Kwanini ni Mbowe na sio Lissu na kwanini CHADEMA haifi?

Aiseee sikujua kama CDM ni wajinga kiasi hiki. Kwamba mnaweza mkaaa na mkamuweka mtu ambaye hana uwezo wa kuwa Rais kugombea Urais. Kwahiyo kwa lugha rahisi unasema Watanzania waendelee kuichagua CCM kwakuwa CDM hawana mtu anayeweza kuwa Rais. Unathibitisha kuwa CDM ni chama cha kijasiriamali, wazee wa maokoto ya Ruzuku. Maskini vijana ambao wamepoteza mwelekeo wa maisha kwa kuamini wanaweza kupata mabadiliko kupitia CDM
Kwa hiyo mkuu uliamini kabisa Lissu anaweza kushida urais na kuongoza hili taifa. 😅😅😅
 
wakati mwingine kushiriki uchaguzi ni kukijenga chama zaidi kuliko kushinda nafasi mnayogombea!
 
Kimara wana-week ya pili hawana maji wote wanaccm na wanachadema wanapata joto la jiwe
 
Hiyo ni ishara ya kukosekana kwa utawala bora na mianya ya wizi na ufisadi
 
Tunamuhitaji Lissu, huwezi kuhubiri demokrasia na kujiita mdemokrasia ili hali kwenye chama chako hauishi kidemo
..jaribu hiyo demokrasia unayoitetea nyumbani kwako kwanza kabla ya kuelimisha wengine.
 
Sasa si hajafa ndugu tuanze kuongea kuhusu marehemu asiyekuwepo?
 
Andiko fikirishi sana ingawa limeandikwa kama kampeni dhahiri ya Mh Mbowe. It’s very well articulated. Hongera sana Y Nyerere.

Kwetu sisi watubaki ambao ni wadau wa demokrasia tunachohitaji ni kuwepo kwa uchaguzi makini ulio huru na wenye haki wa mwenyekiti wa CHADEMA na nafasi zote za uongozi katika chama hicho. Basi.

Mbowe, Lissu na wenye nia wote wapewe nafasi ya kugombea nafasi hiyo kwa usawa wote. Atakayepata kura nyingi za wapiga kura halali ndiye atakayestahili kuiongoza CHADEMA. Basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…