Kwanini nje ya wachaga ni nadra kukuta kampuni kubwa za watanzania wengine wa asili ?

Kwanini nje ya wachaga ni nadra kukuta kampuni kubwa za watanzania wengine wa asili ?

Watanzania wa asili – Hawa ni watu wa makabila ya kienyeji ya Tanzania kama Wanyamwezi, Wazaramo, Wasukuma, Wachaga, Wahaya, n.k.

Hili suala halina chembe yoyote ya kikabila maana ni uhalisia kama ilivyo kwa wafugaji waliofanikiwa sehemu kubwa ni wasukuma na wamasai, nikisema sehemu kubwa ya wenye makanisa waliotajirika ni wanyakyusa ni uhalisia sio ukabila, nikisema sehemu kubwa ya waliotajirika kwenye mbao ni wakinga ni uhalisia sio ukabila

Nchi yetu imejaa rasili mali nyingi sana na shida nyingi zinazohitaji kutatuliwa lakini makampuni mengi yanamilikiwa na watanzania au wageni wenye asili za kihindi, kiarabu, wakenya, n.k.

Tukija kwa upande wetu bado tunasua sana ila at least wachaga kidogo wamo lakini kwa dhati kabisa niseme katika ngazi ya taifa bado hawafui dafu kwa wahindi, waarabu, n.k.

Hivyo solution ni kuongeza nguvu kwa jamii nyingine, sina maana ya kusema makabila mengine hakuna kabisa wenye makampuni makubwa, wapo lakini ni moja moja au hakuna kabisa.

Makampuni nayosemea ni kama mashirika ya ndege, Makampuni ya utalii, Uchimbaji, n.k, sio kampuni ambazo mtu ana cheo kikubwa serikalini anawapa ndugu zake tenda kiupendeleo

Tatizo nini ?
Mwazo niliposoma kichwa cha habari niliona kana kwamba kimejawa na ukabila, lakini baada ya kusoma maelezo yote nimekuelewa, mkuu. Kuna jambo la kujifunza hapo.
 
Kweli wewe hujui unalolisema. Zanzibar maisha expensive sana uliwah kusikia wapi sehem ina maisha expensive hela ikawa ngumu kupatikana?
Maisha expensive kwa Watalii wanaokuja kulala kwenye Hoteli zao na Wazanzibar hawana utamaduni wa kuspend, Zanzibar Maisha siyo Magumu kama unafanya kazi na kazi za kule siyo za Professional kazi nyingi ni za Vibarua vya ujenzi na za hotelini mishahara yao laki tatu tu kwa mwezi, na kule Zanzibar Wenye Mahoteli ni Wazungu na Wazanzibar kwenye sekta ya Utalii wao wanachopata ni kuwa Masuplier wa Samaki na matunda na bora bora tu. Tofauti na Tanganyika kweye Sekta ya Utalii hatupo nyuma, Wazanzibar wapo Nyuma sana kwenye Mambo ya uwekezaji sehemu nyingi wamewekeza Wageni wao wanebakia kurogana tu.
 
Ukileta ukabila ni spana Tu nimeappreciate comments za wadau wengi walikemea ukabila kwa nguvu zote
 
Maisha expensive kwa Watalii wanaokuja kulala kwenye Hoteli zao na Wazanzibar hawana utamaduni wa kuspend, Zanzibar Maisha siyo Magumu kama unafanya kazi na kazi za kule siyo za Professional kazi nyingi ni za Vibarua vya ujenzi na za hotelini mishahara yao laki tatu tu kwa mwezi, na kule Zanzibar Wenye Mahoteli ni Wazungu na Wazanzibar kwenye sekta ya Utalii wao wanachopata ni kuwa Masuplier wa Samaki na matunda na bora bora tu. Tofauti na Tanganyika kweye Sekta ya Utalii hatupo nyuma, Wazanzibar wapo Nyuma sana kwenye Mambo ya uwekezaji sehemu nyingi wamewekeza Wageni wao wanebakia kurogana tu.
Hujui unachokisema mkuu pita kule..
 
Back
Top Bottom