Elections 2010 Kwanini ni vigumu kuiba kura katika Uchaguzi Wetu - Tusitafute visingizio

Elections 2010 Kwanini ni vigumu kuiba kura katika Uchaguzi Wetu - Tusitafute visingizio

PENDEKEZO
Ili kuleta Mabadliko ya Kisiasa ni lazima tume ya Uchaguzi iandae electronic Voting system inayoruhusu mtanzania kupiga kura popote alipo..Japo kuwa Chance ya Serikali Kuchakachua Matokeo ya kielectronic ni Kubwa lakini hiyo ni DHAMBI ya serikali na mimi nitakuwa nimetimiza HAKI yangu. Mifumo hii imefanikiwa nchi nyingine na haijaleta malalamiko

Nasikitika Kwamba harakati za kutafuta Maisha zimenifanya nipoteze haki yangu ya kupiga Kura.

Haya yote siyo kweli kwa sababu hata CCM wanashangaa kinachoendelea kwa sababu walitegemea wangelishinda kilaini. Kwa hiyo, CCM hawakuwa na muda wa kupanga njama zozote zile.

Katika karatasi za kupigia kura Tanzania kamwe haziwezi kuwa na huo upuuzi wa vijikaratasi laini kwa mgombea mmoja tu..............for what?

Ikifanyika hivyo hata Mahakama Kuu itatengua matokeo hayo kwa sababu za "biasness".............Please grow up in this 21st Century......................or you will be outgrown.....................
 
Kuna mpango unaendelea wa namna ya kukinusuru chama cha mafisadi kisianguke vibaya Mkwenye uchaguzi ujuo na mbinu mbali mabali zinafanywa ili kura ziibiwe kwa gharama yoyote ile. Kuna mzee mmoja ndani ya system amenitonya kuwa ballot paper za ziwekea utaalamu kama picha ya kielelezo inavyoonyesha na mpango utakuwa kama ifuatavyo;

1. Mpango huu ni kwa KURA za uraisi tu,

2. Mpango huu utawahusu wagombea wenye nguvu ambapo kura za mgombea D zitahama kwa mgombea A unapokunja au unapo-fold ballot paper yako kwani sehemu ya kupigia kura ya mgombea D ina kikaratasi laini kilichowekewa gundi kali kwa juu ambapo ukipiga kura utaambiwa ukunje karatasi ya kura mara moja na kile kiaratasi kanahama kwa mgombea A,

3. Mpango huu utapandikia kura hizi za kughushi kwa uli mshindi apatikane kwa zaidi ya asilimia 70% bila kushitukiwa kwa weizi wa kuyra wa aina yoyote na mawakala wote kusign kuthibitisha kura zimehesabiwa kihalali

Nini cha kufanya:

Kama mpango huu utatumika kwa basi wapiga kura mnaombwa unapofika kituo cha kura bonyeza kwa dole gumbe kwenye sehemu ya mgombea D ambapo kikaratasi (very transparent with strong glue) kitanasa kidoleni mwako halafu piga kura yako na kunja karatasi bila wasiwasi wowote.

Habari ndio hiyo wizi wa namna hii umeshawahi kutumika sana nchi za kusini mwa amerika....

View attachment 15583


Pia tembelea site ya Dr. Slaa Welcome to the Frontpage - Dr. Wilbrod Slaa 2010

Ufafanuzi kidogo sijaelewa
 
Wana JF,
Habari hii ni uongo ulio waziwazi. Mfunyukuzi ametumwa na CCM ili awagribu mharibu kura zenu siku ya uchaguzi maana wanajua wananchi wengi watampa Dr. Slaa

Hii ni mbinu ya kuwadanganya mharibu kura zenu na ushindi apate Kiwete. Usidanganyike wana JF na wala msisambaze ujumbe huu kwa mtu yoyote ili watanzania wasije wakaharibu kura yao.

Ni wazi nia yake ni kuharibu kura ili wapate ushindi kiulaini.

HATUDANGANYIKI kura zote tick kwa Dr. Slaa

Hiyo ni karatasi tu,kwani nikiweka dole gumba halafu nikaweka tick nimeharibu nini?Kura inaharibika pale ambapo unapigiwa wagombea zaidi ya mmoja,au hupigi kabisa,au unapiga tick sehemu isiyohusika n.k. Lakini nikiweka gumba sidhani kama kuna madhara hapo.

Kwa sasa hivi tunachukulia kila tetesi kwa umakini......
 
Hiyo ni karatasi tu,kwani nikiweka dole gumba halafu nikaweka tick nimeharibu nini?Kura inaharibika pale ambapo unapigiwa wagombea zaidi ya mmoja,au hupigi kabisa,au unapiga tick sehemu isiyohusika n.k. Lakini nikiweka gumba sidhani kama kuna madhara hapo.

Kwa sasa hivi tunachukulia kila tetesi kwa umakini......
Umenena mwanawane lengo la kuweka gumba ni kutoa hicho kijikatatasi then unapiga kura yako ya vema kwa Dr. Slaa
 
Naungana na Mwanakijiji 100% hakuna wizi wa kura kama upo mtu aje na hoja ama mbinu za kitaalamu isiwe tunatoa hoja kama tupo kwenye vikao vya kahawa mitaani. Kwanza ijulikane kabla ya kura kuhesabiwa katika masanduku kwanza wanahesabiwa watu waliopiga kura katika daftari mfano watu 100 then masanduku yanafunguliwa na karatasi sa kura lazima zimatch na idadi ya waliopiga kura. Badala ya kulalamikia wizi wa kura inabidi kutafuta mawakala katika majimbo yote na wawe wenye upeo na uaminifu
 
Mfunyukuzi sema ukweli wasije wakakataa kuhesabu kura zetu bure kisa tumeziharibu. Je? wewe ni mwana CCM au?
 
Ukweli ni kuwa wenye hofu hii ya "wizi wa kura" ni kwamba hawajui upigaji kura wetu ulivyo na kwanini hatua zilizochukuliwa mwaka huu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi zitachangia sana kuondoa wasiwasi wa wizi wa kura. Bahati nzuri nina uzoefu wa kushiriki kama mwangalizi wa Uchaguzi Mkuu katika mojawapo ya chaguzi zetu nchini na kuweza kutembelea maeneo ya Shinyanga, Mwanza na Musoma wakati wa kampeni na wakati wa Uchaguzi kuweza kutembelea vituo vya uchaguzi zaidi ya hamsini vya Mwanza. Nimeshiriki toka kituo kinafunguliwa hadi kura zinamalizwa kuhesabiwa. Kwa hiyo, siandiki kinadharia bali kwa uhakika wa ushuhuda wangu mwenyewe ambao nina uhakika unaweza kurudiwa na mtu mwingine yoyote aliyepata nafasi kama yangu.

Ninachofanya hapa (kuelezea hili) ningependa kungefanywa na Tume ya Uchaguzi ili kuwaondoa watu wasiwasi.

Dah! Mkuu, hii makala ni ndefu kishenzi hususani kwa akina sie tunaofanyia shughuli zetu Internet cafe!!! Hata hivyo, nimei-save kwenye flash ili nikasomee ghetto ingawaje kimsingi nimepata picha ya nini unazungumza!!! In short, YOU ARE REAL ANALYST!! Mchambuzi yeyote makini huwa haegemei upande wowote anapotoa maoni yake bali anaangalia fact!!! Lakini pamoja na yote, hebu cheki kwenye red hapo juu!!! Asilimia kubwa ya wenye hofu ya kuibiwa kura ni members wa JF.

Hivyo basi, maelezo hayo yanaweza kuwa na mshiko zaidi kutolewa na wewe ( I hope most members humu, iwe wana CCM au wana CHADEMA wana-respect contribution zako) kuliko kama yangetolewa na NEC. Kwavile, kutolewa na NEC, bado wale wasiotaka kuuona ukweli wangesema NEC nayo ni walewale tu!!! Hata hivyo, sitashangaa kusikia baadhi ya wana JF wakihofu kwamba nawe tayari ushanunuliwa!!!!

Yeyote anayebisha ukweli huu, basi atoe hint, kama angekuwa yeye angeiba iba vipi hizo kura!!! Assume yeye ndie Team Leader wa uibaji wa kura!!
 
hii ni imani ilijengeka.. watu wengi najua wanaingia kwenye kituo cha kupiga kura na wanatoka lakini hawajui nini kimetokea kabla yao au baada yao. KUtokana na imani hii nadhani kwa kweli Tume ya Uchaguzi lazima itoe tamko la maelezo ya jinsi kura zinavyopigwa na nini kinapaswa kufanywa au kufanyika maana naona watu wengi kweli wanaaminii wizi hutokea kwenye kituo cha kupigia kura. Hili wazo ni la hatari.


Mkuu M, I respectfully disagree with you sir. nadhani ni wewe ndiye una imani kuwa kura haziibiwi, sisi tunajua na tumeona kura zikiibiwa. naunga mkono aliyesema kwamba majimbo uliyoyataja wasingeweza kuiba kwa sababu wangekamatwa na ingekuwa vurugu kwa sababu mwamko ulikuwa mkubwa na kura zililindwa kikamilifu. zanziba majeshi yalitumika sana na watu walipigwa na wengine walikimbilia Shimoni Mombasa.

Tena najiuliza kilichokusukuma kuandika hii "imani" yako potofu hapa. unaweza kuwa umetumwa?
 
NI muhimu tume ya Uchaguzi ikaeleza wazi ni jinsi gani mtu anaweza kuharibu kura.Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa,wakati mwingine unaweza kuharibu bila kujijua.
 
Ndugu Mwanakijiji

Wizi wa kura upo na unafanyika sana. Hayo majimbo uliyotaja ya Karatu, Mpanda kati na Pemba CCM wanashindwa kuiba kura, kwanza wananchi wake ni ngangari na pili ushindi unakuwa landslide kiasi kwamba returning officer wanashindwa jinsi ya kuchakachukua matokeo nilishuhudia haya Tarime.

Kutokana na mabadiliko iliyofanya NEC mwaka huu wizi mkubwa wa kura utakuwa wa AINA MBILI.
1. Kwanza NEC haitapeleka vifaa vya kutosha kwenye majimbo ambayo CHADEMA iko strong, hivyo wananchi wachache watapata fursa ya kupinga kura na wengi wao wakiwa CCM kwani wao watakuwa wameambiwa mapema hivyo watawahi kupiga kura zao kabla ya vifaa havijamalizika. Hayo tulishuhudia mwaka 1995 DSM, na vyuoni ambako wapiga kura wengi walikuwa wanamu support Mrema.
2. Wizi wa pili wa kura ambao umeondokeza ni ule unaoshirikisha wasimamizi wa uchaguzi na mawakara wa vyama. Kwanza lazima ufahamu wasimamizi karibu wote wa uchaguzi ni CCM. (Kumbuka Musoma sasa hivi waalimu wote wanaoshambikia upinzani wameoredheshwa ili wasipangiwe kuwa wasimamizi wa uchaguzi). ILi uweze kuiba kura ni lazima wasimamizi na mawakara wa vyama wahongwe na huu ndiyo mwanya CCM hutumika.

Mfano kuna majimbo ambayo CHADEMA haikusimamisha wagombea, na pia kuna majimbo ambayo CCM imepita bila kupingwa. Believe me katika majimbo hayo msimamizi wa uchaguzi ambaye ni CCM anaweza kuandika kura zozote anavyotaka kwasababu CHADEMA haitakuwa na wawakilishi na hayo ndiyo yakawa matokeo ambayo NEC itayatangaza because CHADEMA hawana mawakara. Na haya majimbo ndiyo yatakuwa sources kubwa ya uchakachuaji wa matokeo ya urais.

PILI katika majimbo yale ambayo CHADEMA imesimamisha wagombea na ina mawakara, kinachofanyika hapa ni kumuhonga wakara wa CHADEMA eg katika kituo kura halisi mathalani ni DR. Slaa 500. Kikwete 200 baada ya kuhesabiwa. CCM kwa kushirikiana na returning officer wanamrubuni wakara wa chadema kwa kumuonga pesa mwisho wa siku matokeo yanayoandikwa na kujazwa kwenye form ambazo mawakara wote husaini inakuwa Dr. Slaa 100 na Kikwete 600 huu wizi unafanyika tulishuhudia haya Ubungo 2005.

Ndiyo unaweza kusema hili tatizo ni la wakara wa upinzani lakini maadamu bado wananchi wetu ni masikini wizi wa aina hii utaendelea kuinufaisha CCM. Kwanza wakara anakuwa ameshatishwa kwamba hata ukikataa hizo pesa Dr. Slaa ameshashindwa tayari, hivyo wakara anaona kuliko kukosa vyote Dr. Slaa na pesa basi bora aambulie pesa.

Kuchunga vituo ni muhimu sana hasa baada wa upigaji wa kura believe me mda huo ndiyo viongozi wa serikali na CCM huanza kupita kila vituo vya kupigia kura na kugawa pesa za rushwa kwa mawakara wa vyama vya upinzani ili kuchakachuwa matokeo. Kama watakuta wananchi wengi wanalinda vituo huo ni vingumu kuingia na kugawa pesa.

KITU kimoja ninachokubaliana na wewe kilingana na uzoefu wangu ili CCM iweze kuiba kura LAZIMA iwashirikishe msimamizi wa kituo na mawakara wa vyama vya upinzani na hilo linawezekana kabisa. Kuna wanaCCM watakuwa planted kuwa mawakara wa vyama vya upinzani ili iwe rahisi kuiba kura. Vyama vya upinzani vilifanyie kazi jambo hili.
 
hivi Majjid Kikula ni nani, maana nasikia jamaa ndiyo master plan wa kuiba kura ambaye CCm wanamtegemea na siku hizi za karibuni amekuwa akionekana sana kwenye ofisi za tume ya uchaguzi.! Mwenye data zake vizuri amwanike mtu huyu hatari kwa usalama wa nchi yetu.
 
Nimepata habari za kushitua sana. Kutokana na kukubalika kwa Dr. Slaa kwa Watanzania na kutokana na tuhuma nzito ambazo amezitupia serikali ya kikwete na kutokana na mafisadi kutokuwa tayari kuachia madaraka kwa njia ya amani, Kikwete, Ikulu kwa kushirikiana na NEC wameamua piga ua lazima Kikwete atangazwe mshindi wa Uraisi. Nimeelezwa kuwa Kikwete ataapishwa kwa minajili ya Kibaki kwani Makame atamtangaza mara moja kuwa ameshinda na hivyo kuapishwa Ikulu pale pale. Wanakiri kuwa safari hii wagombea wao wengi wa ubunge watashindwa lakini hawako tayari kushindwa uraisi.

Ndugu zangu jambo ili limeniuma sana kwani inaonyesha kuwa Kikwete haamini katika demokrasia. Ni jukumu la Chadema, wanaharakati kupinga kwa nguvu zote njama hizi chafu. Nawaomba ndugu zangu tuanzishe mapambano makali sana. Si kawaida yangu kuandika uvumi lakini vyanzo vhangu ni vya uhakika na nimewasiliana na watu wa karibu wa Chadema nao wanasema wana habari hizi. Hivyo badala ya kushabikia na kufurahia kazi nzuri aliyoifanya Dr. Slaa jana kwenye mdahalo tuna kazi kubwa kuzuia kuibwa kwa uchaguzi. Naomba kuwasilisha.
 
Mpiga kura siyo muamua matokeo, muamua matokeo ni muhesabu kura.

Jiulize NEC ni wazalendo au la, utapata jibu bila wasiwasi.
 
Tusitishike na habari kama hizi. Kumbukeni mtu yeyote hawezi kutawala bila ridhaa ya wananchi, hususan katika nchi kubwa kama Tanzania. Tatizo wao bado wanajua watanzania ni mabwege lkn kama Mh Dr Mwakyembe alivyosema Watanzania si mabwege tena! Pia ni muhimu kuwaelzeza ndugu zetu, jamaa zetu wasimamie haki na usawa na wasikubali kura zao kuibiwa. Kumtangaza JK kuwa rais bila kukamilisha mahesau itakuwa vigumu sana na kumbuka ameshakosa public support. Nani zaidiya akina Membe, Moses Kulola na wengineyo ambao wamesimama na kusema wanamsapoti? NI kimyaaaa! So si rahisi kama anavyofikiri hapo bado sijagusia wanajeshi na polisi ambao hawajaridhika. Ila pia kumbuka wanaona ICC ikiwa bize huko Nairobi na wanajua they will be held accountable...
 
Hii isitukatishe tamaa na kuacha kupiga kura pamoja na ujambazi wa kura wanaotaka kuufanya.
 
Tutajuana nao kwanza piga kura. Vinginevyo nina wasiwasi wewe ni usalama wa taifa unaharibu saikolojia yetu. Kura tutapiga kwa fujo mpaka makasi yawatoke safari hii!
 
Nimepata habari za kushitua sana. Kutokana na kukubalika kwa Dr. Slaa kwa Watanzania na kutokana na tuhuma nzito ambazo amezitupia serikali ya kikwete na kutokana na mafisadi kutokuwa tayari kuachia madaraka kwa njia ya amani, Kikwete, Ikulu kwa kushirikiana na NEC wameamua piga ua lazima Kikwete atangazwe mshindi wa Uraisi. Nimeelezwa kuwa Kikwete ataapishwa kwa minajili ya Kibaki kwani Makame atamtangaza mara moja kuwa ameshinda na hivyo kuapishwa Ikulu pale pale. Wanakiri kuwa safari hii wagombea wao wengi wa ubunge watashindwa lakini hawako tayari kushindwa uraisi.

Ndugu zangu jambo ili limeniuma sana kwani inaonyesha kuwa Kikwete haamini katika demokrasia. Ni jukumu la Chadema, wanaharakati kupinga kwa nguvu zote njama hizi chafu. Nawaomba ndugu zangu tuanzishe mapambano makali sana. Si kawaida yangu kuandika uvumi lakini vyanzo vhangu ni vya uhakika na nimewasiliana na watu wa karibu wa Chadema nao wanasema wana habari hizi. Hivyo badala ya kushabikia na kufurahia kazi nzuri aliyoifanya Dr. Slaa jana kwenye mdahalo tuna kazi kubwa kuzuia kuibwa kwa uchaguzi. Naomba kuwasilisha.

Hii inathibitisha kitu kimoja kuwa Kikwete, Makame ambaye Katiba ilibadilishwa ili aendelee kuongoza NEC walivyokuwa watu hatari kwa nchi yetu. Hili ni kosa la uhaini kwa hivyo inabidi Chadema na watu wote wenye mapenzi mema lazima wapinge njama hizi za kihaini. Watanzania tuamuke.
 
Back
Top Bottom