Kwanini ng'ombe anaficha maziwa wakati wa kukamua?

Kwanini ng'ombe anaficha maziwa wakati wa kukamua?

Maswali ya kitoto yanahitaji majibu ya kitoto. Tukiendekeza watu kutoshirikisha akili zao vyema, matokeo yake tutakuwa na taifa la ajabu kabisa.

Ninapenda ifike wakati, JF pawe ni sehemu ya kuuliza maswali ambayo umeshindwa kuyapata sehemu yoyote ile. Umetafuta Google umekosa, umetafuta mtaani kwako umekosa, sasa ndipo unakuja kuuliza hapa.

Ndugu yangu ninaye kupenda sana Retired, nakuahidi, sitaacha kuwajibu watu wanaouliza maswali ya kijinga ipasavyo.

Naamini umenielewa. Asante.
tatizo linapoanzia ni pale unapotaka kuchangia kwenye kila uzi!

ukiona mada iko nje na uelewa wako, nashauri kaa pembeni ujifunze kutoka kwa wengine..

ujinga sio upumbavu[emoji120]
 
Mtafutie chakula,wakati wa kumkamua mpatie awe anakula ili asahau kubana maziwa
 
Bujibuji Simba Nyamaume Jf ina watu wa aina zote, wenye uelewa na elimu tofauti tofauti.

sio kila mada/swali linaloletwa hapa lazima ulijibu wewe! Nakushangaa unaposema ni swali la kitoto na hujaweza kulijibu!

mtoto akikuuliza 1 × 1 ukamjibu kitoto = 2

umempoteza
 
Nitakupa hatua zifuatazo zinaweza kusaidia.

1: Hakikisha Jambo la kwanza kuwa n'gombe ni MSAFI na Banda ni safi.

2: Hakikisha Sehemu ya kukamulia inakuwa na utulivu mzuriunampa Pumba Ng'ombe kabla ya chochote.

3 : Hakikisha unamuosha kiwele chake kwa maji ya Mato kwa sabuni huku ukimfuta na kitambaa kumkausha.

4: Mpake mafuta kwaajili ya kuanza kukamua.

HAKIKISHA AMEKUZOEA NA HUMSHTUI AU KUWA NA MAKELELE YA AINA YOYOTE.

NB.
N'gombe anaendelea mziki kwa mbali.
Ukimuwekea wimbo mzuri RNB za mbele Celine Dion nk atakuongezea Lita 3.

Kama ulikuwa unakamua Lita 10 kwa kusikiliza mziki lakini ATAKUPA Lita 13-15.
 
[emoji3] sawa mkuu
 
Kama ng'ombe anabana miguu wakati wa kukamuliwa mh je ulishawah mpanda huyu ng'ombe?
Madogo walikuw ja tabia ya kupanda ng'ombe, wakiingia zizini tu ng'ombe wanabana miguu🤨
 
Kama ng'ombe anabana miguu wakati wa kukamuliwa mh je ulishawah mpanda huyu ng'ombe?
Madogo walikuw ja tabia ya kupanda ng'ombe, wakiingia zizini tu ng'ombe wanabana miguu
[emoji276]
 
Naombeni mwongozo: kwani ng'ombe anaficha maziwa?

ni ng'ombe mwenye maziwa mengi tu lakini ana tabia ya "kubana" ukiwa unakamua. Sijuwi ni kwanini?!

mwenye uelewa kuhusu hili anisaidie jamani
Uko sahihi hasa kwa ngómbe wakienyeji akiamua hataki kukamliwa utaambulia kikombe cha chai. Ila ukiamwachia ndama anyonye unaona maziwa mpaka yanadondoka chini. Tumia ndama kumconvice, achia ndama anyonye kidoge alafu ukamue, ukiona ameanza kuficha unaachia tena ndama. Pia tumia vilainishi au maziwa yake yake mwenyewe. Usivute chuchu zake zake pale fanya kama unazibinya binya.
 
asante sana
 
Shukrani sana Anigrain [emoji120][emoji120]

kuna jirani yangu ameniambia kwamba sijuwi kukamua! Je ni utaalamu gani labda unatumika kwenye ukamuaji licha kutumia mafuta ya kukamulia??
Duhhh mkuu kumuelekeza mtu kukamua kwa kutumia keyboard ni ngumu sana au Kiswahili chepesi ni haiwezekani

Inabidi umtumie mtu anaejua kukamua vizuri akuelekeze ukiwa unaona na unatenda ili uweze kumaster Kwa haraka

Speed katika ukamuaji inahitajika sana, mtu ukiwa hujui kukamua au huna uzoefu Ng'ombe huboreka na kuamua kuzuia maziwa umwache

Jitajihidi sana ujifunze haraka iwezekanavyo maana muda sio mrefu utaanza kuuguza magonjwa ya kiwele, Ng'ombe akiwa anabakiza maziwa anapata ugonjwa wa Mastitis

Na kama waga mnamkamua bila chakula basi unaweza kuanza kuwa unawawekea pumba kidogo wakati wa kukamuliwa, ili waone kutoa maziwa ni wajibu wao

Hizo pumba unapaswa uchanganye na baadhi ya virutubisho ili kuongeza kiasi cha maziwa lakini pia kuongeza ubora wa maziwa, ili maziwa yawe na uwiano mzuri katika uzito,utamu na mafuta

utaweka madini ya calcium, phosphorus na vitamin D au kifupi wanaita (DCP) pia vingine utachanganya mashudu (Alizeti/pamba) utachanganya na milking boost, utachanganya na chumvi kidogo ya kula, utachanganya na molasses

All the best
 
Duhhh mkuu kumuelekeza mtu kukamua kwa kutumia keyboard ni ngumu sana au Kiswahili chepesi ni haiwezekani

Inabidi umtumie mtu anaejua kukamua vizuri akuelekeze ukiwa unaona na unatenda ili uweze kumaster Kwa haraka

Speed katika ukamuaji inahitajika sana, mtu ukiwa hujui kukamua au huna uzoefu Ng'ombe huboreka na kuamua kuzuia maziwa umwache

Jitajihidi sana ujifunze haraka iwezekanavyo maana muda sio mrefu utaanza kuuguza magonjwa ya kiwele, Ng'ombe akiwa anabakiza maziwa anapata ugonjwa wa Mastitis

Na kama waga mnamkamua bila chakula basi unaweza kuanza kuwa unawawekea pumba kidogo wakati wa kukamuliwa, ili waone kutoa maziwa ni wajibu wao

Hizo pumba unapaswa uchanganye na baadhi ya virutubisho ili kuongeza kiasi cha maziwa lakini pia kuongeza ubora wa maziwa, ili maziwa yawe na uwiano mzuri katika uzito,utamu na mafuta

utaweka madini ya calcium, phosphorus na vitamin D au kifupi wanaita (DCP) pia vingine
[emoji120][emoji120]
 
yawezekana ukamuaji wako sio rafiki ndio maana hvyo kijana mwngne anakamua mengi jifunze kwake.
au unakamua kama unanyetuka??
 
Wakati unamkamua ngombe ukishaanza hilo zoezi jihidi uende kwa kasi sio unakamua kisha unapumzika

Pili kuna ngombe wengine bila kumuona ndama wake hatoi maziwa kwa hiyo mfunge ndama mbele yake.

Tatu kuna ngombe wengine ndama wake lazima anyonye kwanza kidogo kisha unamtoa ndio uanze kumkamua
 
Kila kiti lazima.kiandaliwe kipetiweeee afu ndo awe tiyari
 
Naombeni mwongozo: kwani ng'ombe anaficha maziwa?

ni ng'ombe mwenye maziwa mengi tu lakini ana tabia ya "kubana" ukiwa unakamua. Sijuwi ni kwanini?!

mwenye uelewa kuhusu hili anisaidie jamani
Subiri na mimi nitie neno hapa
Ng'ombe wengi huficha maziwa kutokana na mazoea ulowazoesha

#kma ulikua unampa pumba na virutubisho vyengine hlf ukaacha kumpa au ukapunguza na yy atayaficha tu

#kma ni kipindi cha masika na majani yapo ya kutosha na ww bdo unampa majani makavu ataficha tu maziwa

#kikawaida Ndama atangulie kunyonya kbla kuanza kukamua ukifanya kinyume lazima ataficha

#Mpe pumba kabla kumkamua kiasi cha dakika 5 ivi hlf utaona matokeo yke

#Sio kila mtu akamue ng'ombe tafuta mtu maalumu wa kukamua ng'ombe ili wanyama hao wamzoee

Chunguza vizuri katika dalili nilizozitaja hpo juu huenda jpo moja ulimfanyia uyo ng'ombe
 
Naombeni mwongozo: kwani ng'ombe anaficha maziwa?

ni ng'ombe mwenye maziwa mengi tu lakini ana tabia ya "kubana" ukiwa unakamua. Sijuwi ni kwanini?!

mwenye uelewa kuhusu hili anisaidie jamani
maziwa kwa asili ni kwa ajili ya ndama na si binadamu au matumizi mengine yoyote.
 
maji vuguvugu natumia. Iko hivi: mwanzo maziwa yanatoka vizuri lakini baada ya dk 2 yanakata! akikamua dogo anaewalisha anapata mara tatu ya yale ninayokamua mimi[emoji848]
Labda hujui kukamua. Unamuuza ng'ombe wakati wa kukamua. Au huwa unampiga au kum.treat vibaya hivyo akikuona anapatwa na kiwewe. Kwa kifupi tatizo ni wewe. Ng'ombe wakati wa kukamuliwa anatakiwa awe relaxed kabisa. Apewe chakula anachopenda sana, halafu ni vizuri akakamuliwa na mtu aliyemzoea. Siyo wewe unaenda mara moja moja kumhudumia halafu unakimbilia kukamua.
 
Back
Top Bottom