Kwanini nje ya wachaga ni nadra kukuta kampuni kubwa za watanzania wengine wa asili ?

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
Watanzania wa asili – Hawa ni watu wa makabila ya kienyeji ya Tanzania kama Wanyamwezi, Wazaramo, Wasukuma, Wachaga, Wahaya, n.k.

Hili suala halina chembe yoyote ya kikabila maana ni uhalisia kama ilivyo kwa wafugaji waliofanikiwa sehemu kubwa ni wasukuma na wamasai, nikisema sehemu kubwa ya wenye makanisa waliotajirika ni wanyakyusa ni uhalisia sio ukabila, nikisema sehemu kubwa ya waliotajirika kwenye mbao ni wakinga ni uhalisia sio ukabila

Nchi yetu imejaa rasili mali nyingi sana na shida nyingi zinazohitaji kutatuliwa lakini makampuni mengi yanamilikiwa na watanzania au wageni wenye asili za kihindi, kiarabu, wakenya, n.k.

Tukija kwa upande wetu bado tunasua sana ila at least wachaga kidogo wamo lakini kwa dhati kabisa niseme katika ngazi ya taifa bado hawafui dafu kwa wahindi, waarabu, n.k.

Hivyo solution ni kuongeza nguvu kwa jamii nyingine, sina maana ya kusema makabila mengine hakuna kabisa wenye makampuni makubwa, wapo lakini ni moja moja au hakuna kabisa.

Makampuni nayosemea ni kama mashirika ya ndege, Makampuni ya utalii, Uchimbaji, n.k, sio kampuni ambazo mtu ana cheo kikubwa serikalini anawapa ndugu zake tenda kiupendeleo

Tatizo nini ?
 
ITV ni kampuni kubwa?
itakuwa wewe ni mtoto wa 2000 umezikuta channel nyingi za TV

Kampuni inaitwa IPP Media ndani yake kuna Itv, EATV (Zamani channel 5), Radio one, Magazeti ya Nipashe, n.k.

Radio one na Channel 5 (Zamani iliitwa eatv) wamesaidia sana kuisambaza Bongo Flava ndani na nje ya nchi

Mmiliki alikuwa Reginald Mengi (RIP), ndie Mtanzania wa asili pekee aliewahi kuingia kwenye top 10 ya matajiri wa nchi
 
Changamoto kubwa ni mchakato wa ufanikishaji, urasimu kwa wazawa inaweza kuwa ni mkubwa sana.
Kampuni, kiwanda , au taasisi huanzia chini kabisa na kukuwa kadri ya mazingira yanapokuwa rafiki.
Unfortunately vikwazo vinakua vingi kwa wazawa ndio maana ni wachache sana .
 
itakuwa wewe ni mtoto wa 2000 umezikuta channel nyingi za TV

Kampuni inaitwa IPP Media ndani yake kuna Itv, EATV (Zamani channel 5), Radio one, Magazeti ya Nipashe, n.k.

Radio one na Channel 5 (Zamani iliitwa eatv) wamesaidia sana kuisambaza Bongo Flava ndani na nje ya nchi

Mmiliki alikuwa Reginald Mengi (RIP), ndie Mtanzania wa asili pekee aliewahi kuingia kwenye top 10 ya matajiri wa nchi
Unamjua ally mafuruki???
 
Sasa

Ndiyo maana nikasema umetoka Useri jana...ndiyo unaona hiyo ni kampuni kubwa. Ulimwengu wako umeishia hapo kwenye ITV!

Hivi unaijua Songoro Marine?
Au unamjua Ali Mafuriki? Unajua kampuni alizoanzisha?
 
Sasa

Ndiyo maana nikase a mmetoka Useri jaamna...ndiyo unaona hiyo ni kampuni kubwa? Ulimwengu wako umeishia hapo kwenye ITV!

Hivi unaijua Songoro Marine?
Au unamjua Ali Mafuriki? Unajua kampuni alizoanzisham
Kwanza kabisa, hao uliowataja kina Marehemu Ally Mafuriki tunatambua michango yao lakini kwa Reginald Mengi ile ilikuwa ni level nyingine, kawa inspire hao kina Mafuriki

Pili hao uliowataja ndio mifano mizuri ya kuwekwa kwenye makundi ya watanzania wengine wa asili ambao jamii zao ni mtu moja moja au hakuna kabisa
 
itakuwa wewe ni mtoto wa 2000 umezikuta channel nyingi za TV

Kampuni inaitwa IPP Media ndani yake kuna Itv, EATV (Zamani channel 5), Radio one, Magazeti ya Nipashe, n.k.

Radio one na Channel 5 (Zamani iliitwa eatv) wamesaidia sana kuisambaza Bongo Flava ndani na nje ya nchi

Mmiliki alikuwa Reginald Mengi (RIP), ndie Mtanzania wa asili pekee aliewahi kuingia kwenye top 10 ya matajiri wa nchi
Acha ukabila ndugu yangu

Zuku unaijua vp kuhusu radio free Africa, star tv na kiss FM hizo siyo kampun za wazawa?
 
Ya
Sasa

Ndiyo maana nikase a mmetoka Useri jaamna...ndiyo unaona hiyo ni kampuni kubwa? Ulimwengu wako umeishia hapo kwenye ITV!

Hivi unaijua Songoro Marine?
Au unamjua Ali Mafuriki? Unajua kampuni alizoanzisham
Yaan huyu huenda hata majizo wa efm hamjui yaan hata diamond na wasafi yake hamjui jaman yaan hata mwenye crown naye pia hamjui yeye anajua wachaga tu
 
Back
Top Bottom