Askari mmoja wa cheo cha juu kule Zenji jana kasikika akikemea mtu yeyote atakayebaki kituoni mara baad atu ya kupiga kura atakiona cha moto. Haya si maandalizi ya uchakachuaji wa kura kweli? Nina wasiwasi mkubwa kuwa mawakala wa vyama vya upinzani watanunuliwa na ccm na hivyo kufanya kazi yao kuwa rahisi. Jamani tayari tumeshaliwa. Hebu imagine:-
1. hotuba ya vitisho ya jk itakayotolewa mwisho wa mwezi,
2. askari kusambazwa kwenye vituo vyote vya kupigia kura wakijifanya kusimamia amani,
3. kutoruhusiwa wapiga kura kubaki ili kuchunga kura zao zisiibiwe,
4. kununuliwa kwa mawakala kwa lengo la kurahisisha uchakachuaji wa kura.
Lazima tuwe makini saaaana mwaka huu.