Naombeni mwongozo: kwani ng'ombe anaficha maziwa?
ni ng'ombe mwenye maziwa mengi tu lakini ana tabia ya "kubana" ukiwa unakamua. Sijuwi ni kwanini?!
mwenye uelewa kuhusu hili anisaidie jamani
Mkuu ni kweli kuwa Ng'ombe anaweza kuamua kuficha maziwa hadi pale atakapoona baadhi kama siyo yote, mahitaji yake muhimu amepatiwa
ila kabla ya kumlalamikia anaficha maziwa, inabidi uwe unajua exactly uwezo wake wa kutoa maziwa at maximum ni upi na katika minimum ni upi
Kwanza kabisa sababu namba 1 ambayo inaweza kufanya Ng'ombe akapunguza maziwa ni Maradhi, tukisema Maradhi basi tunamaanisha maradhi yoyote yale, ila angalia zaidi maradhi ya kiwele
Je ana Mimba na kama anayo ina umri gani Hadi muda huu ambao amepunguza utoaji wa maziwa
Baada ya hapo anza kuchunguza kipi kimebadirika hadi atoke kwenye maziwa labda Lita 7 hadi 3
Unaweza kuanza na kucheki mabadiriko ya msosi, kama umebadiri kitu chochote kwenye chakula chake either kwa kuongeza au kupunguza
Angalia milking boost unayotumia hivi sasa ndio ile ile uliyokuwa unatumia kipindi anatoa maziwa mengi au umebadirisha? Angalia mchanganyiko wa chakula chake je umeongeza au kupunguza kipi
Njoo kwenye mkamuaji je anaekamua ndio yule yule au kuna mabadiriko? Ng'ombe pia huzoea mtu anaemkamua ambao hujiskia huru mbele yake, na wakamuaji wengine hawajui kukamua wanamuumiza Ng'ombe
All in all fata taratibu nzuri za ukamuaji, kama kuosha kiwele pamoja na chuchu kwa kutumia maji yamoto, na pia tumia mafuta ya kukamulia na sio unakamulia mafuta ya Kula au mafuta ya kupaka