asome yeye akamueleze mtoto sasa yeye anataka kufundishwa kila kitu mtandaoni bwana, mtoto kukuuliza maana yake ana interest sasa akazame kwenye vitabu aelewe amueleze mtoto.
any way for your child's sake nitamueleza maana ya uplift force
chukua karatasi ngumu kama jarada hivi alafu ishikilie mkononi na karatasi hilo likiwa limesimama wima, geuza kimbiza mkono wako kwa nguvu bila shaka utasikia kwenye mkono kuna nguvu ya upepo inasukuma jarada opposite na uelekeo wa mkono wako. hiyo ni back ward force.
sasa karatasi yako ukiishika ikiwa imelalia mbele kwa sana, yaani upande uliotangulia mbele umeinuka juu na ulio nyuma umeinama kwa chini ukikimbiza mkono wako, hapa utagundua karatasi inaenda inaunika juu. nguvu hii ya kuinuka juu inaenda inabadilika kulingana na ulalo kwa maana upepo unaweka nguvu mmbili moja inasukuma karatasi kwa nyuma na nyingine inasukuma karatasi jii.
hii inayosukuma karatasi juu ndiyo inaitwa up (juu) lift
lakini pia ukiongeza kasi ya mkono nguvu nguvu inayosukuma karatasi kwa maana ya up or back ward zote zinaongezeka.
sasa katika ndege wanabalansi nguvu hii ya kuinua juu inayotokea katika mabawa ili kubeba mzigo wa ndege yenyewe na vitu ilivyobeba.
kama mkono wako unavyosukuma karatasi ndivyo injini za ndege zinavyosukuma ndege kwenda mbele. unaweza kuangalia mfano wa rocket zinavyokwenda juu angani na kwa kuangalia kuwa kuna vitu kama vinakuwa vinachomwa ndani na kutoka kwa kasi sasa ile inaipa ndege msukumo wa kwenda mbele kutokea kwenye injini.
wakati huo mabawa yametegeshewa kama tiara mbili kila upande hivyo injini inavyosukuma ndege mbele ile nguvu ya kusukuma juu (up lift ) inayotokea kwenye mabawa inasukuma ndege kuelekea angani.
Mwambie mtoto akikua na kusoma kwa bidii ataelewa sababu. Atakuwa na motisha ya kusoma kwa bidii.