Kwanini ni Mbowe na sio Lissu na kwanini CHADEMA haifi?

Tulia nikupike mnafki mkubwa wewe. Tarehe 8 April 2021 kwa vidole vyako uliandika ukimuita Lissu Rais wa mioyoya wa Tanzania. Unataka kutuaminisha kuwa Lissu ana sifa zote za kuwa Rais wa mioyo ya wa Tanzania lakini hana sifa za kuwa Mwenyekiti wa chadema. Au kwa maono yako ni rahisi kuongoza nchi kuliko kuongoza chama chenu???. Ole wako usinijibu
 
Ajabu.kwa kweli
 
Kwanini lisu mlimuamini kugombea urais ila kwa chama mnaona hafai? Mlotaka kutuuza wananchi? Wewe kwanini unamtetea san? Una maslah gani?
 
Mbb
Binafsi nakubaliana na wewe kuhusu uimara wa Mr Freeman,ila swali ni je kwa kipindi chote hicho alichokaa kwenye nafasi hiyo ameshindwa kutengeneza mtu mwingine imara ambaye anaweza kuwa mwenyekiti?na huyo mtu akafanya kazi kwa uaminifu asikiuze chama?kuna kitu hakiko sawa.
 
..ccm bila dola itabakia madarakani? hupimi mafanikio ya chama kwa kuhesabu idadi ya wabunge, au madiwani bila kupima mazingira chama kinapitia na viongozi wake..huo ushindani wa kupata wabunge na madiwani ni halali? sheria zikoje..wasimamizi wa uchaguzi wako fair? chama kinazo rasilimali kujiendesha? wanachama wanatimiza majukumu yao? Mbowe hawezi kwenda ccm sabab hawezi kusaliti jambo aliloshiriki kuliumba, bora wengine wote waondoke lkn si yeye..na huo ndio wajibu unapokuwa mwanzilishi wa jambo lolote!
 
Nakuuliza wewe muabudu mizimu, Tarehe 30 November kwa mkono wako uliandika matamanio yako ukisema unatamani Makamu mwenyekiti awe Lissu, kama toka 2004 utumishi wake ndani ya cham haukuwa sanifu kama unavyosema je kwa nini uli mu endorse kama makamu mwenyekiti? Ulikuwa una mu endorse mtu asiye na sifa?????????
 
Kwanini lisu mlimuamini kugombea urais ila kwa chama mnaona hafai? Mlotaka kutuuza wananchi? Wewe kwanini unamtetea san? Una maslah gani?
..wakati mwingine kushiriki uchaguzi ni kukijenga chama si kushinda nafasi mnayogombea!
 
Kwakweli, nimeshangaa sana kumbe Chadema tuna akili kama za CCM tu hatuna tofauti. Ni hivi Nampongeza mama samia kwa kukandamiza demokrasia maana tunamlaumu kumbe sisi tunafanya yale yale.

Watu wanasema CCM kuna machawa haya angalieni CHADEMA sasa.
Kwani ni kosa kwa yeriko kumsupport mbowe
Kama ni muhumuni wa demokrasia yeriko hama kosa lolote

Kwamba wewe unamuamini lisu mtu yeyote aliyeko kinyume chako means anamsupport mbowe ni chawa
Mbona point ya kijinga sana hii

Sio kosa lakini kwa watu aina ya Yericko ni kosa kufanya Jambo hilohilo wanalolifanya.
 
Mbowe haendani tena na mahitaji ya siasa za Tanzania za kuanzia mwaka 2019, hatoshi kuwa Mwenyekiti wa chama kuifanya CHADEMA ilete mabadiliko yoyote 2025
Lissu hafai kabisa kwa nafasi kubwa. Tofauti ya TL na Magufuli ni ndogo sana. Wote wamekaaa kidikteta na ni wabinafsi kwenye maamuzi. TL anafaa tu kuwa mtu wa kutumwa lakini siyo kiti kikubwa cha nchi. BIG NO for Tundu Lissu. Mkishindwa tuleteeni John Mnyika
 
Hesabu zitapigwa tu alichoingiza Mbowe na alichochukuwa ikiwemo michango nk.

Baada ya hesabu kama kuna hela zake Wanachama tutachanga na kumrejeshea lakini kwasasa Lissu ndie anayetufaa.
 
Ni kweli kuna uwezekano wa Lisu kutuingiza kwenye machafuko kutokana na majeraha uake ya moyo yaliyotokana na kupigwa risasi. Lakini kama machafuko hayo yataleta Katiba mpya hakuna ubaya!
..hao wa kuleta machafuko na Lissu wapo?
 
Soma uelewe..si mara zote kushiriki uchaguzi ni lengo ni kushinda hiyo nafasi, lengo linaweza kuwa kukijenga chama zaidi kuliko kushinda nafasi mnayogombea!
Yaani unalazimisha nielewe utakavyo wewe?
 
Hesabu zitapigwa tu alichoingiza Mbowe na alichochukuwa ikiwemo michango nk.

Baada ya hesabu kama kuna hela zake Wanachama tutachanga na kumrejeshea lakini kwasasa Lissu ndie anayetufaa.
..mngejua hilo Lissu angetembeza bakuli achangiwe apate gari na kina Makala..faraja za wafu hizo!
 
 
Tarehe 8 Jun 2020 (Miaka minne tu iliyopita) Uli mu endorse Lissu kama Rais ajaye, hii ilikuwa miezi minne kabla ya uchaguzi mkuu. Kama Lissu hana ufanisi huo unaotaja, je unataka kutuaminisha kuwa ulikuwa una mu endorse mtu asiye na sifa? Leo ndio nimejua kuwa waabudu mizimu nao ni wanafiki.
Kwa kifupi wewe bwana mdogo unasumbuliwa na ugonjwa unaitwa Political Amnesia tafuta tiba mapema. Na nikuhakikishie hii dhambi ya unafiki itakurudia.

 
CHAMA chochote kipo chini ya wanachama, kiongozi hawezi kuongoza kama wanachama hawapo, hivyo basi Mbowe asipewe sifa, lakini pia huo ndio wako u wake kama kiongozi.
 
Yaani unalazimisha nielewe utakavyo wewe?
..sababu unarudia rudia jambo limetolewa majibu, kushiriki uchaguzi iwe kwa mgombea au kwa chama kuna malengo mengi! usikariri lengo moja la kushiriki uchaguzi ni kushinda unachogombea..ukielewa hutalaumu kwamba kwa nini Lisu aligombea km hakuwa na sifa!
 
Huyu hana sifa za kuwa mwandishi , ni mwandishi wa hovyo kabisa
 
Kaandika Gazeti kumsifia Freeman! Uchawa mbaya sana! Uchawa ni zaidi ya kansa!

Walamba asali wameanza kutoka mapangoni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…