Kwanini nguruwe hauzwi minadani kama mbuzi, kondoo, ng'ombe na kuku?

Mkuu jeshini kuna siku tumepangiwa kwenda kuhudumia nguruwe, nikapangwa banda linaitwa Muhimbili, kumbe ni wale wagonjwa! Imagine nguruwe mgonjwa... Sisahau hadi leo
 
Nakubali ni nyama pendwa sana hata kwangu pia naikubali sana.

Utofauti wake ni ni hasa asiuzwe mnadani ukisema ni Luxury meat ni hoja nyepesi sana hii
Sababu ni hii: Nguruwe na nyama yake vimepata umaarufu siku za karibuni tu. I mean miaka ya nyuma kwenye 60, 70 na 80, nyama ya nguruwe haikuwa inaliwa kama sasa. Hata mabucha ya nyama ya nguruwe yalikuwa ni machache sana sana na nyama ya nguruwe ilikuwa inauzwa kwa msimu. i.e. mfugaji wa nguruwe (walikuwapo wachache sana) anapotaka kuchinja nguruwe, anatoa habari kwa majirani na watu wa karibu ili wakanunue nyama siku atapochinjwa. Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa nguruwe hauzwi mnadani kwa sababu umaruufu wa nyama yake umeibuka siku hizi tu. Fanya uchunguzi utakuwa hata wazee wa zamani wengi walikuwa hawapendi nyama ya nguruwe. Na zaidi mambo ya ku-roast au kukaanga hayakuwepo kama sasa. Nguruwe wachache waliokuwepo walikuwa wanafungwa na kunenepeshwa ili yapatikane mafuta ya kupikia. Ilikuwa ni kawaida nguruwe anapochichwa watu wanakwenda kununua mafuta yake ili wakayatengeneze kwa kupikia chakula,
 
Nakubali ni nyama pendwa sana hata kwangu pia naikubali sana.

Utofauti wake ni ni hasa asiuzwe mnadani ukisema ni Luxury meat ni hoja nyepesi sana hii
Kama nilivyosema zamani watu wengi walikuwa hawali kitimoto. Na pia enzi hizo kumtoa nguruwe point A mpaka B ilikuwa siyo kazi rahisi kwa sababu huwezi kuwaswaga kama mbuzi. Kipindi hicho magari na vyombo vya usafiri kwa ujumla vilikuwa hapa. Hivyo kuna combination ya sababu
1. Nyama ya nguruwe zamani ilikuwa hailiwi kama sasa hivyo kulikuwa hakuna uhitaji wa nguruwe wengi kwa mara moja.
2. Kuswaga nguruwe mpaka mnadani nayo ni shughuli kwa sababu hawana nidhamu kama mbuzi.
 
Kwa nini Rolls Royce haiuzwi Magomeni na Hapo mlimani city kwa madalali.
 
Sina hakika kama kelele pekee ndo inaweza kuwa chanzo Cha kutompeleka mnadani
Tatizo ndugu zetu wana nongwa sana, watasusa kwenda mnadan kununua hata vitu vingine kisa tu Kuna nguruwe. We c unaona hata kuku tunawapa wachinje, maana ukichinja wewe hawali.

Tunawapenda sana ndugu zetu, Ila wana noma sana.
 
Kwanza nakubaliana na wote walichangia mada

Nafikiri ni kwasababu ya

1)Nguruwe hawafugwi kwa wingi kama ng'ombe na mbuzi,kwahiyo hao soko lao linaishia majumbani tu.

2)Dhamiri.
Ukichanganya nguruwe na wanyama wengine kwenye biashara au sokoni tegemea kukosa wateja wa Imani Fulani na hii yaweza leta mkanganyiko kwenye jamii na hapa nakubaliana na Atacms

Mwisho:ukitoa nguruwe,wanyama karibia wote waliobaki wanauzika kwa watu wa Imani zote..

Nashauri nguruwe wawe na soko lao maalumu
 
Huo mnada ungekuwa ni mbio mbio za kufukuza nguruwe maana hawajawahi tulia sehemu moja. Yaani ukiwa na hamu ya mbio unae sa mnada wa nguruwe mpaka jion umekimbia kilomita za kutosha.
Anaefuatia kwa kukosa utulivu ni mbuzi.
 
nenda minada ya mbulu kule manyara mkuu wa meza yupo kama kawa hii ni kwa viongozi haiwezi kuwa kila sehemu
 
Manyoya yanacover only 1% ya uzito wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…