Kwanini ni Mbowe na sio Lissu na kwanini CHADEMA haifi?

Hoja ya mwandishi kwa ufupi ni:-
Hakuna Chadema bila Mbowe: Mbowe ni Chadema na Chadema ni Mbowe.

SWALI: Kama Chadema haiwezi kuwa hai bila Mbowe it means Mbowe akifa leo ndio mwisho wa Chadema?
..ukifahamu hatari km hizo, pigania nchi ipate katiba nzuri ambayo vyama vya siasa vitakuwa na nafasi ya kupata wanachama wenye sifa na uwezo tofauti kwa lengo la kujenga nchi, zamani kulikuwa na watu waliompinga Nyerere wengi..leo hii je, wangapi wanajitokeza hadharani kuwapinga ccm ukimwondoa Mbowe..unadhani kwa nini hawapo wengi, au km wapo wengi kwa nini wanajificha? si kweli kabisa kwamba watu wengi wanafurahishwa na vile ccm inafanya kwa nchi, lkn mbona hawaonekani hadharani? Ni gharama kubwa kuwa kiongozi au hata kusaidia vyama vya upinzani Tanzania na hivyo usidhani mtu yeyote anafaa kuongoza chama wakati wowote!
 
Watu wamepoteza KAZI wengine tumepigwa vikwazo kupoteza nafasi.Sababu kubwa ni misimamo ya kukiunga mkono CHADEMA kumbe hiki chama n mali ya mtu binafsi
Nmeumia sana kupoteza muda wangu kuwashabikia hawa wajinga,wapumbavu,wakanda na wabinafsi.
 

Nyie kina Yericko, Martin Maranja na Bonicafe Jackob na machawa wenzenu wote ni wabinafsi wa kutupwa. Kwa hiki mlichokifanya mmekipa chama cha mapinduzi ushindi mchana kweupe yani hata ccm wakitaka kusimamisha Mwijaku kama mgombea wa urais against chadema yenu ya kibinafsi na kinafko bado ccm watashinda.
Inaumiza sana sababu naichukia sana ccm, na niliwategemea nyie wahubiri wakuu wa demokrasia kuwa mna uwezo wa kuitoa ccm madarakani 2025 kama mngepigania tume huru na katiba mpya, lakini kumbe nyie hamuwezi kuishi mnacho hubiri. Hamna tofauti na wapiga debe wanaohamasisha abiria waingie ndani ya basi kisha wao wanabaki stendi.

SHAME ON YOU TO THE MOON AND BACK A TRILLION TIMES.

 
Watu wamepoteza KAZI wengine tumepigwa vikwazo kupoteza nafasi.Sababu kubwa ni misimamo ya kukiunga mkono CHADEMA kumbe hiki chama n mali ya mtu binafsi
Nmeumia sana kupoteza muda wangu kuwashabikia hawa wajinga,wapumbavu,wakanda na wabinafsi.
Inauma sana yani inauma mno.
 
Hiiii kazi umeitendea haki karibu mitandao yote umechafua hal ya hewa nina matumain madogo sanaaa na huu uchaguzi kama utakuwa wa hak na demokrasia ndan ya chadema(CCM kwenye UBORA WAKE hasa idara ya usalama) kila kit kina muda wake mbowe bila chadema inawezekana,, acha tushindane kwa hoja na kila nafsi ina kila SABABU yakufanya jambo flan katika nyakati flan
 
Atakaye chaguliwa na wengi ndiye huyohuyo.
 
Kila jambo lina wakati wake, huo muda aliohudumu unatosha na sasa kijiti kiende kwa wengine tukaribishe fikra mpya za kissable
 
Daaaaaah!! Bado sijaamini kama wewe mkuu Yeriko Nyerere ndiye uliyeandika haya.
Nilikuwa nawapuuza kila siku waliokuwa wanasema kuwa CHADEMA ni saccos ya mtu........
 
Muda ni ukuta, hata kama unampenda vipi, huu ni muda wa kupumzika awapishe wengine.
Kwani ikitokea amekufa kwa sababu naye ni binadamu itakuwaje?
 

Inatosha kwangu najua hata andiko linalofuatia hapo chini litakuwa ni point tupu juu ya msingi huu imara!
 
Sisi wanachama tutachanga hizo fedha hata kama ikichukua miaka hamsini.
..sio utachanga, mlitakiwa muwe mmechanga..kwa kila mara mkumbushwe, mnampenda Lisu au furaha yenu aharibikiwe.
 
KUTOKA KWA AFISA WA CHADEMA MAKAO MAKUU

Na, Remigius Selestine.

Tunataka Mwenyekiti mwenye kutuletea Secretariat Mpya ya Makao Makuu CHADEMA. Hii iliyozuia wanachadema wasiwe na TV yao ambapo kila mwaka CHADEMA ingeingiza Bilioni (4) nne na milioni themanini haitufai.



Mjumbe wa Mkutano Mkuu na Baraza Kuu la Chama, nisikilize Mimi Remigius nakufungua ubongo namna Chama chako kinavyoendeshwa kiajabu ajabu!

Nikiwa Mkuu wa Idara ya IT, nilikuja na wazo la kusaidia Chama kuweza kujiendesha lakini pia wanachama kukata kiu yao ya kuwa na TV CHANNEL YA CHADEMA ndani ya Kingamzi cha Zuku.

Nilitafuta Mwekezaji (Jina nalihifadhi) nikakaa nao vikao vinne ili waione fursa ya wao kuwekeza Chadema. Wazione faida watakazozipata kutoka kwetu, management ya kampuni hiyo kubwa kabisa hapa Tanzania yenye makao makuu yao Nairobi Kenya wakanielewa

Hatua zikaanza Chama makao makuu kupitia Secretariat nikawashawishi na wakaelewa Plan ya kuwa na TV ya Chadema. Nikaanda vikao kati ya Wajumbe wa Secretariat ya Chama na management ya Huyo Mwekezaji ili wakubwa hawa wasonge mbele, mimi mtumishi jukumu langu kuu likamilike.

Mwekezaji akaja Makao Makuu, aka-present namna Kazi itakavyokwenda, faida tutakazopata kama Chama na wao faida watazozipata. Mpango ukawa nikwamba kila mwezi Chadema itakusanya milioni 340,000,000 kutoka kwenye malipo ya subscribers.

Yaani kwa kila mtu mmoja akilipia kingamzi chake, Sh. 3,400 ni pesa ya Chadema na inaingizwa kwenye akaunti ya Chama. Target ilikuwa ni kuuza vingamzi na dishi lake vyenye Channel ya Chadema kwa watanzania laki moja (100,000). Kadili wanunuzi wangeongezeka vile vile pato la Chadema lingeongezeka.

Ili kufanikisha hili, Mwekezaji akasema, gharama za maandalizi hadi Chadema inaanza kuruka hewani kwenye vingamzi ni "zero cost" yaani Chadema hatutalipa hata shilingi 10, wao wawekezaji watafanya kila kitu kwa gharama zao.

Sharti pekee ambalo chadema tulipewa na tulipaswa kukubali na kusaini ni kumuhakikishia mwekezaji kuwa tutawafikia
watu wapatao 100,000 wenye uwezo wa kununua KINGAMUZI ambacho tutakileta sokoni.

Mimi, Remigius niliwahakikishia kuwa tayari ninayo mpango kazi wa namna ya kuwafikia watu Hao hususani wanachama na viongozi nchi nzima. Kumbuka nilishatembelea majimbo yote nina network ya wanachama na viongozi.

Wajumbe wa Secretariat walikubali, wakaniruhusu mimi na mafundi wa hiyo Kampuni tuanze huku maboss hawa na Mwekezaji waendelee na kazi za kiutawala za kusainiana mikataba ya kazi

Mimi pamoja na mafundi wa mwekezaji, tulianza kufunga mifumo. Tulipeleka vifaa vya kisasa kanda zote Tanzania bara na zanzibar, gharama zote ni za mwekezaji ni mamilioni yalitumika.

Yote haya tulitaka yaruke hewani kabla ya uchaguzi mkuu 2020 lakini pia tuwe na uwezo wa sisi kwa sisi kuwasiliana mikoa yote hata kama internet imekatwa. Ili Ndani ya uchaguzi mkuu kila mwanachadema na mtanzania aone kampeini zetu bila wasiwasi, na TV iruke hewani 24/7.

Nikaanza Kuandaa Mkakati wa kuwapata watu watakao pewa mafunzo ya awali ya kuandaa matangazo, tulikusudia walau kila jimbo tuwe na mtu wa IT/Afisa Habari.

Mauzauza yakaanza;

Wakati sisi watalaamu tukiendelea kufunga mifumo watu wa management na Secretariat wao wanakamilisha mambo ya kiutawala ikiwa ni pamoja kusainiana mikataba, wawekezaji wakanza kupigwa chenga .

Mikataba Chama kikagoma kusaini, Mimi nikiuliza shida ni nini na mimi nakwepwa, nikajua tayari shida ile ile ya utendaji wa jabu ajabu!

Nikaanza kuwa mkali na kutaka kujua sababu na kama hawataki si wangesema mapema bila kusababisha hasara kwa mwekezaji, nikaambiwa Secretariat imekataa kuipitisha moja kwa moja na sababu ni kuwa Wakubwa hawajaanzisha hiyo Plan, hivyo Remigius atapata sifa kwa wanachama.

Wengine wakasema eti Remigius lazima atakuwa na 10% hivyo wakazuia kazi hii muhimu isifanyike wakidhani wanamkomoa Remigius! Kumbe wanakikomoa chama na wanachama.

Nikapitia manzigira magumu sana, kumbuka Mwekezaji ameshaanza na ameshatumia gharama, chama kikanitelekeza mimi nipambane na Hao wawekezaji, hii ni 2020 mwezi June.

Leo watu wale wanataka kutuaminisha kuwa wanaweza kuendesha chama na kikawa bora, wanaweza kuwa na fikra na mawazo ya kuendesha taasisi ikajiendesha kiuchumi na wanachama wakanufaika! SAHAU! Watu wanaowaza sifa binafsi bila sifa za taasisi, wanaowaza kula bila kuingiza Sahau!

Kama unaweza kukataa uwekezaji huu, wenye kukupa fedha zaidi ya bilioni 8 kwa miaka miwili, Wenye kuwapa fursa wanachadema kwenye majimbo yote kufanya kazi na kuingiza kipato, wenye kuwapa fursa watanzania wapenda mabadiliko kuona Shughuli za Chama live kwenye Chanel yao, Kweli huyu aliyezuia anania ya dhati?

Kama wanabisha nitaachilia Mpango kazi wote, na Email zote!

Tundu Lissu Pekee anaweza kuturekebishia utendaji wa makao makuu Chadema.

#WameyatakaWatayapata
#Wasikimbie
TrueVoter
 
Muda ni ukuta, hata kama unampenda vipi, huu ni muda wa kupumzika awapishe wengine.
Kwani ikitokea amekufa kwa sababu naye ni binadamu itakuwaje?
..hakuna anayejua ratiba ya Mungu, hao walioficha mtu anaumwa alipona? lkn si wapo wanafanya yale yale zaidi hata ya yule aliyekufa!
 
sugu ni kama fahamu zimemrudia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…