Kwanini NSSF isiwe na tawi la bank kusaidia wateja wake?

ZALEMDA

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Posts
1,956
Reaction score
2,225
Mikopo ya bank muda mwingi haisaidii sana watumishi wa umma au sekta binafsi kwa sababu ya riba kubwa.

Sasa kwa sababu watumishi huwa ni wateja wa kudumu wa mfuko huu na kila mwezi wanachangia fedha nyingi, kwa nini NSSF isiwe na bank ambayo itatumika kuwapa mikopo wateja wake kwa riba ndogo sana ili kuboresha kipato cha wateja wake?

Asanteni
 
wakitengeneza mfumo inawezkana..
Hakuna kischowezekana kama mipango ingekua hivyo ila kila chombo kina majukumu yake. Pension funds wana wajibu na kazi zao na banks wana wajibu na kazi zao.
 
Jukumu kuu la nssf sio kutoa mikopo
Jukumu Lao ni lipi sasa kama hawawezi kuboresha Maisha ya wateja wake na kukuza uchumi wa nchi kwa kutoa mikopo nafuu kwa wateja wake?
 
Hakuna kischowezekana kama mipango ingekua hivyo ila kila chombo kina majukumu yake. Pension funds wana wajibu na kazi zao na banks wana wajibu na kazi zao.
Hizo bank Nyengine watawakopesha wafanyabishara na watu wengine lakini Bank ya NSSF ni kwa wafanyakazi tu. Nakwambia wakifanya hivi Maisha ya wafanyakazi yataboreka vizuri sana.
 
Jukumu Lao ni lipi sasa kama hawawezi kuboresha Maisha ya wateja wake na kukuza uchumi wa nchi kwa kutoa mikopo nafuu kwa wateja wake?
Kama ni kutoa mikopo hata hizo bank zinaweza kutengenezewa mfumo nimefanya hicho mtoa maada anachotamani. Ni swala la maboresho kwa maendeleo tuu
 
Hizo bank Nyengine watawakopesha wafanyabishara na watu wengine.lakini Bank ya Nssf ni kwa wafanyakazi tu.nakwambia wakifanya hivi Maisha ya wafanyakazi yataboreka vizuri sana
Nadhani kuwa na product ya watumishi wenye pension nssf kwenye bank ni rahisi pia kuliko kufungua bank mpya ya nssf
 
We
Kama ni kutoa mikopo hata hizo bank zinaweza kutengenezewa mfumo nimefanya hicho mtoa maada anachotamani. Ni swala la maboresho kwa maendeleo tuu
Wewe unafikiri bank hizi za biashara zina moyo huo wa kuwarumia wafanyakazi kwa kuwapa mikopo nafuu wafanyakazi?

Nikupe mfano mzuri wa NHIF,wanakopesha madawa na vifaa kwa hospitali .nakwambia riba yap ndogo sana kiasi kwamba unajisikia raha mstarehe.
 
Hahahaaaa.inaonekana wewe muoga sana.usifungwe mdomo ndugu.tunawajibu wakuikosoa au kuishauri serikali lakini kistarabu
ukishaandika unafkir wanajua kma ulkuw unaandika huku unatabasam. 🙂
 
Jukumu kuu la nssf sio kutoa mikopo

Hilo ndio jibu sahihi mkuu lakini bahati mbaya sana watu hawajui kuwa NSSF ni inatumika tu kama kitega uchumi cha kunenepesha mfuko wa serikali kama vile TRA anavyofanya
 
Sidhani kama umenielewa nilichokiandika .kabla ya kuropoka ulitakiwa usome kwanza.

Nimesema bank hiyo ingeweza kutoa mikopo nafuu kwa wateja wake.sijasema mikopo bure.tumia akili kujibu hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…