Kwanini ng'ombe anaficha maziwa wakati wa kukamua?

Naombeni mwongozo: kwani ng'ombe anaficha maziwa?

ni ng'ombe mwenye maziwa mengi tu lakini ana tabia ya "kubana" ukiwa unakamua. Sijuwi ni kwanini?!

mwenye uelewa kuhusu hili anisaidie jamani

Ni tabia ya mnyama anampenda mwanae.
Jitahidi ule muda wa kukamua weka na mwanae pale kwenye chuchu mama amwone nae alafu kamua utayapata yote
 
Unatakiwa kuyatomasa, hasa chuchu zake, pia ngo'mbe anatakiwa wakati unamkamua kuna yale mafuta flani siyakumbuki jina, unampatia Pumba zenye makapi ya molasses, ama lile jiwe la chumvi, hapo lazma arembue na akuachie ukamue mpaka kamasi. Lakini kabla ya yote unamwita ndama anayavuta kidogo kisha unakatimulia mbali..umenikumbusha mbali sana Mzee nilikuwa ng'ombe mmoja nilikuwa nikimwita kibaka enzi hizo
 
Hata ungekuwa wewe ungefurahi mtu aje akushishike maziwa yako afu akuache bila kukunyandua?
 
asante sana
 
[emoji120]
 
Naombeni mwongozo: kwani ng'ombe anaficha maziwa?

ni ng'ombe mwenye maziwa mengi tu lakini ana tabia ya "kubana" ukiwa unakamua. Sijuwi ni kwanini?!

mwenye uelewa kuhusu hili anisaidie jamani
wanawake wanajua hilo inaitwa kufinya kwa ndani anabana zile glands kwa ajili ya matumizi ya mwanaye
 
[emoji3][emoji1666]
 
Naombeni mwongozo: kwani ng'ombe anaficha maziwa?

ni ng'ombe mwenye maziwa mengi tu lakini ana tabia ya "kubana" ukiwa unakamua. Sijuwi ni kwanini?!

mwenye uelewa kuhusu hili anisaidie jamani
Hivi ikitumika mashine ya kukamulia bado ataweza kuyabana?
 
[emoji3] sawa mkuu
Usidhanie utani. Ngombe wanapenda miziki ya taratibu na huwafanya kurelax na kutoa maziwa mengi. Hii tafiti ilifanyika huko Europe niliona DW wanaonyesha.

Walikuwa wanawawekea nyimbo za Slow Jazz, Soul, na zile nyimbo za opera. Yaani ngombe anatulia anasikiliza hizo ngoma anarelax kabisa. Wanamuwekea na sehemu ya kujikuna mashine imekaa kama brush, na kuna sehemu imekaa kama turubai imetandikwa sakafuni kwa chini ina mashine ya massage.

Hii sio mzaa ni kweli. Ingia YouTube utaona.
 
maji vuguvugu natumia. Iko hivi: mwanzo maziwa yanatoka vizuri lakini baada ya dk 2 yanakata! akikamua dogo anaewalisha anapata mara tatu ya yale ninayokamua mimi[emoji848]
Uzoefu wa kukamua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…