Kwanini nguruwe hauzwi minadani kama mbuzi, kondoo, ng'ombe na kuku?

Kwanini nguruwe hauzwi minadani kama mbuzi, kondoo, ng'ombe na kuku?

Uliwahi kuona Ngamia, Farasi, Sungura wakiuzwa mnadani? Vitu hadimu huwezi kuviona vikitembezwa tembezwa
Ukisema farasi nitaanza kushangaa mwenyewe hapahapa maana sijawahi ona mfugaji wa farasi anao hata 50 Kwa pamoja Hapa nchini. Pia sungura walaji wake ni wachache sana mkuu fatilia tu
 
Mkuu mbona naonaga ngamia anasomewa Dua Hadi ana lala mwenyewe na kuchinjwa?


Tena kwenye sikukuu za uislamu utasikia boss kajitoa kuwa atachinja ngamia na anasomewe Dua kwanza ndo anachinjwa Nini maana yake?
Hata mimi nimeona kama wewe ila sijajua wanatumia sheria gani,maana mafundisho yapo wazi kwenye vitabu kuhusu nini cha kula na nini kisiliwe
 
Ni elimu mbovu TULIO NAYO KUHUSU UFUGAJI WA NGURUWE na hii imepelekea serikal kukoswa mapato mengi hasa ya uuzaj holela wakuto kuweka mazingira rafik ya kisoko hasa minada ka wanyama wengine,, MI NASHUKURU PAMOJA NA HILI ILA TUNAPIGA HELA MING SANAAA ss wafugaji wahitaji wana TUTAFUTA WENYEWE soko hali tuumizi vichwa ukilinganisha na wanyama wengine,, nitambue pia uwepo wa machinjio karibu kila mkoa na baadh ya wilaya sasa TUNACHINJA NA WANAKAGULIWA kwa mazingira rafik kabisaaa kidogo dogo TUNABADILIKA HUENDA SIKU ZA USON tutaona minada
 
Huwa naona mara nyingi ni Hivi lakini nakuwa nawaza kwanini mnadani hawapeleki ama Kuna katazo la serikali. Leo ndo nimepata majibu humu
Halafu kwenye biashara ya kitimoto hai, mnunuzi na muuzaji wote wanafahamu ni kilo ngapi za nyama zilizopo hapo japokuwa mnyama bado anatembea i.e. yupo hai kwa kutumia "weigh band." Hakuna kudanganyana kama wafanyavyo wale jamaa almaarufu Galagaja kwenye ng'ombe na mbuzi.
 
Demand yake ipo juu anafuatwa alipo
Inakuwa hivyo kwa sababu takriban 98% ya mwili wake ni Consumable items. i.e. Kila kitu hapo mwilini kwake kinauzwa/kinatumika kuanzia kongoro, kichwa, utumbo, mafuta, n.k. wa hiyo faida ni kubwa. Kinachotupwa labda ni manyoya tuu kwani hakuna ngozi. Ngozi hutolewa na mafuta yake.
 
Jf saalam.

Wakuu tukitazama tu Kwa jicho la kawaida hata bila kuingiza dini/Imani zetu hapa napata ukakasi sana.

Ni kwanini Nguruwe pamoja na kupendwa sana na watu lakini sijawahi ona kwenye minada ya kawaida nguruwe nae anauzwa kama ilivyozoeleka kuona ng'ombe na punda wakiuzwa kwanini kwakwe ni tofauti?

Tangu nianze kutembelea minada mikubwa nakiri wazi sijawahi ona nguruwe minadani.

Ndio swali ninalo jiuliza ni kwamba hairuhusiwi nguruwe kuuzwa minadani?View attachment 3140160
Utashambuliwa na mashehe
 
Sahihi mkuu lakini hapo hapo mnadani ukienda sehem ya nyama choma ukiuliza kitimoto Unapata.

Pia kwenye nanenane wapo nguruwe wengi tu. Hapo ndo napata ukakasi kwanini mnadani tu?
Sasa ikiwa nyama choma ya kitimoto unapata na wanapatikana hadi nanenane, sidhani kama wanahitaji kupatikana hadi mnadani. Wangu maisha ni mafupi na kuna mambo mengi hebu tujadili vipi tunaweza kuwarithisha kizazi kijacho Tanzania yenye matumaini.
 
Jf saalam.

Wakuu tukitazama tu Kwa jicho la kawaida hata bila kuingiza dini/Imani zetu hapa napata ukakasi sana.

Ni kwanini Nguruwe pamoja na kupendwa sana na watu lakini sijawahi ona kwenye minada ya kawaida nguruwe nae anauzwa kama ilivyozoeleka kuona ng'ombe na punda wakiuzwa kwanini kwakwe ni tofauti?

Tangu nianze kutembelea minada mikubwa nakiri wazi sijawahi ona nguruwe minadani.

Ndio swali ninalo jiuliza ni kwamba hairuhusiwi nguruwe kuuzwa minadani?View attachment 3140160
Nenda wilaya ya siha kijiji makiwaru katikat panasoko upande mmoja mnada wa ng'ombe upande wapil kama unaenda hospital ya ngartat mnada wa nguruee tena zipo za kushatooo
 
Back
Top Bottom