Kwanini nje ya wachaga ni nadra kukuta kampuni kubwa za watanzania wengine wa asili ?

Hivi unaijua mapembelo kago ya wakinga?
Ninaijua vizuri sana, Ni kampuni ambayo ilikuwa inaelekea kuzuri lakini sijui wamepatwa na nini, kuelekea mwishoni mwa mwaka jana nilikuwa naona mitandaoni malalamika ya mizigo haifiki, mizigo inachelewa, n.k. nini kinaendelea ?

Post ya mwisho kwenye ukurasa wao wa Instagram ni ya mwaka jana maana comment nyingi watu wanalalmika
 
Sasa point yako ni nini? Hoja ya Wachagga tu kuwa ndiyo wanaweza kuanzisha kampuni kubwa haina mantiki
 
Sasa point yako ni nini? Hoja ya Wachagga tu kuwa ndiyo wanaweza kuanzisha kampuni kubwa haina mantiki
Naomba urudi post ya mwanzo soma uelewe, inavyoonekana umesoma kichwa cha habari tu,

Hao wachaga wenyewe bado wapo wachache wenye makampuni sio kuwasifia wamefika mbali sana, tunahitaji kuunganisha nguvu watanzania wa asili maana hali ni mbaya, wageni wengi wame dominate
 
Wachaga ni wafanya biashara wazuri ila huna hoja zaidi ya chembechembe za ukabila boss.
Hapo ukabila upo wapi, ni sawa nikisema wafugaji waliofanikiwa ni wasukuma, wamasai, n.k. huo ni uhalisia sio ukabila

Nikisema wachungaji walioweza kupiga pesa nyingi ni wanyakyusa huo ni uhalisia sio ukabila
 
Mkuu, umetumia data gani kama si hisia za kiukabila? umepata wapi data za uzawa za midirectors wa makampuni ya raia wa hii nchi? Tunajua zipo BRELLA ila ni taarifa confidential mno.
 
Je wewe unayo kampuni kubwa 🤣🤣🤣🤣
 
Wewe bwana wewe!
 
Kuna familia nyingi za watanzania wa asili zina connections serikalini ni ngumu kuwekewa vikwazo wala kuhangaishwa kwenye process za kufungua viwanda, taasisi, kampuni, n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…