Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Kama unawajua vyema, nguruwe ni moja ya wanyama wasafi na wenye akili sana duniani. Sasa kwanini wanasifa ya kuwa wanyama wachafu sana?
Kuna mawili.
1. Nguruwe huwa hawana tezi za kutolea jasho. Wala hawawezi kupunguza joto kwa kutoa ulimi kama mbwa. Hilo linafanya wahitaji mazingira yenye kivuli ili waishi vizuri. Kama wakikosa kivuli basi watajipaka matope ili kijikinga na jua kali. Kama hamna matope hata kinyesi chao watajipaka kuepuka joto. Ni suala la survival. Nguruwe wakifugwa sehemu yenye kivuli kizuri cha miti huwa wanaonyesha usafi wao halisi. Utaona anajisaidia mbali kabisa na anapolala. Mwili wao ukiwa msafi bila matope wala kinyesi.
2. Nguruwe ni kama binadamu. Hata chakula chake ni kama binadamu. Nguruwe hana uwezo wa kula majani kama mbuzi au ng'ombe. Nguruwe wanafanana sana na binadamu. watu wanaokula watu, husema kuwa nyama ya binadamu inanoga kama ya nguruwe. Hata dawa kama Insulin au Pepsin huchukuliwa kutoka kwa nguruwe. Sasa basi chakula chake ni nafaka kama binadamu au makombo. Akikosa, atakula mizoga hata vinyesi. Hata binadamu wakizidiwa hula vinyesi vyao, mizoga, makombo na vitu vingine vichafu. So nguruwe huanza kula vichafu baada ya kukosa msosi wa maana.
Sasa. Wataalamu wanasema kuwa dini zilizoanzia mashariki ya kati(Uyahudi na Uislamu)zinakataza kula nguruwe kwa sababu hizi. Mashariki ya kati kuna joto kali huku hakuna miti ya vivuli. Muda wote nguruwe walikuwa wakijigaragaza kwenye matope na vinyesi. Wale nguruwe wa mijini walikuwa wakigombania chakula na binadamu. Wakaishia kula makombo na mizoga. Mambo haya yalionekana ni uchafu wa kupindukia. Matokeo yake wenye mamlaka wakapiga marufuku ulaji wa Nguruwe. Matokeo yake marufuku hizo zikaingia hadi kwenye dini.
My take.: Nyama ya binadamu inanoga kama ya nguruwe.