Kwanini nikivaa jezi za Arsenal na Yanga warembo wanakuja wenyewe kunipa namba za simu?

U-30 wanaoshabikia liver po hawapo, kama wakiwepo kibongo bongo ni 1%
 
Kwani kupewa number ni dhambi?
La pili ni hili;
Inzi huufuata mfuko wenye uchafu ndani.
 
U-30 wanaoshabikia liver po hawapo, kama wakiwepo kibongo bongo ni 1%
Acha utani ndugu yangu!! Ushabiki wa soka Bongo tunarithishwa ujue!! Aliye U-30 ina maana babake yupo kwenye 50's!

Hawa wa 50's ni wale ambao Liverpool ilikuwa moto usiozimika kwa fire extinguisher wala "intinguisher" na ndo maana licha ya kwamba alisugua benchi kwa miaka kadhaa, lakini bado ni ManU pekee ndie kamzidi mataji ya soccer league champions!

Sasa hawa wazee wa 50's wapo waliowarithisha mashipa watoto wao! Lakini kwa upande mwingine, licha ya kukosa mataji LP bado ni club maarufu sana duniani, ni maarufu pengine kuliko hao wanaobeba mataji, na ndo maana bado ni moja ya vilabu tajiri sana, sio tu UK bali duniani, huku akiwaacha hata wao watwaa mataji wa Premier League!

Huo ni ushahidi tosha kwamba bado LP ina ushawishi mkubwa kwenye ulimwengu wa soka licha kutofanya vizuri, uzuri kwa kuangalia level zake!
 
Sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…