mawakala ndio vinara wakushiriki kuiba kura,na mwaka huu wakichagua mawakala njaa ndo wataumia sana,tena kuna mpango wa kupandikiza mawakala chama ndani ya upinzani,:A S thumbs_up:I know the perception.. wanaibaje kura? Mawakala hawahesabu kura!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mawakala ndio vinara wakushiriki kuiba kura,na mwaka huu wakichagua mawakala njaa ndo wataumia sana,tena kuna mpango wa kupandikiza mawakala chama ndani ya upinzani,:A S thumbs_up:I know the perception.. wanaibaje kura? Mawakala hawahesabu kura!
hii ni imani ilijengeka.. watu wengi najua wanaingia kwenye kituo cha kupiga kura na wanatoka lakini hawajui nini kimetokea kabla yao au baada yao. KUtokana na imani hii nadhani kwa kweli Tume ya Uchaguzi lazima itoe tamko la maelezo ya jinsi kura zinavyopigwa na nini kinapaswa kufanywa au kufanyika maana naona watu wengi kweli wanaaminii wizi hutokea kwenye kituo cha kupigia kura. Hili wazo ni la hatari.
Malafyale.. hilo tatizo halipo mwaka huu; matokeo yanatangazwa kila kituo na kila jimbo linatangaza rasmi.. hakuna haya ya takwimu za mawakala! Na as a matter of fact.. mawakala hawahesabu kura wao wanaangalia tu, sasa hawa mawakala wa Zanzibar walileta namba zao wote wakazijumlisha na zikapingana na zile za Tume ya Uchaguzi? How realiable was their tally?
Kama "wenye authority" watafanya hivyo mnachosema watafanya kwanini watu waende kupiga kura? Kama mawakala wanaweza kuhongwa kirahisi hivyo na kubadilisha matokeo wakati ni kosa la jinai kwanini watu waende kupiga kura. Maana kila ninapowasoma ninaona kuwa ni hopeless case kwenda kupiga kura:
a. NEC watamtangaza wanayemtaka
b. Kura zitaongezwa kwa wagombea wa CCM vituoni
c. Mawakal wa vyama watakatiwa kitu kidogo ili wachakachue kura
d. Kura hazitolindwa vizuri.
Kama yote a - d yana ukweli (hasa ukisoma sentiments za watu hapa), ni wazi kuwa mpiga kura wa Tanzania hana sababu ya kwenda kupiga kura. Hiki ni kisingizio cha kuwapatia ushindi CCM kirahisi, na miye nina hofu wanaokieneza wana lengo hilo kabisa.. KUWAKATISHA TAMAA WAPIGA KURA WA UPINZANI WASIPIGE KURA KWANI KURA ZAO ZITAIBWA! CCM wanajua hili. Ni lazima tukatake.. KURA HAZIIBWI NA KILA MTU AKAPIGE KURA YAKE!!!! LETS CHANGE THE MESSAGE!
mmh.. Jamani mnataka wote tuanze kuimba "kuna wizi wa kura" wakati kiakili haikubaliki hata kivitendo? Hakuna mtu hata mmoja ambaye amewahi kuonesha kura zinavyoibwa ambaye siwezi kuonesha ni kwa jinsi gani hilo atakalopendekeza haliwezekani. Nimeweka ushahidi wa kiakiil kuwa kama kuna maeneo ccm wangeweza kweli kuiba kura na walikuwa na sababu ya kufanya hivyo ni moshi mjini na karatu.. Kwanini hawakuiba?
Anayejua kura zinaweza kuibwa tanzania kituoni aseme basi nimsikilize.. I'm open minded. Ila tusiwatafutie watu kisingizio.. Ushindi na kushindwa katika hili uko mikononi mwa chadema na miye nawasupport kwa asilimia 100 kushinda lakini siyo kwa kulilia "tutaibiwa kura". Ushindi utakuja kwa kupata kura nyingi period! Now.. Go and get them! Washawishi watu wapige kura, wasihi watu waichague chadema n.k lakini hilo la wizi ... Miye kwa kweli simo..
Obvious mbinu iko Rahisi Hayo Majimbo yalikuwa au yana wabunge/wagombea wakweli na wachapakazi... so this tell us that what matters is putting competent aspirants. Wizi wa Kura ni Strategy ya CUF ambayo ilishindwa all the way. CHADEMA yaweza iga kama inaona it is a working strategy.naomba tuchukue muda kumwelewa mwanakijiji, anauliza mbona kila mara moshi mjini cc, wanashindwa kuiba kura? Mbona kwa zitto walishindwa? Mbona tarime walishindwa. Kilichofanyika huko mwaka 2005 na katika uchaguzi mdogo ndicho kinachotakiwa kufanyika mwaka 2010 na hoja ya kura kuibiwa itashindwa kufanya kazi. Hebu tujiulize ni nini kilfanyika katika majimbo hayo ambayo chadema ilipata ushindi?
Anachosema mwanakijiji ni kuwa...Jukumu letu watanzania ambao tumejiandikisha kupiga kura ni kwenda kutumia haki yetu ya kupiga kura siku ya Jumapili tarehe 31 Oktoba; Period!
Hofu ya kuibiwa kura iliyopo miongoni mwa wanajamii ni kubwa na ndio itakayopelekea wananchi wengi waliojiandikisha kukata tamaa ya kupiga kura. Kuna watu wengi sana, hususan vijana ambao walikosa kujiandikisha, kwa kuwa waliona hamna maana yoyote ya kufanya hivyo kwani kwa mtazamo wao hata wangejiandikisha na baadaye wakapigia kura vyama vya upinzani, CCM itashinda tu (kwa hofu hiyo hiyo ya kuibiwa kura)
Na sasa kuna baadhi ya wengi waliojiandikisha wameshaanza kuwa na hofu ya kuibiwa kura na kuona kwamba hata siku ya uchaguzi ukifika hawataenda kupiga kura kwani CCM itashinda tu, na hata kama watapigia kura upinzani, CCM wataiba kura na kuwa washindi.
Hii hofu ni mbaya na ndio maaana Mwanakijiji anasema kazi yetu sisi tuliojiandikisha ni kwenda kupiga KURA siku ikifika.
offcourse this was your main message na umesomeka vizuri.
Si vizuri kurudia mambo lakini ndani ya ccm kauli waliyonayo ni ushindi ni lazima. Kama 'great thinker' chama tawala kinapoweka kauli mbiu ya namna hiyo maana yake ni nini? Nini maana ya lazima?
Pili baadhi yetu ni wazoefu wa namna kura zinavyoibwa....tumekaa kimya muda mrefu kwenye hili tusionyeshe kura zinaibwa vipi ili tuendane na makusudi mema ya kupiga kura na kutimiza wajibu wetu.
Ni kweli kabisa wakati huu hata ukweli wa mambo unaweza kutumika vibaya na mdudu mtu akapita bila kupingwa.....hivyo umesomeka vyema mm...tukapige kura kana kwamba hakuna uchakachuaji.
Nakubaliana na wewe kwamba tuache mjadala wa uchakachuaji.....lakini elezea hilo........ Isipokuwa unapodai kuwa watu waelezee wizi unatokeaje...kukaa kimya haimaanishi hatujui....lakini kama unaturuhusu tutaweka hapa vizuri na kurejea matokeo mbalimbali ya kweli na tutakupa sababu kwa nini karatu na kwingineko inakuwa vigumu wakati ubungo na kawe huwa ni kama kumnyatia kiziwi.
Na pia jaribu kutafuta maana ya neno 2010 hatudanganyiki uone kwa nini shimbo alilazimika kuingilia kazi zisizomuhusu....
jamani, matokeo ya kura yakibadilishwa mtu anaweza kwenda kufungua kesi kwani masanduku yale hayatupwi. Kwamba kuna uwezekano wa kuwa na ukiukwaji wa taratibu hilo lawezekana lakini massive rigging sasa hivi nimesema ni "ngumu mno"... Tusiwatishe watu kuwa kura zao zitaibwa. Kura wakapige kwa wingi kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuzuia uwezekano wa wahalifu kuchakachua upigaji kura.