Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,156
Kwanza nitasikitika kwasababu naipenda nchi yangu hivyo Kama mzalendo na agent wa maendeleo siwezi kufurahi kuona nchi yangu inadumaa kwa kukosa mawazo mbadala.
Pili nitafurahi wapinzani makini wakikosa wabunge ambao miaka yote ndio wamekuwa wasemaji wakubwa wa shida za wananchi lakini wananchi hao hao wamekuwa nyuma kuwatetea wasemaji wao hata pale wanapoonewa hadharani.
Mtoto anayemjali Mzazi wake hawezi kuvumilia anaposhuhudia Mzazi wake anadhalilishwa hadharani bila sababu.
Nitafurahi pia kwasababu tangu upinzani uanze kuminywa nchini imekuwa sala yangu kuu kwamba wakae pembeni kidogo ili raia waonje utamu wa nchi hii kutawaliwa bila mawazo mbadala. Labda somo likiwa kwa vitendo litaeleweka kirahisi zaidi.
Nitafurahi tena ili CCM wajionee uhalisia wa nini wapinzani walikuwa wanasaidia na kipi walikuwa hawasaidii katika ku push maendeleo ya nchi hii.
Binafsi naamini Kuna mkakati mahususi wa kuwaondoa wote ndiomaana wameanzia kwa Mbowe.
Laana ni kwa wote waliokubali kwa akili zao timamu kuhusika kupindua matokeo hasa hasa walimu wanaolia shida kila siku lakini kwasababu ya posho ya kusimamia uchaguzi wamesahau vilio vyao na kukubali kuwa sehemu ya kupindua meza.
Labda tukikaa miaka hii mitano bila kelele za wapinzani tutajua ubaya na uzuri wao.