Kwanini nikivaa jezi za Arsenal na Yanga warembo wanakuja wenyewe kunipa namba za simu?

Kwanini nikivaa jezi za Arsenal na Yanga warembo wanakuja wenyewe kunipa namba za simu?

Nakumbuka nilikuwa Form I enzi hizo... shabiki lia lia wa Yanga! Kama kawaida, Jmosi fulani nimetoka zangu home naenda taifa kucheki mtanange...

...siikumbuki ulikuwa ni wa timu zipi lakini bila shaka moja wapo ilikuwa Yanga!

Basi bhana...

...ile nafika jirani na Indoor Stadium, nikaona kipande cha gazeti! Nikainama na kukiokota! Enzi zile nilikuwa naokota na kusoma kila ninachokiona! Nina mashaka ikiwa kweli silka hii nimeiacha kwa sasa!

Kipande hicho cha gazeti hakikutoa fursa ya kufahamu ni gazeti lipi, wala tarehe ya kuchapwa kwake! Hata hivyo, ni zamani sana, kwahiyo huenda ikama ama Uhuru, Mzalendo au pengine Mfanyakazi!

Gazeti, ama kipande hicho cha gazeti kilikuwa kinazungumzia timu inayoitwa Arsenal! Ilikuwa ndo mara yangu ya kwanza kuisikia...

...kama nilivyosema, ni zama zile ambazo hata tv zilikuwa bado; labda kwa kina Sheikh Yahya na wenzake, ingawaje home ilikuwepo just for VHC!

Habari ile ilikuwa ni yenye msisimko kweli kweli kwa upande wangu!

Habari iliyokuwa ikieleza udugu kindaki ndaki uliopo kati ya timu hiyo ya London na Dar es salaam Young Africans! Ni raha iliyoje kugundua una ndugu Ulaya!!

Hapo hapo nikayagawa mahaba yangu ya dhati kwa ndugu yangu huyu wa Ulaya! Hadi matangazo ya tv yanaanza kuingia na kuanza kufuatilia soka la UK, ndipo nikaja kumfahamu kwa sura ndugu yangu huyu Mzungu!

Ikawa ikifungwa Yanga chakula hakinogi, akipigwa Arsenal maji hayashuki!

Uzuri, Arseno ile ilikuwa Arseno kweli kweli... Arseno iliyokuwa inaunda ukuta wa Timu ya Taifa ya Uingereza! We acha tu! Sa' unakosaje kwa mfano kuongeza mahaba kwa ndugu wa aina hiyo!!

Leo hii natamani ningemfahamu Mwandishi wa habari ile ili nikamkabili kokote kule aliko na hatimae anieleze kwanini kaniletea mahangaiko yote haya!

Mshenzi yule sijui uzushi ule aliutoa wapi hadi akaja kutusababishia magonjwa ya moyo ya vipindi! Na ujinga wa haya mambo, ukiingia hutoki! Kama ngiri na baridi, au bangi na jua kali!!

Sema duniani kuna Misukule lakini hii ya Liverpool imerogwa na ikarogeka hasa!!! Uzuri hawa nimeanza kuwachukia tangu nipo primary kwa sababu tu kuna Mapaka ya Kariakoo yalikuwa yanijiita eti Liverpool ya Msimbazi... Jinga sana!

Sa' hivi nyie madogo wa 1990's to 2000's ilikuaje hadi mkaambukizwa haya mashipa?! You're U-30, halafu eti shabiki wa Liverpool!! We bhana hata kuoa itakuwa umeingia chaka tu, naapia!! Na kama demu basi hata kuvutia am sure huvutii... mademu wazuri hawana muda wa ku-handle stress!!!
U-30 wanaoshabikia liver po hawapo, kama wakiwepo kibongo bongo ni 1%
 
U-30 wanaoshabikia liver po hawapo, kama wakiwepo kibongo bongo ni 1%
Acha utani ndugu yangu!! Ushabiki wa soka Bongo tunarithishwa ujue!! Aliye U-30 ina maana babake yupo kwenye 50's!

Hawa wa 50's ni wale ambao Liverpool ilikuwa moto usiozimika kwa fire extinguisher wala "intinguisher" na ndo maana licha ya kwamba alisugua benchi kwa miaka kadhaa, lakini bado ni ManU pekee ndie kamzidi mataji ya soccer league champions!

Sasa hawa wazee wa 50's wapo waliowarithisha mashipa watoto wao! Lakini kwa upande mwingine, licha ya kukosa mataji LP bado ni club maarufu sana duniani, ni maarufu pengine kuliko hao wanaobeba mataji, na ndo maana bado ni moja ya vilabu tajiri sana, sio tu UK bali duniani, huku akiwaacha hata wao watwaa mataji wa Premier League!

Huo ni ushahidi tosha kwamba bado LP ina ushawishi mkubwa kwenye ulimwengu wa soka licha kutofanya vizuri, uzuri kwa kuangalia level zake!
 
Sawa
 
Back
Top Bottom