Kwanini nguruwe huwa wachafu sana?

Kwanini nguruwe huwa wachafu sana?

Kama unawajua vyema, nguruwe ni moja ya wanyama wasafi na wenye akili sana duniani. Sasa kwanini wanasifa ya kuwa wanyama wachafu sana?

Kuna mawili.
1. Nguruwe huwa hawana tezi za kutolea jasho. Wala hawawezi kupunguza joto kwa kutoa ulimi kama mbwa. Hilo linafanya wahitaji mazingira yenye kivuli ili waishi vizuri. Kama wakikosa kivuli basi watajipaka matope ili kijikinga na jua kali. Kama hamna matope hata kinyesi chao watajipaka kuepuka joto. Ni suala la survival. Nguruwe wakifugwa sehemu yenye kivuli kizuri cha miti huwa wanaonyesha usafi wao halisi. Utaona anajisaidia mbali kabisa na anapolala. Mwili wao ukiwa msafi bila matope wala kinyesi.

2. Nguruwe ni kama binadamu. Hata chakula chake ni kama binadamu. Nguruwe hana uwezo wa kula majani kama mbuzi au ng'ombe. Nguruwe wanafanana sana na binadamu. watu wanaokula watu, husema kuwa nyama ya binadamu inanoga kama ya nguruwe. Hata dawa kama Insulin au Pepsin huchukuliwa kutoka kwa nguruwe. Sasa basi chakula chake ni nafaka kama binadamu au makombo. Akikosa, atakula mizoga hata vinyesi. Hata binadamu wakizidiwa hula vinyesi vyao, mizoga, makombo na vitu vingine vichafu. So nguruwe huanza kula vichafu baada ya kukosa msosi wa maana.

Sasa. Wataalamu wanasema kuwa dini zilizoanzia mashariki ya kati(Uyahudi na Uislamu)zinakataza kula nguruwe kwa sababu hizi. Mashariki ya kati kuna joto kali huku hakuna miti ya vivuli. Muda wote nguruwe walikuwa wakijigaragaza kwenye matope na vinyesi. Wale nguruwe wa mijini walikuwa wakigombania chakula na binadamu. Wakaishia kula makombo na mizoga. Mambo haya yalionekana ni uchafu wa kupindukia. Matokeo yake wenye mamlaka wakapiga marufuku ulaji wa Nguruwe. Matokeo yake marufuku hizo zikaingia hadi kwenye dini.

My take.: Nyama ya binadamu inanoga kama ya nguruwe.
Mbona nguruwe pori Hana sifa hizo ulizozitaja
 
Hakuna aliewahi kupigana vita na huyu kiumbe akashinda. Tulimtafuna, tunamtafuna, na tutaendelea kumtafuna!

Hivi mnajua balaa la kitimoto rosti nyie? Upate na tubia hata tuwili tu twa kusindikizia, Aroo!
[/QUO

Nyama tamu sana hii big up pig
 
Mouthwatering for the love of pork
Chinese-red-pork-recipe.jpg
 
mambo gani ya kutiana appetite na hili baridi sasa?!ukimyaja tuu huyu jamaa medula inavurugika asee...ngoja niende kwa masaweee hapo
 
Hii ni kweli mkuu, kama banda la nguruwe ni safi lenye kivuli huwa wana eneo moja la kujisaidia.

Hata ng'ombe ni wachafu sana kama mfugani ni mchafu.
 
Kama unawajua vyema, nguruwe ni moja ya wanyama wasafi na wenye akili sana duniani. Sasa kwanini wanasifa ya kuwa wanyama wachafu sana?

Kuna mawili.
1. Nguruwe huwa hawana tezi za kutolea jasho. Wala hawawezi kupunguza joto kwa kutoa ulimi kama mbwa. Hilo linafanya wahitaji mazingira yenye kivuli ili waishi vizuri. Kama wakikosa kivuli basi watajipaka matope ili kijikinga na jua kali. Kama hamna matope hata kinyesi chao watajipaka kuepuka joto. Ni suala la survival. Nguruwe wakifugwa sehemu yenye kivuli kizuri cha miti huwa wanaonyesha usafi wao halisi. Utaona anajisaidia mbali kabisa na anapolala. Mwili wao ukiwa msafi bila matope wala kinyesi.

2. Nguruwe ni kama binadamu. Hata chakula chake ni kama binadamu. Nguruwe hana uwezo wa kula majani kama mbuzi au ng'ombe. Nguruwe wanafanana sana na binadamu. watu wanaokula watu, husema kuwa nyama ya binadamu inanoga kama ya nguruwe. Hata dawa kama Insulin au Pepsin huchukuliwa kutoka kwa nguruwe. Sasa basi chakula chake ni nafaka kama binadamu au makombo. Akikosa, atakula mizoga hata vinyesi. Hata binadamu wakizidiwa hula vinyesi vyao, mizoga, makombo na vitu vingine vichafu. So nguruwe huanza kula vichafu baada ya kukosa msosi wa maana.

Sasa. Wataalamu wanasema kuwa dini zilizoanzia mashariki ya kati(Uyahudi na Uislamu)zinakataza kula nguruwe kwa sababu hizi. Mashariki ya kati kuna joto kali huku hakuna miti ya vivuli. Muda wote nguruwe walikuwa wakijigaragaza kwenye matope na vinyesi. Wale nguruwe wa mijini walikuwa wakigombania chakula na binadamu. Wakaishia kula makombo na mizoga. Mambo haya yalionekana ni uchafu wa kupindukia. Matokeo yake wenye mamlaka wakapiga marufuku ulaji wa Nguruwe. Matokeo yake marufuku hizo zikaingia hadi kwenye dini.

My take.: Nyama ya binadamu inanoga kama ya nguruwe.
Hahahaha
Hiyo take yako hapo chini ni ya Kichawi Mkuu
 
Inategemea na mazingira pia,mfugo wowote ukiufugia mazingira machafu utakua mchafu.Banda la nguruwe likisafishwa mara kwa mara,nguruwe wenyewe wanachagua,sehemu ya pembeni ya banda kama sehemu ya kujisaidia kubwa na ndogo,na sehemu nyingine kuwa ya malazi.

Huwezi kuta wanakula kinyesi,na pale usiposafisha sehemu za kulia chakula,au ukachanganya na walichobakiza hawali,(nimefuga nguruwe).Hivyo usafi wa nguruwe au mfugo wowote hutegemea na usafi wa mtunzaji mwenyewe.
 
Back
Top Bottom