Kwanini nje ya wachaga ni nadra kukuta kampuni kubwa za watanzania wengine wa asili ?

Kwanini nje ya wachaga ni nadra kukuta kampuni kubwa za watanzania wengine wa asili ?

Hivi unaijua mapembelo kago ya wakinga?
Ninaijua vizuri sana, Ni kampuni ambayo ilikuwa inaelekea kuzuri lakini sijui wamepatwa na nini, kuelekea mwishoni mwa mwaka jana nilikuwa naona mitandaoni malalamika ya mizigo haifiki, mizigo inachelewa, n.k. nini kinaendelea ?

Post ya mwisho kwenye ukurasa wao wa Instagram ni ya mwaka jana maana comment nyingi watu wanalalmika
 
Kwanza kabisa, hao uliowataja kina Marehemu Ally Mafuriki tunatambua michango yao lakini kwa Reginald Mengi ile ilikuwa ni level nyingine, kawa inspire hao kina Mafuriki

Pili hao uliowataja ndio mifano mizuri ya kuwekwa kwenye makundi ya watanzania wengine wa asili ambao jamii zao ni mtu moja moja au hakuna kabisa
Sasa point yako ni nini? Hoja ya Wachagga tu kuwa ndiyo wanaweza kuanzisha kampuni kubwa haina mantiki
 
Sasa point yako ni nini? Hoja ya Wachagga tu kuwa ndiyo wanaweza kuanzisha kampuni kubwa haina mantiki
Naomba urudi post ya mwanzo soma uelewe, inavyoonekana umesoma kichwa cha habari tu,

Hao wachaga wenyewe bado wapo wachache wenye makampuni sio kuwasifia wamefika mbali sana, tunahitaji kuunganisha nguvu watanzania wa asili maana hali ni mbaya, wageni wengi wame dominate
 
Wachaga ni wafanya biashara wazuri ila huna hoja zaidi ya chembechembe za ukabila boss.
Hapo ukabila upo wapi, ni sawa nikisema wafugaji waliofanikiwa ni wasukuma, wamasai, n.k. huo ni uhalisia sio ukabila

Nikisema wachungaji walioweza kupiga pesa nyingi ni wanyakyusa huo ni uhalisia sio ukabila
 
Hapo ukabila upo wapi, ni sawa nikisema wafugaji waliofanikiwa ni wasukuma, wamasai, n.k. huo ni uhalisia sio ukabila

Nikisema wachungaji walioweza kupiga pesa nyingi ni wanyakyusa huo ni uhalisia sio ukabila
Mkuu, umetumia data gani kama si hisia za kiukabila? umepata wapi data za uzawa za midirectors wa makampuni ya raia wa hii nchi? Tunajua zipo BRELLA ila ni taarifa confidential mno.
 
Watanzania wa asili – Hawa ni watu wa makabila ya kienyeji ya Tanzania kama Wanyamwezi, Wazaramo, Wasukuma, Wachaga, Wahaya, n.k.

Nchi yetu imejaa rasili mali nyingi sana na shida nyingi zinazohitaji kutatuliwa lakini makampuni mengi yanamilikiwa na watanzania au wageni wenye asili za kihindi, kiarabu, wakenya, n.k.

Tukija kwa upande wetu bado tunasua sana ila at least wachaga kidogo wamo lakini kwa dhati kabisa niseme katika ngazi ya taifa bado hawafui dafu kwa wahindi, waarabu, n.k.

Hivyo solution ni kuongeza nguvu kwa jamii nyingine, sina maana ya kusema makabila mengine hakuna kabisa wenye makampuni makubwa, wapo lakini ni moja moja au hakuna kabisa.

Makampuni nayosemea ni kama mashirika ya ndege, Makampuni ya utalii, Uchimbaji, n.k, sio kampuni ambazo mtu ana cheo kikubwa serikalini anawapa ndugu zake tenda kiupendeleo

Tatizo nini ?
Je wewe unayo kampuni kubwa 🤣🤣🤣🤣
 
itakuwa wewe ni mtoto wa 2000 umezikuta channel nyingi za TV

Kampuni inaitwa IPP Media ndani yake kuna Itv, EATV (Zamani channel 5), Radio one, Magazeti ya Nipashe, n.k.

Radio one na Channel 5 (Zamani iliitwa eatv) wamesaidia sana kuisambaza Bongo Flava ndani na nje ya nchi

Mmiliki alikuwa Reginald Mengi (RIP), ndie Mtanzania wa asili pekee aliewahi kuingia kwenye top 10 ya matajiri wa nchi
Wewe bwana wewe!
 
Changamoto kubwa ni mchakato wa ufanikishaji, urasimu kwa wazawa inaweza kuwa ni mkubwa sana.
Kampuni, kiwanda , au taasisi huanzia chini kabisa na kukuwa kadri ya mazingira yanapokuwa rafiki.
Unfortunately vikwazo vinakua vingi kwa wazawa ndio maana ni wachache sana .
Kuna familia nyingi za watanzania wa asili zina connections serikalini ni ngumu kuwekewa vikwazo wala kuhangaishwa kwenye process za kufungua viwanda, taasisi, kampuni, n.k.
 
Back
Top Bottom