Kwanini nikiweka Mafuta kwenye hii sheli yanakaa sana? Kuliko nyingine

Naomba tuelewani vizuri kupitia huu Uzi utajifunza mambo mengi sanaaa kuhusu Fuel

1.Total na puma wanauza mafuta ambayo ni Unleaded. Unleaded ni mafuta yanayochanganyiwa vimiminika uitwa addictives ambayo ni Methane na Benzene ii addictives inaipa mafuta nguvu kufanya uchomaji wa mafuta uwe mdogo tofauti na mafuta mengine yanakuwa sio makali kwa hiyo caburator inakuwa inabugia mafuta

2. Mafuta huletwa kwa bulk na muagiza na serikali sasa kila fuel station inakuwag na utaratibu kwasababu unleaded n bei wanafanyag kuchanganya na vimiminika vingine Ili yawe mengi n kupata faida za juu sas apo ubora wa mafuta unapotea

3. Petrol kuchanganywa na mafuta ya taa. Ila kwasasa Ii imepungua kutokna na serikali ya magu kugundua Ili mafuta ya petrol yalikuwa yanachanganywa na mafuta ya taa Ili yawe mengi fuel station ipate faida ya juu na ndo magufuri kupandisha mafuta ya taa Ili kudiscourage ichi kitendo

N. B petrol ikichanganywa na mafuta ya taa na kuongezewa kimiminika kiitwacho alkanes (paraffins), cycloalkanes (naphthenes), and aromatic hydrocarbons. Hufanya mafuta kuchanganyikan na mtumiaji ambaye sio great thinkers kutojua maan inapoteza halufu na nguvu ya mafuta ya taa kuwa na harufu Kali ya petrol na Ii ufanywa na fuel stations nyingi sana isipokuwa Total pamoja na puma tuuuu

4. Janjaa janjaaa katika vituo vya kuwekea mafuta vituo vingi vimeset mashine kias kwamba uwez kugundua kma unaweka kweny gari ukisoma digital pale inasoma 20 litre kumbe kuna litre 3 zimewekwa pembeni bila wew kujua ndo maan kuna Sheri baadhi ukienda na dumu kuna pump maalumu kwajili ya vidumu kuepuka kuumbukaa

5. Kutokuwa makini na wauhudumu hawa waudumu sio wakuwaamini kabisaaa mi uwa nawakubari sanaaa madereva bajaji wakifika wanazima na kushukaaa wanawekewa mafuta na kuhakiki sometimes unamwambia mafuta ya laki na nusu anaweka ya laki na 20 so kwa kuwa unakuwa na haraka ata risit upati au anakwambia subir pale tuweke roller mara mashine ya inazingua omba risit pia akiki

6. Sas wafanya kazi wengi wa total na puma uongo Bure uwa hawana janjaaa unatak ya 60k unawekewa 60k kwerie

Mwisho ukiangalia takwimu Total ndo alipewa tuzo ya muuzaji wa mafuta Bora Tz 2022 ushauri wa Bure ukikosa total kaweke Puma over kwasababu gari hasa Eurepean car wanakushauri kuweka mafuta masafi ambayo n unleaded Ili kuzuia nozzel pipe zinazopeleka mafuta kwenye caburator

Nini kifanyike ingali nimeweka mafuta kwa muda mrefu ambayo yamechakachuliwa cha kwanza tumia mafuta ad taa ya mafuta iwake then nunua fuel injector zipo za diesel na petrol uwe makini nenda kaweka mafuta yako ya kutosha kaweke unleaded maisha yanasongaaa uajachelewa bado hivi vituo vingine waachien boda wanaweka mafuta ya elfu 3 mara aende uku ya elfu 2 ana cha kupoteza
 

Mkuu unaongea facts, Puma na Total naona hawana janja janja kama kampuni zingine hata wese lao ni clean.
 

Ahsante kwa elimu.
 
Nimejaribu kusoma kwanza wachangiaji wengine naona hakuna aliejibu sahihi.

Nakujibu kama mdau wa mafuta. Mafuta yote huagizwa pamoja hata unaweza kuta kituo ni cha Oryx lakin mafuta yamechukuliwa depot ya Engen sababu yaliisha au depo zimeazimana au kuuziana.

Sasa Shida inaweza kua kwenye pump au staff sio waaminifu au vyote. Yaan inawezekana Pump haiko well calibrated (imechezewa).

Lakin pia kuna wale pump attendant ambao ikija bodaboda ikaweka mafuta labda ya alfu 5 Kisha ukaja wewe wa alfu 30 basi pump hairudishi ianze mwanzo ndo akuwekee, anaunga hapo hapo. Unajikuta umewekewa ya 25 alfu but umelipa alfu 30 na risiti unapewa.

Kuna kampuni umezitaja hapo attendant wake ndio wanaongoza kwa hiyo michezo. Nikienda kwao nashusha kabisa kioo nione anavyorudisha nyuma (ku-zero) kabla ya kuanza kuniwekea.

Lakini pia inawezekana ni imani yako tu na labda Geographical Position ya hivyo vituo. Yaan Cha mbali vs Cha karibu.
 
Ili uweze kua sahihi katika uchunguzi wako inabidi ufanye calibration ya Mafuta kila kituo kwa njia kama tatu hivi kama ifuayavyo.

1) Dumu,
Chukua Dumu la lita 5 chukua boda ikupeleke kila "Sheli" waambie ununue labda ya alfu 10 kila moja uone kama yanalingana. Bodaboda ni Ili uwadanganye kua umeishiwa mafuta gari limekuzimikia njian maana lasivyo watajua unawachunguza watakukataa.

2) Empty your Tank.
Nunua madumu ya kulingana ujazo uweke mafuta kila kituo uyaweke ndani ya gari. Tembea yakiisha record kilometers zake Kisha tia Dumu la pili pima hivyo hivyo. Utaweza kujua Dumu la "Sheli" ipi limeenda kilometers nyingi. Hapa ni mpaka izime kabisa ndio utapata jibu. Kuna wamiliki hawapendi kuzimikiwa na gari labda pump inaharibika.

3) Full your Tank
Jaza mafuta full tank. Tembea hata kilometers 30 Kisha kajaze tena "Sheli" mojawapo. Mafuta yatakayojazwa kurudi kua full tank ndio sawa na kilometers 30 ulizotembea. Rudia hilo zoezi la kujaza kila after 30km kwa vituo vyote vitatu uone kama yanalingana. Utacheki wapi umejaza mafuta mengi kuliko kwengine.

Assumption ni uendeshaji wako uwe constant. Sio mara kwengine uende mkoa kwengine Dar hapa hapa, kwengine hewa ya Mungu kwengine utumie AC
 

Umeandika uzi mrefu mrefu ila hueleweki. Watu washafanya research wakajua mafuta ya Total/Puma yanakaa sana na pia ni mafuta bora.
 
Umeandika uzi mrefu mrefu ila hueleweki. Watu washafanya research wakajua mafuta ya Total/Puma yanakaa sana na pia ni mafuta bora.
Hujaelewa sababu hujataka kuelewa,
Kaweke mafuta Puma Sinza Kijiweni kama yatakaa.
 

Petrol station yangu ya uhakika ni TOTAL basi
Zingine naweka kwa dharura tu

Nawaamini saana Total mpk nmechukua pre-paid card

So nkifika kituoni nachanja tu fasta,uhakika

 
Kaka hii pre-paid card inakuaje? Naomba abc kidogo

Hii ni kama credit card

Unaweka pesa kene card

Then katika petrol station yeyote ya total tanzania utakuwa na uwezo wa kufanya yafuatayo:
-kuweka mafuta
-car wash
-car service mfano lubricants
-services from zile coffee shop zao
 
Una hoja nzuri ila tafuta namna nzuri ya kuiaddress
 
Umeandika uzi mrefu mrefu ila hueleweki. Watu washafanya research wakajua mafuta ya Total/Puma yanakaa sana na pia ni mafuta bora.
Uzi auna content ata kidogooo
 
Hahahahah Total gani hio ambayo mafuta yanakaa sana? 😀
 
Hii ni kama credit card

Unaweka pesa kene card

Then katika petrol station yeyote ya total tanzania utakuwa na uwezo wa kufanya yafuatayo:
-kuweka mafuta
-car wash
-car service mfano lubricants
-services from zile coffee shop zao

Ukitumia hii card kuna discount unazopata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…