Mwanakijiji hujui wizi unavyofanyika; ngoja tukujuze
1)Wizi wa kuwanunua mawakala katika vituo vya kupigia kura
Hapa mara nyingi zile kura za watu ambao hawakujitokeza, zote hupigiwa chama fulani kwa makubaliano ya kifedha
Kubadilisha kura zote ndani ya sanduku na kuweka nyingine zenye tiki ya chama husika
(Hapa lazima mtu kutoka nje alete hizo kura mpya na ndiyo dhana ya kuambiwa ukishapiga kura nenda nyumbani)
Kuharibu kura za chama kimojawapo kwa kuongeza tiki ya pili
Kwa kuwa katika hatua hii ni makubaliano ya wasimamizi wa kituo na mawakala, fomu zote hujazwa baada ya wizi huo kufanyika
2)Wizi wakati wa kusafirisha masanduku kwenda jimboni
Baada ya kura kuhesabiwa na mawakala kupewa nakala ya matokeo, huo siyo mwisho. Masanduku hupelekwa kwenye kata ambapo kura za diwani hujumlishwa na kutangazwa; lakini kura za rais na mbunge hazifanyiwi kazi pale, masanduku hubaki yamefungwa tu lakini hupelekwa kwa msimamizi wa jimbo kwa majumuisho na uhakiki.
Wizi hapa hutokea njiani wakati wa kuyasafirisha kwani huwa hayana wakala wa chama chochote. Mawakala mara nyingi hawakubaliwi kuyasindikiza kwa visingizio kuwa si kazi yao au gari limeshajaa masanduku.
Humo njiani, hasa usiku kura ndani ya masanduku huondolewa na kuchomwa moto na kuwekwa kura nyingine. Msimamizi wa sanduku la kituo husika hutafutwa (kwa kweli kuwa anajua mpango mzima) na kutengenezwa fomu nyingine za matokeo, na wakala wa chama husika huitwa na kuweka saini kwenye fomu mpya ya matokeo na ile ya zamani huharibiwa. Kwa saini za mawakala wa vyama vingine, huwekwa saini za kufoji.
Wakati wa kujumlisha matokeo ukifika ni wazi kutakuwa na fomu mbili tofauti za matokeo ya kituo hicho; moja ni ile iliyojazwa kituoni (ambayo huwa ndiyo sahihi) na ile ambayo imejazwa njiani baada ya kuchakachua. Kwa vyovyote vyama vitabishana juu ya fomu ipi ni sahihi, kila chama kikivutia upande wake – suluhu ni kufumgua tena lile sanduku na kuona exactly kuna nini ndani. Na kwa kuwa kura zilishabadilishwa njiani, fomu ya chama husika itaonekana kuwa na matokeao sahihi na hata kama kutakuwa na utofauti bado, kura zitakazotambuliwa ni zile zitakokuwa kwenye sanduku – zilizochakachuliwa. (nadhani umenielewa)
3)Wizi mezani: Hapa ni mabavu ya dola tu hutumika na kutangaza kuwa Fulani kashinda,Utakuta FFU na Polisi wamejaa na magari ya maji ya upupu yamewekwa standby kabla ya matokeo kutangazwa. Ukiona dalili hizo ujue kuwa dola inajiandaa kutoa matokeo yasiyowaridhisha wananchi (Hii sijui njia ya kuidhibiti)
Njia za kudhibiti wizi huo:
Kwa kuwa kila karatasi ya kupigia kura huwa ina namba, na kwa kuwa kila msimamizi wa kituo hukabidhiwa vitabu hivyo kwa namba; yafuatayo yafanyike
1)Kila chama kipate nakala ya namba za vitabu vya kupigia kura vilivyopelekwa kila kituo
2)Mawakala waelekezwe kunukuu namba za vitabu kwenye kituo kabla upigaji kura haujaanza na msimamizi awadhibitishie kuwa hivyo ndivyo vitabu alivyopokea toka msimamzi wa jimbo
3) Iwe ni lazima kwa kila wakala kusaini fomu ya matokeo kituoni na kama ana malalamiko yoyote yale ajaze kwenye fomu ya malalamiko (unajua mkiachia wa CCM pekee akasaini, hata ikijabadilishwa anatafutwa huyo mmoja anasaini na mchezo unakuwa umeisha)
4) Wakati wa kuhesabu kura, iwe vituoni au wakati wa kuhakiki katika ngazi ya jimbo (ambako huwa ndipo matokeo huwa yameshachakachuliwa), kila sanduku la kura lihesabiwe peke yake na ihakikishwe kuwa namba za karatasi zilizozomo zinaoana na namba alizokuwa amekabidhiwa msimamizi wa kituo na mawakala wawe wametoa taarifa kwa vyama vyao juu ya namba zilizotumika kwenye vituo vyao.
5) Kwa kuwa mawakala ndio wameaminiwa na vyama vyao, wayasindikize masanduku ya kura hadi jimboni pale uhakiki na utangazaji unapofanyikia. Kuyasindikiza hadi kwenye kata na kuishia hapo hutoa mwanya kwa watendaji wa kata kushirikiana na CCM kuyabadili. Sanduku lolote litakalowasilishwa bila mawakala litengwe na lihasabiwe tofauti na kama litakuwa na kura tofauti na fomu za mawakala, likataliwe - Nakumbuka hii ilifanyika Temeke wakati Mrema akigombea. Ni marufuku mawakala kusafiri tofauti na masanduku yao - magari yabebe masanduku kidogo na mawakala.
6) Mwakala wapewe elimu ya kutosha na wajue kuwa wanamuwakilisha mgombea, wasiwe tayari kununuliwa –kuna thread nzuri humu yenye kipeperushi juu ya elimu.