Kwanini ni Mbowe na sio Lissu na kwanini CHADEMA haifi?

Kwanini ni Mbowe na sio Lissu na kwanini CHADEMA haifi?

Ninavyoelewa uhitaji mkubwa wa Rais mpya ni kuunda mpya mfumo wa utawala na dola katika nchi yetu. Kazi hiyo Lissu angeiweza sana. Lakini hilo hitaji haliko Chadema. Chadema kinahitaji kiongozi mpambanaji lakini mwenye uwezo pia wa kuhakikisha survival ya chama chake. Hiyo kazi Lissu haiwezi.

Amandla...
Anaiweza nani?
 
Sababu ya sita inayomnyima Tundu Lissu sifa ya kuwa mwenyekiti wa Chadema Taifa ni ya kiuchumi, Duniani kwa modern politics pesa ni silaha muhimu ya kuiendesha taasisi ya kisisa, Ifahamike Chadema kwa sasa ni chama kisisa kilichotayari kushika madaraka ya nchi, Sio kikundi cha harakati, bali chama cha siasa ambacho utendaji kazi wake unahusu dialogue, convincing, and black-mailings, mambo hayo yanahitaji pesa sio maneno wala harakati, tena pesa utoe mfukono mwako kwakuwa chama chetu hakina ruzuku ya maana, milioni miamoja na hamsini ya ruzuku hata kuhudumia makao makuu tu haitoshi, hivyo lazima uwe na misuli ya uchumi ili uwalipe wataalamu niliowaeleza hapo juu. Zingatia wataalamu hao juu hawawezi kuwa wanachama wengi unawapa tenda unawalipa. Sasa Lissu kwa sasa hajarejea vizuri kwenye utumishi wake wa Uwakili nchini, anaishi kwakutegemea misaada ya wahisani hasa Diaspora, Chama kinaingi kwenye uchaguzi mkuu mwakani, itakuwa ni masihara kutegemea mwenyekiti wa aina hiyo awaingize kwenye uchaguzi kwakutegemea ruzuku ya milioni mia hamsini. Hivi tu sasa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi huu ikiwa utafanyikia Dar bajeti yake inafika Bilioni 1, na ikiwa utafanyikia Dodoma angalau bajeti inaweza kuwa milioni 800 hivi, Muulizeni Lissu anaweza kuchangia shingapi bajeti hii? Zitto kakimbia kuongoza chama chake sio kwamba anapenda bali kakimbizwa na uchumi, kakaa pembeni na remont anamwelekeza yule mama tu, Kuongoza chama lazima uwe na pesa zako mfukoni sio za mfuko wa mtu. Mimi sitampa kura yangu!
Nina bahati Mbaya sana niliwaamini Nyie wahuni kumbe mnajali Pesa tu.

Wananchi wanalilia haki zao za msingi, watu wanatekwa na kupotezwa na wengine wanapitia mateso makali kumbe wenyewe mnaangalia Ulaji tu.

Aisee Lissu amefanya jambo jema sasa panya mmeibuka na tumewajua Nia zenu.
 
Well said. Chadema ni Mbowe na mbowe ni chadema......
Mimi nilishasema Tundu lissu ni mzuri ila hayuko financially stable. Hana tofauti na Lipumba, marehemu Mrema, Mbatia, Zitto na kadhalika.
Hata wanamapinduzi wengi ulimwenguni ukiwasoma walikuwa kwanza wanahakikisha Wana nguvu ya kiuchumi kufinance hayo mapinduzi. Sio wote pangu pakavu halafu mnaongozana. Mtafika wapi.
Aanzishe chama chake halafu aone kama ni rahisi. Useless
Kwahiyo Mbowe anaweza kui finance CDM akiwa mwenyekiti tu? Hawezi kukifinance chama akiwa mzee wa CDM? Kwahiyo unasema kuwa anapenda uenyekiti kuliko anavyokipenda chama? Reginald Mengi (RIP) alikuwa ana finance CDM akiwa na cheo gani CDM?

Mnafikiria kwa kutumia nini?

Mbowe unaona vijana wako wanavyokutukanisha?
 
Yeriko upuuzwe

Huna akili kabisa
Aisee nimejifunza andiko la Yerricko sitawaamini tena hawa wahuni.

Kumbe hawana tofauti na ccm hata kidogo.

Vijana tuachaneni na Siasa za Bongo na dini.

Kijana ukitaka maisha yako yaende uwe maskini uwe tajiri bora ujikite kwenye Mademu, Pombe, Sigara. Ila sio Siasa za bongo na hizi dini za uongo.

Mimi kuanzia leo siwatilii maanani tena.

Nahamishia burudani zangu kwenye Music, connections, betting na Mpira wa simba na yanga huku angalau ntaambulia Burudani kuliko hizi dini na siasa ambazo unaambulia kutekwa hata kuawa au kupotezwa.

Nina shukuru sana Mh Lissu hatua zako zinaleta mwanga na kuokoa maisha ya vijana.
 
Well said. Chadema ni Mbowe na mbowe ni chadema......
Mimi nilishasema Tundu lissu ni mzuri ila hayuko financially stable. Hana tofauti na Lipumba, marehemu Mrema, Mbatia, Zitto na kadhalika.
Hata wanamapinduzi wengi ulimwenguni ukiwasoma walikuwa kwanza wanahakikisha Wana nguvu ya kiuchumi kufinance hayo mapinduzi. Sio wote pangu pakavu halafu mnaongozana. Mtafika wapi.
Aanzishe chama chake halafu aone kama ni rahisi. Useless
Wapuuzi nyie akina Hand to Mouth, miaka yote mnatudanganya mnapigania haki za wananchi.

Haya ana pesa 2019 uchaguzi serikali za mitaa pesa yake ilisaidia nini? 2020 uchaguzi mkuu pesa zake zilisaidia nini?

Ali kibao kauliwa, vijana Soka na Wenzake wamepotezwa hizo pesa zimeokoa nini?

2024 uchaguzi serikali za mitaa zimesaidia nini hadi watu wamepigwa risasi na wengine mapanga na wamefariki?

Then unatwambia sijui pesa? Financially stable imesaidia nini?

Kumbe wachumia tumbo tu nyie
 
Mimi nilishasema kuhusu Lissu nikapuuzwa. Nakupongeza sana Yericko Nyerere kwa kujitokeza na kumshambulia huyu adui wa demokrasia na kirusi ndani ya CHADEMA. WanaCCM tupo tayari kushirikiana na Mbowe kwenye ujenzi wa CHADEMA. Kamati kuu imchukulie hatua kali za kinidhamu Tundu Lissu.
Umeongea kama Kikwete, ni afadhali yeye asiwe Rais lakini sio Tundu Lissu kuwa mbunge.

Hapo ndipo tunaelewa kuna kitu kwa TL, Viva.
 
Kama viongozi wa CHADEMA wanawaza kwa namna hii Bora CCM iendelee kwa miaka mia
MImi ni Mwana chadema lakini andiko la Yeriko limenibunja moyo sana.

Asante Mungu umetufunulia kwamba tuliokuwa tunawaamini kumbe na wao ni Nyoka. Lao moja na ccm.

Hizo bilioni za Mbowe wanasema alizipoteza kuna mashaka alikuwa anarudishiwa kivingine kwa mlango wa nyuma.
 
Yeriko Nyerere wewe ulikuwa Mtumishi mtiifu wa hayati Membe na unaelewa kabisa Mbowe ni CCM

Waache Lisu na Mbowe wapambane kwenye Uchaguzi huru na haki utakaosimamiwa na Chama Cha Wanasheria wa Kenya

Nimemaliza 🐼
Aisee Itafahamika......mambo yote hadharani.
 
Mnadhani akiachia ngazi kwa kebehi na matusi atakuwa na huo moyo wa kuchangia CDM kama awali?

Amandla...
 
Nimeishia kusoma hapa tu, yaani leo hii Lissu aliyekua jasiri pekee kumface JPM na kuupa uhai siasa za upinzani kipindi kile cha udikteta ndio leo mnamuita anatumika na CCCM? yaani ali risk maisha hadi kupigwa risasi all that ili aje kutumika na CCM?

Nimekudharau sana hata kitabu chako nitakichoma moto, nilidhani upo intelligent kumbe ni just another Mbowe's pawn!! So embarrassing
Zitto junior usiku wa leo tare 16 Dec 2024 nimevunjka moyo sana.

Tangu asubuhi sikuwa nataka kuusoma huu uzi. Wakati napita Youtube nimeona Uburu Media inapigia chapuo hoja za Yerricko tena wanasoma Neno kwa neno Video clip zaidi ya 15min

Nikashtuka kwani Yerricko kaandika nini hadi kimewakuna Uhuru Media platiform kubwa ya CCM na Propaganda??
Ikabidi nirudi huku kuusoma.

Mungu ni Mwema sana. Hii Nchi tunapigwa na wale tunaoamini.

Mwisho wao unakaribia sio rahisi wamefunuliwa kiasi hiki.
 
Nimesoma mpaka hapo kwenye simulizi ya Abdul kupelekwa kwa Lissu na kiongozi mkubwa wa Chadema. Tukihoji kwa nin Mbowe alienda straight ikulu baada ya kutoka jela mnasema tunapenda vita hatupendi watu waelewane.
Umewaza sana kama mimi exactly.....nimefanya reflection ya Matukio yoote yaliyotokea tangu 2015 hadi 2024 nov 27.

Nina mengi yakusema siwezi kuyaandika hapa. Mungu wa Mbinguni ametufunulia, Daudi Tundu Lissu ana mkono wa Mungu.
 
Upuuzi mtupu uyo mbowe akifa na chama kitakufa tengenezeni mfumo si mtu
Mtu atapita ila mfumo utabaki
Yaani ianze taasisi alafu itengeneze watu
Shubamit
 
Yaani nawewe unasema maridhiano yakikua na faida,ilhali akina George Sanga hadi sasa wako ndani,na kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mlikatwa kutoka asilimia 98 ya wagombea mliowasimamisha hadi asilimia 34,bado unaona ni mafanikio?
Lissu alitaka hadi kuuawa kwasababu ya misimamo yake,leo eti unambeza wewe ambaye uko vuguvugu na hata sijawahi kukuona ukiwa front kwenye maandamano zaidi ya kupiga porojo mitandaoni.
Wewe itakua ni mmoja wa watu wanaotumika,unajishuhia kredit sana.
Tuseme kwamba hiki alichosema huyu Nyerere ni kweli na kwamba Tundu Lissu alikuwa amezungukwa na Nyoka tupu.
 
Kugombea Urais kuongoza watu 60m, sawa anafaa. Ila kugombea uenyekiti kuongoza watu wachache, ana nia ovu hafai. Pumbavu kabisa hili jamaa.
Hawa ndio wale wachawa wanaotaka Mbowe aendelee kwa faida ya matumbo yao
Akina Lucas na Tlaatalaa ndio.hawa akina Chiembe
 
Nchi hizi ina maajabu mengi sana, hivi Abdul ana cheo gani serikalini mpaka aweze kumlipa Lissu stahiki zake za kibunge?
Eti mfanya bishara na kiongozi mkubwa wa Chama.

Cha ajabu amewataja Abdul, Lissu, Jumbe, Huyo Kiongozi hajamtaja

Nimecheka.kwa hasira
 
Barikiwa sana kwa bandiko lililotukuka
Hakika kwa sasa kwenye upinzani wa nchi hii hakuna mtu jasiri na mwenye msimamo asiyekurupuka kama Mbowe jamaa kapita mengi sana kiasi kwamba angekuwa mwingine angeshaunga mkono juhudi au kuamua kuachana na siasa kabisa!
Mungu mbariki sana kamanda Mbowe
Alikuwa anarejeshewa hasara zake.....it was very well calculated.
 
Kwa hiyo mkuu uliamini kabisa Lissu anaweza kushida urais na kuongoza hili taifa. 😅😅😅
Hili Taifa hata Baba Levo au Juma Lokole anaweza. We kweli ndezi kama huwezi kuongoza Taifa hili.

Hili taifa hakuna mtanzania hawezi kuongoza, shida ni kupata tu hiyo nafasi.
 
Wewe ni mtumishi wa idara ya usalama wa Taifa toka ulivyotekwa 2015

Ambayo ni idara ya ulinzi wa CCM

Mnampiga Vita Lissu kwa sababu ya kulinda vibarua vyenu ukiwa na Boniface Jacob, Malissa and .com

Mwaka huu hatutakubali Bora tugawane mbao chama kife chama kuwa chini ya ccm hapana !!

Hayo mawazo ya kutaka kutuletea January makamba au Gwajima kugomea urais hatutakubali..

Watu waliokipambania chama miaka nenda miaka Rudi ndio mnawatukana tu mnavyojisikia

Mwaka huu ndio tunataka tujue kweli chadema ni chama Cha umma au ni chama Cha familia ya Mbowe?

Pigeni promotion tu lakini mwaka huu ni Lissu!! Mkateni tuanzishe chama kipya mnapambana na Mungu, Umma na wakati hamtakaa mfanikiwe wajasiliamali wa kisiasa siasa sio biashara!!


Tufanye tumekubaliana na hoja zake nyepesi,bt he Mbowe kama binadamu aliekamilika ataiongoza milele CDM,he siku akifa?inamaana kila anaetaka kugombea uenyekiti wa CDM kushindana na Mbowe mnamwita msaliti?
 
Kama sisi walokole wa GEN Z hatuwakubali wachungaji masikini, kwetu lazima mchungaji awe tajiri ili kutuhamasisha kuwa dini zinalipa....
Huyu Lissu ni masikini, na kama tija tunavyojijua masikini tuna kelele nyingi ili kupata mwanya wa kupiga dili....
Hii familia ya Mbowe ni matajiri tokea enzi ya nyerere, ndio maana CDM iko mpaka leo.....

1734303317408.png
 
Back
Top Bottom