Kwanini ni Mbowe na sio Lissu na kwanini CHADEMA haifi?

Swali Kwako Ndugu Mwandishi.... Mbowe Ataenda Kufanya Kitu Gani Ambacho Hakukifanya Katika Miaka Ishirini Ya Uenyekiti Wake?
..siasa za kutaka mgombea awape ahadi ni za kilaghai, Mbowe anajua maadui wa chama chao wanapanga nini dhidi yao? Lkn lengo kuu la kuongoza chama cha siasa ni kusimamia juhudi za kutoa alternative ya sera, usimamizi wa serikali na kukosoa yasiyofaa yanayofanywa na serikali..na mengine ya aina hiyo..zaidi ya hayo unataka akupe ahadi za uongo na wewe uishi kwa ahadi za uongo ili asipofanya muanze kuzozana kwa jambo ambalo wewe hasa ndio chanzo sabb ulitaka yeye akuambie uongo!
 
Kwa uchambuzi huu,Naunga mkono Hoja
Mbowe aendelee

Hali ya zito kabwe kweli ni tete,kakimbia kamuachia mama chama
 
Kwakweli, nimeshangaa sana kumbe Chadema tuna akili kama za CCM tu hatuna tofauti. Ni hivi Nampongeza mama samia kwa kukandamiza demokrasia maana tunamlaumu kumbe sisi tunafanya yale yale.
Taratibu mkuu. Labda kuna kitu sikijui. Huyu Yeriko Nyerere ni kiongozi mwenye hadhi ya kutoa msimamo wa CHADEMA?

Mimi nimeelewa hapa kaandika kibinafsi kama mpiga debe wa Mbowe.

Haitakuwa sawa kuhalalisha udikteta wa Rais wa JMT kwetu sisi wananchi kwa mawazo ya mtu binafsi. It’ll be very unfair.

Msiokubaliana naye, andikeni kumkanusha.

Sisi watu baki tunasubiri uchaguzi huru na haki utupe kiongozi halali wa CHADEMA. Basi.
 
Hakuna double standard yoyote Lissu kutangaza nia imeonekana kama ni "uhaini" hicho ndio naona sio sawa.
..kwa nini wewe huoni attention, kelele na ushabiki nyuma ya alichosema Lisu? Hakikupi ujumbe..?
 
We
wewe jamaa kumbe ni mjinga kiasi icho, kwaiyo kwa maelezo yako marefu yasiyo na tija unamaanisha Lissu hana mchango ndani ya CHADEMA!!
Kwanini risasi apigwe Lissu na si Freeman Mbowe kama kweli unataka kutuaminisha kuwa Lissu hana mchango ndani ya CHADEMA?
Kwanza ni chama gani cha Kidemokrasia Mwenyekiti anakaa miaka 20 madarakani,kwani CHADEMA haina watu wengine wa kuongoza chama?what if akifa Freeman Mbowe,mtavunja chama?
Mkuu una heshima yako mtaani acha utoto!!
 
..kwa nini wewe huoni attention, kelele na ushabiki nyuma ya alichosema Lisu? Hakikupi ujumbe..?
Tatizo lipo ndio maana nimesema Lissu katangaza nia mbona kelele nyingi na sio mtia nia pekee , wao watie nia washindane kidemokrasia hicho ndio wanachokihubiri miaka yote kama Chadema waache gimmicks na intimidation hayo ni mambo ya CCM na fomu moja .
 
..kwa nini wewe huoni attention, kelele na ushabiki nyuma ya alichosema Lisu? Hakikupi ujumbe..?
Lisu anachokosea ni kitendo cha kumu attack mwenyekiti wake kwenye public kua kashindwa kupambana na samia

Haya anatakiwa anaongelee ndani kwa kua yeye ni mojawapo ya kiongozi mkubwa mwandamizi,tena makamu mwenyekiti.
Anafanya kosa la kuleta Mambo ya chama ya ndani,nje hata kama wana tofauti wamalizane wenyewe ndani sio ayaseme nje

Hii kiuongozi haifai,hapa lisu kakosea tena saana
 
..mchango wa anayechimba kisima na anayekuletea maji nyumbani unalingana..?
 
Mtu kugombea Umwenyekiti tena kwa njia ya demokrasia NI KURUBUNIKA?
Kwa nini msisubiri SANDUKU LA KURA ZENU LIAMUE?
Wewe ni nani kakurubuni kuandika haya?
 
..hizo kelele na ushabiki kwa Lisu ndio zinaleta ujumbe wa uwepo wa nia mbaya dhidi ya chama kupitia kwa Lisu, hata km yeye Lisu hajui!
 
Andiko murua kabisa
 
Kelele zote za kale kabibi kaajuza kanajifanya ni kapinzani kumbe ni mboga mboga
 
Naona handler wa Yeriko kabonyeza activation code…..kazi imeanza😅
 
Mbowe haendani tena na mahitaji ya siasa za Tanzania za kuanzia mwaka 2019, hatoshi kuwa Mwenyekiti wa chama kuifanya CHADEMA ilete mabadiliko yoyote 2025
Huyu chawa wa Mbowe hawezi kukuelewa.
Anamchafus Lisdu hajui kuwa tunajua Mbowe yupo kwenye payroll ya Mamdul
 
Niseme tu wewe ni CHAWA tena wa hovyo Sana
Kama we ni msomi basi ni kielelezo Cha wasomi wa hovyo mnaochelewesha maendeleo ya nchi hii kisiasa, kiuchumi na kijamii. Wasomi wa kujikomba komba Ili mpate uteuzi au tuzo
Ni kwanini kila anapotokea mtu kugombea nafasi ya Uenyekiti basi anaonekana hafai na ametumwa??
Umeelezea mabaya ya Lisu na mazuri ya Mbowe, kwa akili zako hizo Mbowe hana mabaya wala Lisu Hana mazuri?
Mbowe ameongoza CDM miaka mingi Sana , je hakuna wa kuchukua nafasi yake?
Mfano akaitwa na Muumba mtafanya nini??
Umerahisisha Sana swala la Lisu kupigwa lisasi na umekuza sana swala la Mbowe kutaka kuwa.....Mbowe ana vyuma mwilini?..au miguu ipi ilivunjwa??
Chadema hii ya Mbowe unaiona imekua au ndo inashuka kwa kulazimisha siasa zile zile mwaka nenda mwaka rudi?
Chadema Ina wabunge wangapi nchi nzima?...madiwani??...wenyeviti wa mitaa, vitongoji na vijiji??
Linganisha na 2010 na 2015?
Mbowe anahujumiwa kwa mabilioni lakini bado ana pesa za kuwekeza, kwa biashara ipi zaidi ya kutumia chamq kujinufaisha??
Mimi si mwana chama wa chadema lakini ni mpenda mabadiliko
Napokutana na watu kama wewe naihurumia sana nchi yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…