Sababu kubwa kabisa ni "civilization". Kuna sababu nyingi tu za jamii fulani kuwa civilized kuliko nyingine. Ni bahati tu kuwa mfumo wa madrasa unaotumiwa na waislamu pia hufunza civilization lakini mfumo wa kikristo au wa kipagani haufundishi kabisa civilization. Unaweza kuuliza mbona nchi za kizungu zina ukristo mwingi lakini civilization ipo juu. Jawabu ni kama nilivyosema hapo juu. Kuna sababu nyingi za jamii fulani kuwa civilized, na kwa nchi za magharibi civilization yao haikusababishwa na Dini (ukristo); yumkini imesababishwa na kutembea kulikofanywa na wazungu wenyewe kwa karne hadi karne (na mpaka leo vizazi vinaendeleza mfumo wa kutembea), maendeleo ya sayansi na teknolojia, mfumo rasmi wa maisha pamoja na sheria kali zilizopo.
Mfumo wa elimu ya madrasa uliopokewa pwani umefanya jamii hizo kuwa "wajanja" siku nyingi. Lakini pia mfumo huo umesisitiza sana kwenye kuwaaminisha watu wake juu ya makatazo ya kiimani. Ofcourse, kuna exclusion kadhaa lakini relatively jamii iliyoenda madrasa na kwa mazingatio ni nadra sana kufanya matukio ya kuua kwa sababu ya mapenzi.
Lakini pia jamii hizi zimekuwa katika mifumo ya communal ukiongezwa chachu na mfumo wa vijiji vya ujamaa ambao uliathiri zaidi maeneo ya pwani (ambako waislamu wengi wapo).
Sababu nyingine ni mfumo wa kiutawala uliokuwepo kuanzia ngazi ya familia ambapo vikao vya kiukoo lilikuwa jambo la kawaida. Mfumo huu ulileta nafuu ya kujenga discipline kuwa kabla ya kuchukua maamuzi binafsi, kuna ngazi za sheria hupaswa kufuatwa kwa kumshtaki mkosa katika vikao vya kiukoo. (Rejea mfumo wa liwali, jumbe na akida katika tawala za kikoloni). Hali hii ilijenga mazoea hapo baadaye kufuata ngazi za sheria katika mfumo wa kiserikali pale mifumo ya kutoa haki ya kifamilia/ kiukoo ilipoyumba. Hali hii imekuwa tofauti kwa mikoa ya pembezoni (mbali na ngazi za kimaamuzi serikalini).
Ujirani wa jamii hizi na Jiji la Dar ulifanya jamii hizi kufika Dar es salam kirahisi na hivyo kupata "exposure" ya jamii fulani iliyostaarabika.
Ubinafsi. Hapa kuna mchango wa elimu ya madrasa kidogo. Hizi jamii hazina ubinafsi kabisaa. No wonder leo unaenda Rufiji au Tanga au Mafya, hutakuwa na mtu hata mmoja anayekujua lakini utakuwa treated kama ndugu yao. Utapewa support zote na taarifa zote muhimu ikiwa pamoja na mke/mume au uongozi. Ni nadra sana hali hiyo kuikuta kwenye jamii nyingine za Bara.
Ucheshi na utani. Jamii hizi zimekuwa na utani mwingi mnoo uliotokana na michezo ya tangu utotoni. Kiukweli, utani huongeza upendo baina ya watu. Sijajua exactly why jamii hizi zinapenda sana utani na michezo ya aina hiyo tofauti na jamii za Bara.
Jiografia...