minda
JF-Expert Member
- Oct 2, 2009
- 1,068
- 67
ni wazi hili suala la wizi wa kura ( rigging of election results) lipo mfano
inavyoonekana upande wa serikali unakuwa na 100% ya wizi wa kura na upinzani 0% ya ushindi na hapo kwa sababu ya wizi wa kura na hapo ndipo 'busara' inapotumika to save the nation.
tumekuwa tukishuhudia usaliti kwa upande wa upinzani kwa kurudi au kujiunga na chama tawala wakati wa mchakato wa kufikisha majina ya wagombea kwa kila chama. chama tawala kimekuwa kikituhumiwa kuwaghilibu wapinzani japo nacho kimekuwa kikikanusha malengo hayo.
hoja inayojengwa imelala kwenye hiyo ya ghiliba; kwamba kuna uwezekano kwamba kwa kuwa chama tawala kina uwezo mkubwa wa kifedha, kama inavyoonekana kwenye uwezo wake wa 'kuvasha' akina mama, vijana na akina baba kwa sare zilizosambaa nchi nzima, kinaweza kuwa nunua mawakala wa upiga ji kura na hivyo , wizi wa kura ukafanikishwa kwa nadharia hiyo.
hivyo, ni wazi wizi wa kura upo na kuna uwezekano katika hayo wanayodai wakuu wengi ikafanyika na ndio maana mimi nalikataa kwa nguvu zote suala la kulinda kura siku ya uchaguzi kwa kuwa hiyo, kwa mtazamo wangu, ni wajibu wa moja kwa moja wa wakala wa upigaji kura.
- kenya
- zimbabwe
- zanzibar
- ongezea...