Kwanini ng'ombe anaficha maziwa wakati wa kukamua?

Kwanini ng'ombe anaficha maziwa wakati wa kukamua?

Naombeni mwongozo: kwani ng'ombe anaficha maziwa?

ni ng'ombe mwenye maziwa mengi tu lakini ana tabia ya "kubana" ukiwa unakamua. Sijuwi ni kwanini?!

mwenye uelewa kuhusu hili anisaidie jamani

Ni tabia ya mnyama anampenda mwanae.
Jitahidi ule muda wa kukamua weka na mwanae pale kwenye chuchu mama amwone nae alafu kamua utayapata yote
 
Unatakiwa kuyatomasa, hasa chuchu zake, pia ngo'mbe anatakiwa wakati unamkamua kuna yale mafuta flani siyakumbuki jina, unampatia Pumba zenye makapi ya molasses, ama lile jiwe la chumvi, hapo lazma arembue na akuachie ukamue mpaka kamasi. Lakini kabla ya yote unamwita ndama anayavuta kidogo kisha unakatimulia mbali..umenikumbusha mbali sana Mzee nilikuwa ng'ombe mmoja nilikuwa nikimwita kibaka enzi hizo
 
Hata ungekuwa wewe ungefurahi mtu aje akushishike maziwa yako afu akuache bila kukunyandua?
 
Wakati unamkamua ngombe ukishaanza hilo zoezi jihidi uende kwa kasi sio unakamua kisha unapumzika

Pili kuna ngombe wengine bila kumuona ndama wake hatoi maziwa kwa hiyo mfunge ndama mbele yake.

Tatu kuna ngombe wengine ndama wake lazima anyonye kwanza kidogo kisha unamtoa ndio uanze kumkamua
asante sana
 
Subiri na mimi nitie neno hapa
Ng'ombe wengi huficha maziwa kutokana na mazoea ulowazoesha

#kma ulikua unampa pumba na virutubisho vyengine hlf ukaacha kumpa au ukapunguza na yy atayaficha tu

#kma ni kipindi cha masika na majani yapo ya kutosha na ww bdo unampa majani makavu ataficha tu maziwa

#kikawaida Ndama atangulie kunyonya kbla kuanza kukamua ukifanya kinyume lazima ataficha

#Mpe pumba kabla kumkamua kiasi cha dakika 5 ivi hlf utaona matokeo yke

#Sio kila mtu akamue ng'ombe tafuta mtu maalumu wa kukamua ng'ombe ili wanyama hao wamzoee

Chunguza vizuri katika dalili nilizozitaja hpo juu huenda jpo moja ulimfanyia uyo ng'ombe
[emoji120]
 
Naombeni mwongozo: kwani ng'ombe anaficha maziwa?

ni ng'ombe mwenye maziwa mengi tu lakini ana tabia ya "kubana" ukiwa unakamua. Sijuwi ni kwanini?!

mwenye uelewa kuhusu hili anisaidie jamani
wanawake wanajua hilo inaitwa kufinya kwa ndani anabana zile glands kwa ajili ya matumizi ya mwanaye
 
Unatakiwa kuyatomasa, hasa chuchu zake, pia ngo'mbe anatakiwa wakati unamkamua kuna yale mafuta flani siyakumbuki jina, unampatia Pumba zenye makapi ya molasses, ama lile jiwe la chumvi, hapo lazma arembue na akuachie ukamue mpaka kamasi. Lakini kabla ya yote unamwita ndama anayavuta kidogo kisha unakatimulia mbali..umenikumbusha mbali sana Mzee nilikuwa ng'ombe mmoja nilikuwa nikimwita kibaka enzi hizo
[emoji3][emoji1666]
 
Naombeni mwongozo: kwani ng'ombe anaficha maziwa?

ni ng'ombe mwenye maziwa mengi tu lakini ana tabia ya "kubana" ukiwa unakamua. Sijuwi ni kwanini?!

mwenye uelewa kuhusu hili anisaidie jamani
Hivi ikitumika mashine ya kukamulia bado ataweza kuyabana?
 
[emoji3] sawa mkuu
Usidhanie utani. Ngombe wanapenda miziki ya taratibu na huwafanya kurelax na kutoa maziwa mengi. Hii tafiti ilifanyika huko Europe niliona DW wanaonyesha.

Walikuwa wanawawekea nyimbo za Slow Jazz, Soul, na zile nyimbo za opera. Yaani ngombe anatulia anasikiliza hizo ngoma anarelax kabisa. Wanamuwekea na sehemu ya kujikuna mashine imekaa kama brush, na kuna sehemu imekaa kama turubai imetandikwa sakafuni kwa chini ina mashine ya massage.

Hii sio mzaa ni kweli. Ingia YouTube utaona.
 
Back
Top Bottom