kuwa ndugu na wazazi wako..
Pili, kuna hili swala sisi Tanzania kuingia vita ya Congo, aidha iwe kweli tumefanya hivyo kwa sababu ya mauaji yalokwisha tokea ama tumefanya ivyo kwa msukumo wa nchi za magharibi ambazo mashirika kama Barricks yanamezea mate miradi ya madini toka nchini humo. Kwa nchi kama Rwanda na Uganda hizi zote zimekuwa zikifaidika na madini ya Congo. Rwanda ikifanya export ya dhahabu na Almasi kuliko Kongo wenyewe na Kagame huyu tunayempa sifa kaijenga nchi yake haraka na vizuri kutokana na utajiri wa Kongo. Pia Wanyarwanda wameweza kusambaa na kurithi ardhi eneo ya Kongo hivyo kuondoa tatizo la ardhi ambalo ndilo hasa sababu ya vita ya kwanza na wahutu.
Hivyo kwa nchi kama Uganda na Rwanda wao wanatushangaa sisi kama wanajumuiya imekuwaje leo tumeingia vita dhidi ya mwanajumuiya mwingine kwa kuungana na jumuiya nyingine ya SADC dhidi ya EAC... tumesimama wapi haswa? - ndivyo wanavyojiuliza! Na kibaya zaidi baada ya marumbano ya kihuni baina ya Kagame na JK, sisi tulichukua uamuzi wa kuwafukuza wakimbizi wa Rwanda tukiwaita wahamiaji haramu.. Je huu muungano wetu wa EAC ulikuwa na lengo gani hasa ikiwa mwanajumuiya Mnyarwanda leo ni mhamiaji haramu japo hahitaji visa wala kibali cha uhamiaji kulingana na malengo ya EAC acha mbali kuwa ni mikimbizi alopata sharia kuihsi nchini kama mkimbizi.
Na toka lini mkimbizi alojipa nchi Fulani akarudishwa makwao kwa sababu tu vita imeisha? tunahakika gani ya usalama wao, na kusema kweli binafsi yangu ndio mara ya kwanza kuona Mkimbizi alokubaliwa Ukimbizi kisheria, kesho anaondolewa na kurudishwa makwao ati vita imeisha au kutokana na mkwaruzano wa marais wake. haya yote ni maswali magumu sana kuyajibu japo sisi tunazo sababu,nia uwezo wa kufanya hivyo.
Kisha ajabu leo unakuta viongozi wetu wanataka kujua sababu kwa nini sisi tumetengwa?.. yaani mwanamke/mume alotembea nje ya ndoa, ukimnyima mchezo anaweza kweli kuuliza kwa nini hapewi?...anyway, pengine mimi nafikirikinyume sana na ndio maana huwa sieleweki kwa sababu tu hutazama pande mbili za sarafu with open minded.
Mwisho, wangu namalizia tu kwa kusema. haitakuwa kosa kubwa sisi tukirudi nyuma na kutazama kwa nini Jumuiya ya kwanza ilivunjika mwaka 1977 na kwa nini makubaliano ya Kampala yalikuwa chachu ya kuvunjika Muungano huo na hata kuleta uhasama mkubwa baina ya Tanzania na Uganda, Kenya na Uganda na kadhalika ili tusishangae tena haya ya Kagame na Museveni tulowaweka madarakani sisi wenyewe.