Uchaguzi 2020 Kwanini nitasikitika na kufurahi kwa pamoja wapinzani wa kweli wakikosa mbunge hata mmoja?

Uchaguzi 2020 Kwanini nitasikitika na kufurahi kwa pamoja wapinzani wa kweli wakikosa mbunge hata mmoja?

Huna hulijualo kaa kimya..watu wanaambiwa fanya juu chini chama kipite sasa hapo unategemea nini.
Hao wasimamizi wa vituo wanayao moyoni ila watafanyeje aliekupa kazi ndio ashasema lakufanya..
Usiamini kila unachokiona,zakuambiwa changanya nazako.
Nasema haya kwakuwa nimeshuhudia mimi mwenyewe wala sikuambiwa..
Sasa si ukatoe ushahd
 
Yote kwa yote, laana ni kwa wote waliohusika kupindua meza ya matokeo
Nani kapindua meza ya matokeo mkuu? watanzania sio wajinga, hatukuwa na upinzani isipokuwa vibaraka vya mabeberu, hakuna kitu kilinikera kama akina Zitto na Mbowe waliyokuwa wakiyafanya dhidi ya Taifa katika kipindi cha Corona, na waadhibiwe kisawasawa.
 
Acha tufanikiwe sasa maana hayo mabeberu tumeyatoa yote
 
Naendelea kusisitiza japo watakuwa wamekosa kazi Kama chanzo halisi cha mapato kwao, ila binafsi niliwahi kutamani wanasiasa wote wa upinzani wakae pembeni wawaachie hao wanaccm wanaodhani nchi ni yao ili akili zitukae sawa kwanza
Hujajifunza ya Zanzibar? CCM hawaogopi kususiwa.
 
Kwanza nitasikitika kwasababu naipenda nchi yangu hivyo Kama mzalendo na agent wa maendeleo siwezi kufurahi kuona nchi yangu inadumaa kwa kukosa mawazo mbadala.

Pili nitafurahi wapinzani makini wakikosa wabunge ambao miaka yote ndio wamekuwa wasemaji wakubwa wa shida za wananchi lakini wananchi hao hao wamekuwa nyuma kuwatetea wasemaji wao hata pale wanapoonewa hadharani.

Mtoto anayemjali Mzazi wake hawezi kuvumilia anaposhuhudia Mzazi wake anadhalilishwa hadharani bila sababu.

Nitafurahi pia kwasababu tangu upinzani uanze kuminywa nchini imekuwa sala yangu kuu kwamba wakae pembeni kidogo ili raia waonje utamu wa nchi hii kutawaliwa bila mawazo mbadala. Labda somo likiwa kwa vitendo litaeleweka kirahisi zaidi.

Nitafurahi tena ili CCM wajionee uhalisia wa nini wapinzani walikuwa wanasaidia na kipi walikuwa hawasaidii katika ku push maendeleo ya nchi hii.

Binafsi naamini Kuna mkakati mahususi wa kuwaondoa wote ndiomaana wameanzia kwa Mbowe.

Laana ni kwa wote waliokubali kwa akili zao timamu kuhusika kupindua matokeo hasa hasa walimu wanaolia shida kila siku lakini kwasababu ya posho ya kusimamia uchaguzi wamesahau vilio vyao na kukubali kuwa sehemu ya kupindua meza.

Labda tukikaa miaka hii mitano bila kelele za wapinzani tutajua ubaya na uzuri wao.
Mkuu, mawazo yangu yote na siku zote nmemwomba mungu CCM ibaki pekee ili angalao au labda watz waonje machungu ya chama kimoja.Machungu ya kukosa mtetezi kule bungeni. Naamini kuanzia kesho tutaanza kulia na kusaga meno pamoja.NA MUNGU AMESIKIA KILIO CHANGU.
 
Hao wapinzani makini wapo wapi? Nadhani huu upinzani tulikuwa nao unahitaji kubadilishwa na kuja aina nyengine mpya ya upinzani ambao utakuwa na hoja zenye nguvu na wenye msimamo wenye kueleweka wanachokipinga na sio upinzani unaotegemea tu hasira na chuki walizozijenga kwetu dhidi serikali .

Maana sasa tuna upinzani ambao haushauriki wala kukosoleka,wao wanatuaminisha kila kitu kibaya na makosa hufanywa na ccm tu ila wao kwa sababu ni upinzani basi kila kitu kwao ni perfect.
 
Kabisa mkuu, wapumzike wajipange upya
 
Acha iliweeee hamna jinsi, ngoja tukomae kivyetu nchi ina wenyewe na ni CCM
Mbona unajitenga bila kutenga sasa, kuikosa dola sio kesi maana hata waliopata wangekosea hesabu wakaikosa wangetulia tuu.
Siasa sio chuki sisi sote ni watoto wa mamatanzania.. Sasa tusimame, tushikane kujenga nchi yetu.

Maendeleo hayana vyama mkuu
 
Mbona unajitenga bila kutenga sasa, kuikosa dola sio kesi maana hata waliopata wangekosea hesabu wakaikosa wangetulia tuu.
Siasa sio chuki sisi sote ni watoto wa mamatanzania.. Sasa tusimame, tushikane kujenga

Mbona unajitenga bila kutenga sasa, kuikosa dola sio kesi maana hata waliopata wangekosea hesabu wakaikosa wangetulia tuu.
Siasa sio chuki sisi sote ni watoto wa mamatanzania.. Sasa tusimame, tushikane kujenga nchi yetu.

Maendeleo hayana vyama mkuu
Ayaa vizuri maendeleo hayana chama, ila 2025 msije sema hapa kulikuwa na mpinzani ndo maana hamna hichi. tusubilie Tanzania ya Dubai
 
Ayaa vizuri maendeleo hayana chama, ila 2025 msije sema hapa kulikuwa na mpinzani ndo maana hamna hichi. tusubilie Tanzania ya Dubai
Upinzani ni muhimu sana kwa afya ya taifa ila vyama vya upinzani Tanzania ni dhaifu mnooo. Vimechangia sana kulemaza na kupotosha hata hicho wanachokiita demokrasia
 
Back
Top Bottom