Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 4,994
- 9,625
Habari za majukumu Wakuu wa jukwaa hili,
Leo ningependa tuguse eneo linalohusu mipango miji, makazi, na uwekezaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) hapa jijini Dar es Salaam.
Kama umetumia Barabara ya Morogoro au maeneo ya Upanga, kuanzia makao makuu ya Zimamoto (Fire), kuelekea Upanga Mashariki na Magharibi, maeneo ya Muhimbili kushuka hadi kufikia Daraja la Selander, utakuwa umeshuhudia uwepo wa vighorofa vingi vya kale vya ghorofa moja tu (floor moja). Nyumba hizi kwa asilimia kubwa zinakaliwa na wenzetu wenye asili ya Asia (Wahindi).
Ukiangalia kwa umakini, majengo haya yamechoka sana, yana sura ya kale na kiuhalisia yanatia aibu yanapokuwa mbele kabisa ya barabara kuu kama ya Morogoro, katikati ya jiji linalokuwa kwa kasi. Kubwa zaidi, majengo haya yanachukua maeneo makubwa sana (prime areas) ambayo kama yakivunjwa, yanaweza kujengwa maghorofa marefu ya kisasa (High-rise apartments) zenye malls na maeneo ya burudani na mapumziko (recreational areas) kama vile parks na gardens, maeneo ya wazi kwa ajili ya michezo ya watoto, viwanja vya michezo kama mpira wa miguu, tennis na basketball , swimming pools n.k.
Hatua hiyo ingesaidia mambo makubwa mawili:
Karibuni kwa mjadala.

- Kutatua uhaba wa makazi: Kuongeza idadi ya familia zinazoweza kuishi hapo, huku NHC ikitoa makazi nafuu kwa watanzania wengi zaidi katikati ya jiji.
- Kuboresha taswira ya Jiji: Kupandisha hadhi ya jiji la Dar es Salaam kulingana na kasi ya sasa ya ukuaji wa miundombinu.
- Ni nini kinachokwaza NHC kuvunja hivi vighorofa vya ghorofa moja ili kupisha majengo marefu yenye uwezo wa kubeba mamia ya familia?
- Je, kuna changamoto za kisheria, mikataba ya zamani, au kuna ukweli wowote kwamba baadhi ya wakazi hawa wamejimilikisha kabisa hizi nyumba kiasi kwamba shirika haliwezi kuzigusa?
- Je, upendeleo au urasimu ndio unaochelewesha mabadiliko katika maeneo haya ya kimkakati?
Karibuni kwa mjadala.