Kwanini nikimtamkia mtu baraka zinakuwa kweli ila nikijitamkie mimi hazikubali?

Kwanini nikimtamkia mtu baraka zinakuwa kweli ila nikijitamkie mimi hazikubali?

Mwab Evelina

Member
Joined
Jan 24, 2025
Posts
12
Reaction score
34
Binadamu Mungu ametupatia karama kubwa Sana na tofauti Sana.

Mimi huwa nikimtamkia mtu mema lazima yatokee.

Mfano Mimi ni Jobless sijapata Ajira Ila mpaka sasa nimewatafutia wengi sana Kazi na wamepata mpaka huwa najiuliza huu ni uwezo wa aina gani.

Yawezekana kitu kilichomo ndani yangu ni kikubwa Sana kiasi cha kufika hatua ya mimi kuwa na uwezo wa kuwabariki watu na wakabarikiwa. Ila Mimi nikashindwa kujibariki.
 
Njoo tufungue kanisa tuzile sasa!
 
Inabidi uombe sana! Una karama nzuri..sasa karama yako isiwe unawafanikishia wengine wainuke na wakatajirike wakati wewe upo hapo hapo Huo huwa sio mpango wa Mungu.
Ingia kwenye maombi Mungu akufungue kuna sehemu imefungwa kwako.
 
Kila kitu ni Imani ... Kila baraka au maombi unaowaombea wengine ni lazima Imani ihusike! ... Sasa kujikita katika kuielezea Imani Iko hivi ... kulingana na Biblia

Imani ni kuwa na UHAKIKA wa mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana .... Yaani Imani ni kuwa na UHAKIKA utapata kazi ambayo Bado hujapata.

Note nimeandika kwa maandishi makubwa UHAKIKA.

Hiyo ni tafsiri ya Imani! Lakini je chanzo Cha hiyo Imani ni Nini?

Kurudi kwenye swali lako ni hivi Imani unayotumia kuwaombea wengine na kuwatamkia baraka si Imani sawa utakayotumia kujiombea wewe!

Fanya uchuguzi katika hili! Ukiwa unaowaombea wengine au kuwatamkia baraka unakuwa huna hofu wala wasiwasi

Lakini ikifika swala la kujiombea wewe Sasa!

All in all ... Ni IMANI
 
Back
Top Bottom