Kwanini nguruwe hauzwi minadani kama mbuzi, kondoo, ng'ombe na kuku?

Jf saalam.

Wakuu tukitazama tu Kwa jicho la kawaida hata bila kuingiza dini/Imani zetu hapa napata ukakasi sana.

Ni kwanini Nguruwe pamoja na kupendwa sana na watu lakini sijawahi ona kwenye minada ya kawaida nguruwe nae anauzwa kama ilivyozoeleka kuona ng'ombe na punda wakiuzwa kwanini kwakwe ni tofauti?

Tangu nianze kutembelea minada mikubwa nakiri wazi sijawahi ona nguruwe minadani.

Ndio swali ninalo jiuliza ni kwamba hairuhusiwi nguruwe kuuzwa minadani?View attachment 3140160
Kizuri chajiuza, kibaya cha jitembeza.
 
Kule wanafugwa kama kuku, wanafunguliwa asubuhi jioni wanarudi wenyewe zizini. Ukimpenda nguruwe wa mtu mnauziana popote pale
Ni sawa mkuu hii hata Mimi nimewahi ona lakini kuona kabisa mnadani kama mifugo mingine sijawahi muona. Mara zote Huwa nafikri labda Kuna katazo la serikali hata ukiangalia kwenye vibari vya mifugo nguruwe sijawahi muona.
 
Unajua kabisa ndugu zetu katika iman kwao hiyo kitu hua ni mwiko vile vile kwa wasabato pia
Sasa mnada hua ni mjumuiko wa watu wote ukiweka iyo kitu huoni kua utawakosa hao wateja wasio tumia hiyo makitu?
 
Jf saalam.

Wakuu tukitazama tu Kwa jicho la kawaida hata bila kuingiza dini/Imani zetu hapa napata ukakasi sana.

Ni kwanini Nguruwe pamoja na kupendwa sana na watu lakini sijawahi ona kwenye minada ya kawaida nguruwe nae anauzwa kama ilivyozoeleka kuona ng'ombe na punda wakiuzwa kwanini kwakwe ni tofauti?

Tangu nianze kutembelea minada mikubwa nakiri wazi sijawahi ona nguruwe minadani.

Ndio swali ninalo jiuliza ni kwamba hairuhusiwi nguruwe kuuzwa minadani?View attachment 3140160
Hiyo ni Luxurious meat lazima iuzwe kwa heshima.
 
Unajua kabisa ndugu zetu katika iman kwao hiyo kitu hua ni mwiko vile vile kwa wasabato pia
Sasa mnada hua ni mjumuiko wa watu wote ukiweka iyo kitu huoni kua utawakosa hao wateja wasio tumia hiyo makitu?
Mkuu wazo lako/point Yako Haina mashiko. Kwa sababu uliingiza Imani msabato hata Bata tu Hali pia kambale lakini hao wote huuzwa mnadani na masokoni.
 
Back
Top Bottom